Mafunzo Matatu Kutoka Kwa Viwavi


Mwanasayansi wa kifaransa John Henry Fabre  alifanya jaribio kwa kutumia viwavi. Alichukua viwavi akaweka kwenye sahani, huku kiwavi mmoja akiwa amemgusa kiwavi mwingine. Viwavi hawa wakawa wametengeneza mzunguko kamili. Akachukua chakula pendwa cha viwavi na kukiweka katikati yao, ikiwa ni sentimeta chache sana kutoka pale walipokuwa. Wale viwavi walianza kuzunguka kwa kufuatana, kiwavi mmoja akimfuata kiwavi wa mbele yake. Masaa ishirini na nne yalipita viwavi wale wakizunguka kufuatana,  siku mbili zikapita na siku ya tatu zikafika huku viwavi wale wakizidi kuzunguka kwakufuatana. Mwisho wa siku wale viwavi walikufa kutokana na  uchovu uliokuwa unaambatana na njaa.
Hahahha leo hii nimeamua nikuandikie kisa hiki sio tu kwa sababu napenda kujifurahisha kuandika bali kuna somo kubwa sana ambalo linatokana na jaribio hilo hapo

SOMA ZAIDI: Hii Ndio Kozi Inayofundishwa Katika Vyuo Vyote

FUNZO LA KWANZA, USIISHIE TU KUZUNGUKA BALI JIULIZE KWA NIN UNAZUNGUKA
Kuna watu  wanapita katika maisha wakizunguka huku na kule. Anafanya kitu kwa sababu tu rafiki yake, anafanya. Anaenda kufanya biashara kwa sababu tu rafiki yake naye anafanya au kwa sababu aliskia kwamba biashara ile ina hela. Je, wewe unayo sababu ambayo inakusukuma wewe hapo kwenda kufanya hiyo kazi? Viwavi ambao tumewaona hapo juu ni kioo cha watu wengi sana ambao wao wanapita katika maisha kwa kufuata mkumbo wa watu. Muda wote hakikisha kwamba unajiuliza kwa nini unazunguka? Kama unaamua kufanya kitu hakikisha kwamba unajiuliza swali kwa nini unafanya kile kitu?  Dunia yenyewe inazunguka jua kila sekunde ila ina sababu. Tena sababu kubwa sana. Mojawapo ya sababu ikiwa ni kwamba mimi na wewe tuweze kupata majira mbali mbali ya mwaka. Dunia hii haishii tu hapo bado inaendelea kujizungusha kwenye mhimili wake, lengo kubwa sana likiwa kwamba watu tupate usiku na mchana.  Kama dunia inayo sababu ya kuzunguka kwa nini wewe usiwe na sababu ya kufanya kazi uanyofanya? Kwa nini na wewe usiwe na sababu ya kuzunguka kwenye mhimili wako? Fikiria nje ya kumi na nane!!
SOMA ZAIDI: Nimezaliwa Mshindi; Mawazo—->hisia—–>matendo—->matokeo
FUNZO LA PILI, TATIZO SI RASILIMALI ZILIZOPOTEA

Dunia hii ina kila aina ya rasilimali. Rasilimali zipo kila mahalii zikiwa zimetuzunguka. Hivyo hata siku moja usije ukaanza kusema, sina hiki au sina kile. Badala yake jiulize je, ni rasilimali gani hapa karibu naweza kutumia kwa haraka? Je, ni rasilimali gani ambazo zitanifanya mimi niiishi siku hii ya leo?
Viwavi walikufa kwa njaa, sio kwa sababu hawakukwa na chakula. Bali kwa sababu hawakuangalia pembeni kuweza kuziona rasilimalilz zilizopo. Hali hii inaonesha ukweli wa maisha ambao unawakumba watu walio wengi sana. Watu ambao wanapita katika maisha wakilia njaa, wakilia njaa ya pesa, wakilia njaa ya muda. Ingawa vitu hivi vyote vipo katika mazingira  vimewazungukuka ila hawataki kuvitumia.
Rafiki yangu wewe hupaswi kuwa mmoja wao.
FUNZO LA TATU, MAISHA BILA MALENGO NI MAISHA BILA MWELEKEO

Kama unataka uishi maisha magumu sana hapa duniani, basi ishi maisha ya viwavi. Yaani ishi maisha ambayo haujui unaenda wapi na kwa nini unaenda kule. Utaishia tu kuzunguka huku na kule. Lakini kama kiwavi kimoja wapo kingekuwa na sababu za kwa nini kinazunguka, nina hakika kwamab kisingekufa kwa sababu ya njaa. Hii ndio kusema kwamba kingekuwa kinajua kwa nini kinazunguka. Kingepangilia ratiba yeka na kila kitu. Hali hii ndio inaonesha umuhimu mkubwa sana wa malengo. Hii ndio kusema kwamba kila siku, kila wiki , kila mwezi kuna watu ambao tunawapoteza. Na awatu hawa tunawapoteza kwa sababu tu ya kutokuwa na malengo. Wanapotea kwa sababu tu wanatumia muda mwingi sana kuzunguka bila kujua waendako. Je, wewe unajua unapoenda?

SOMA ZAIDI; Vitu Viwili Vinavyozuia Watanzania Kufikia Malengo Yao
Wewe Ni Zaidi ya ulivyo sasa.
Tukutane kwenye meza ya wanamafanikio.
Tukutane kwenye mzunguko wa wanamafanikio

Kujiunga na kundi la wasp la HAZINA YETU BONYEZA HAPA

Ndimi
Coach Godius Rweyongeza
godiusrweyongeza1@gmail.com
www.songambeleblog.blogspot.com


Ili kupata kitabu cha KUTOKA SIFURI MPAKA KILELENI  BONYEZA HAPA

Bonyeza hapa ili uweze kupata makala maalumu kila wiki.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X