NAAM! KIPENGA KIMEPULIZWA


Duniani hapa kumeshuhudiwa mitanange mingi sana ya mpira tangu dunia imekuwepo mpaka leo hii unaposoma makala haya. Mitanange hii si ya mipira ya ligi kuu ya vodacom au ligi kuu ya ulaya tu bali pia kuna mitanange ya michezo mingine ya maisha.
Kuna mechi ambazo huwa zikichezwa, kwa hakika huwa zinavutia sana. Sio tu kwamba mechi hizi huwa zinavutia wachezaji bali pia huwa zinavutia hata wadhamini kutoka maeneo mbali mbali. Sio hilo tu, kwa watu ambao huwa hawapati nafasi ya kuwa kiwanjani huwa wanafurika kwenye nyumba za sinema na kumbi mbali mbali za kuonesha mitanange hii. Hakika, hii huwa inatia moyo na inavutia na huonesha kwamba mechi inayoenda kuchezwa ni ya kipekee.
Kitu kimoja ambacho huwa kinanivuta sana ni yale majigambo ya wachezaji na mashabiki wa timu za mpira husika. Kila upande huwa unasema utashinda. Ukimwuliza mchezaji atakwambia timu pinzani tayari imelala chali. Huku ukiongea na shabiki atakwambia sisi tunaye mchezaji fulani, yaani huyo ni balaa sana.
Kwa hakika maneno haya ukiyasikia huwa yanakuvutia masikioni (hata kama wewe sio shabiki wa mpira kama mimi) kufuatilia na kutaka kujua matokeo yake yatakuwaje mwisho wa siku. Kwa Tanzania mechi ambayo huwa inavuta sana na kukonga nyoyo za watu tunayo moja ambayo binafsi naifahamu. Nayo ni mechi ya yanga na simba.
Siku ya siku muda wa mechi huwa unafika na kipenga kupulizwa. Wahenga wanasema “hayawi hayawi Sasa yamekuwa”.  Yale majigambo, maneno mengi na vitu vingine kedekede huwa vinaamrishwa na kipenga, lakini pia dakika 90,za uwanjani ndizo huwa zina usemi kuliko maneno ya mashabiki na wachezaji wenyewe.
Naam kipenga sasa kimepulizwa! Tupo sasa dani ya mwaka 2018, tukiwa na dakika 90 za kucheza. Mwaka jana 2017 ulijigamba sana. Ulisema “unajua Mimi mwaka kesho nitatimiza 1,2,3″. Sasa uwanja ni wako. Na dakika 90,ni hizo zipo mbele yako. Kile kipenga ulichokuwa umesubiria kimepulizwa na mashabiki wanayo hamu ya kukuona wewe ukiweza kucheza vizuri sana mechi hii ya 2018. Yaani mashabiki wanataka kusikia ukisema hii ni mechi ya nyumbani na nipo uwanja wa nyumbani. Wanataka kusikia maneno yanayosema kwamba utamfunga mpinzani wako wiki nzima (magoli saba). Kiufupi mashabiki wanataka matokeo makubwa sana. Je, upo tayari? Umejipangaje kuhakikisha unaleta ushindi nyumbani? Utatumia mbinu gani?
Mashabiki hawataki tu kusikia ukiwaambia kuwa kwa mkapa hatoki mtu, bali wanataka kuona waziwazi mtu akiwa hatoki kwa mkapa.
Sasa kwa kuwa kipenga kimepulizwa hapa nakuibia mbinu nne muhimu zitakazokufanya ufunge magoli ya murua ndani ya 2017. Hizi ni mbinu zitazokufanya ung’ae wakati wengine wanalalamika. Wakati wengine wanasema refa hajatenda haki wewe utakuwa unang’aa na kupiga chenga zenye maana ukielekea golini huku wengine wakishangaa. Wegine wataongezea kwa kusema refa kakupendelea. Na pengine wapo watakaosema sasa vyuma vimekaza lakini kwako hii itakuwa grisi yenye maana kubwa sana. Yaani hii itakuwa grisi ya kukuvusha 2018 ukiwa umefaulu kwa kiwango kikubwa sana. Na hii ndio njia nzuri sana ya kumfanya refa akupendelee ndani ya 2018.
1. WEKA MALENGO 2018.
Kama unataka kushinda mechi hii ya 2018 weka malengo sasa hivi. Je, ungependa kufunga magoli mangapi? Je, unahitaji akina nani kwenye timu yako? Je, unamjua atakayekupasia mpira? Kama unataka kuanzisha biashara mwaka 2018 utahitaji kujiuliza maswali kama hayo hapo. Kitu kikubwa na muhimu zaidi unapaswa kujua kwamba tayari kipenga kimepulizwa na hivyo wewe uwe tayari kuicheza mecho hii. Haya ni baadhi ya maswali ambayo unaweza kujiuliza kwenye biashara 2018. Je, ninaenda wapi? Ninaenda na nani? Kwa nini ninaenda huko? Weka Malengo ya biashara yako sasa hivi.
