TATIZO SI RASILIMALIZ ZILIZOPOTEA-66 tatizo hujajua mahali ulipo


Sasa hivi tunapoelekea mwishoni mwa waka 2017 mchakato wa watu kuweka malengo umeanza. Bila shaka na wewe kwa sasa utakuwa unafikiri au upo katika mchakato wa kuweka malengo. Katika akili yako una mpango wa kwenda mbele sana. Lakini ebu tulia kidogo nikuulize swali moja ambalo ninaomba jibu lako sasa hivi. Uko wapi sasa hivi? Ndio hilo ndio swali langu kwa sasa. Watu wengi sana hawajui wako wapi, wala hwawajuI walipotoka. Jambo ambalo linayafanya maisha yawe magumu sana kwao kuweza kufika kule ambapo wao wanataka kufika kaitika maisha yao.
Kama katika akili yako mpaka sasa hivi unafikiri ni kwa jinsi gani utaweza kufanya mambo makubwa mwaka kesho ila hujui mwaka huu umefanya kiasi gani, basi jua kwamba unapaswa kukaa chini na kuhakikisha kwamba sasa unajipanga zaidi. Maana kama haujui ulipotoka, haujui mahali ulipo ni vigumu kwenda kule unapoenda. Ila suala sio kwammba uanze kurudi nyuma sasa na kuanza kufukua yale ya zamani. Jambo la msingi sana ni wewe hapo kuhakikisha kwamba unaipangilia baadae yako sasa hivi. Usiseme kwamba mwaka kesho nitafanyamauzo makubwa  zaidi ya ambavyo nimefanya mwaka huu. Ila hakikisha kwamba unaweka kiwango ambacho unapawa kukifikia. Ndio maana nikaanza kwa kusisitiza umuhimu wa kujua wapi ulipo sasa hivi.

Ukishajua wapi ulipo ssasa hivi, na ujakua wapi unataka kwenda. Basi hapo anza kwenda hatua moja kwa moja. Usilenge kumwangusha mtu aliye kileleni. Bali wewe hakikisha kwamba unalenga kumpita kwanza mtu aliye  mbele yako. Hii ndio kusema kwamba msururu wote ulio mbele yako haupaswi kukutisha katika safari yako. Bali wewe hapo unapaswa kuhakikisha kwamba unaundea kwa mpango maalum, mwisho wa siku utajikuta kwamba umeweza kuupita msururu wote.

,

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X