Maisha siku zote yanaongozwa na malengo na pasipo na malengo watu hupoteza mwelekeo, hatimaye kushindwa chanzo cha wako kufungwa magoli mengi sana. Mechi ya 2018 ni mechi rahisi sana kwako kuwahi kucheza, sasa kagunge magoli kwa uhakika kwa kuwela malengo.
2. ANZA NA MOJA
2018 ni mwaka Mpya kabisa. Kila kitu ni kipya na wewe unapaswa kuwa mpya. Anza na moja ndani ya 2018. Usikimbilie kufunga magoli mengi kwa wakati mmoja na ni jambo ambalo haliwezekani. Hata wachezaji maarufu akina Messi na Ronaldo hawajawahi kufunga magoli mawili kwa wakati mmoja. Ila huwa wanatafuta goli moja tu kwa wakati. Na wewe unaweza kuwa una shughuli nyingi sana, lakini ukaamua kujikita kufanya shughuli moja baada ya nyingine. Hii ndio kusema kwamba haugusi shughuli moja na nyingine bila kuikamilisha. Kama unataka kufunga magoli mengi sana ndani ya 2018 basi hakikisha kwamba unafanya shughuli moja kwa umakini na kufanya nyingine inayofuata kwa umakini pia.
3. KAMILISHA ULICHOANZA
Ndani ya dakika za mwanzo wa mchezo wachezaji huwa wana motiaha na nguvu kubwa sana. Hali kama hiyo haijawaacha  wajasiliamali na watu wengine wenye ndoto zao. Inapofika januari mosi wanakuwa kama msitu ambao umewashwa moto. Yaani hawashikiki. Lakini kadri siku zinavyoenda motisha yao huja kuzimwa ghafla. Yaani moto huzimwa na mvua za rasha rasha. Hahahah, sasa hakikiaha kwamba hauwi miongoni mwa watu ambao wanaacha kufanya biashara au wanaacha kutimiza malengo, kwa sababu ya kikwazo kidogo utakachokutana nacho ndani ya 2018. Kikwazo chochote utakachokutana nacho ndani ya 2018 ni mvua za rasha rasha. Wewe songa mbele na hakikisha unamaliza kufanya kile ulichoanzisha. Kiufupi ni kwamba, usiishie njiani 2018. Kamilisha kila unachoanzisha. Jiambie sasa kwamba Mimi……(jina) nitakamilisha kila kitu nitakachoanzisha ndani ya 2018.
4. NENDA HATUA YA ZIADA 2018.
Kama ni mchezo kila mchezaji anacheza. Kama chenga kila mchezaji anafanya hivyo, sasa wewe una nini cha kukutofautisha na wengine?? Kumbe hapo unapaswa kwenda hatua kadhaa zaidi ya wengine.
Siku hizi kama ni biashara wengi wamefungua. Sasa kwa nini mteja aje kwako na asije kwangu? Ndani ya mwaka 2018 hakikisha unajitofautisha kwa kutoa huduma bora zaidi kwenye biashara yako. Fanya kile ambacho wengine hawafanyi, yaani toa huduma ambayo wengine hawatoi ndani ya 2018. Je, wewe utatoa huduma gani? Utajitofautishaje na wengine? Utafanyaje kuhakikiaha Amina anakuja kununua kwako na si kwa jirani yako? Je, utafanyaje kuhakikisha Amina akija kununua mara ya kwanza anarudi tena?
5. FANYA KILA KITU KAMA VILE HUTAKUJA KUKIFANYA TENA
Kila kijacho mbele yako hakikisha unakifanya kwa ubora zaidi. Kifanye kama vile leo ni aiku yako ya kwanza na kama vile leo ndio siku ya mwisho. Kifanye kama vile hii ndko nafasi yako pekee ya wewe kukifanya.  Chukulia ungekuwa kazini leo hii. Na kama utakosea kufanya kazi ile basi kutumbuliwa kunakuhusu. Je, upo tayari kutumbuliwa?? Beba picha hiyo akilini mwako. Kama kutumbuliwa basi jitumbue mwenyewe kwa kufanya kwa ubora zaidi. Jitumbue kwa kuhakikisha kila kazi inayopita mikoni mwako imefanyika kwa ubora asilimia 100.
Kwa hakika kama utayazingatia haya ndani ya mwaka 2018 utang’aa sana. Utaufurahia sana mwaka na utakuwa ukifunga magoli wakati wengine wakitafuta nafasi hiyo wanaikosa. Na kamwe ndani y 2018 hautakuja kufunga goli la mkono!!
Ukikiwa nami,
Godius Rweyongeza
$ongambele
Mwandishi, kocha na mjasiliamali
0755848391
songambele.smb@gmail.com
www.songambeleblog.blogspot.com
✋🏿✋🏿✋🏿


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X