Habari ya siku hii ya leo rafiki yangu na ndugu msomaji wa blogu yako ya songa mbele. Imani yangu kwamba leo umekuwa na siku njema sana. Na hivyo unazidi kuweka juhudi kubwa sana kuhakikisha kwamba unaweza kufikia mafanikio makubwa sana ya kimaisha.
Bila shaka katika maisha yako umewahi kucheza mchezo wowote ule. Bila shaka katika maisha yako kuna mchezo mzuri sana ambao wewe binafsi unakufurahisha na unaupenda sana. Bila shaka kuna mchezo ambao unafurahi sana hasa pale unapowaona watu wakiucheza. Je, ni mchezo gani huo wa maisha ambao unafurahia kuucheza?
Unaweza ukawa mzuri sana katika mchezo wa ujasiliamali, mchezo wa kuimba, mchezo wa kuchora na mingine mingi sana. Binafsi naupenda sana mchezo wa kuandika. Mchezo huu ni sehemu ya maisha yangu. Naucheza mwenyewe lakini pia natazama wachezaji wengine wakiwa wanaucheza.
Hata hivyo katika makala haya ya siku hii ya leo tutaenda kuuzungumzia mchezo katika maana ambayo inafahamika kwa watu wengi sana. Maana watu wengi wanaposikia ukizungumzia juu ya mchezo moja kwa moja kile kinachokuja katika akili yao ni kwamba unazungumzia mchezo wa mpira wa miguu, mchezo wa kikapu, mpira wa wavu, masumbwi kutaja ila michache. Katika makala ya leo moja kwa moja tutajikita katika mchezo wa mpira wa miguu. Wengine wanauita kandanda, huku wengine wakiuita football kwa lugha ya wenzetu. Kila mchezaji ambaye amewahi kucheza mchezo huu au shabiki ambaye amewahi kushabikia mchezo huu atakubaliana na mimi kwamba kama wachezaji wakiingia uwanjani na kukuta kwamba hakuna magoli siku hiyo mechi haichezwi. Je, unajua kwa nini?
Kwa nini wachezaji wanapoingia uwanjani na kukuta kwamba magoli yameondolewa hawaendelei kucheza wakisema kwamba ni kawaida? Nani anaweza kunipa jibu la haraka?
Haya wakati wewe unazidi kutafuta jibu sasa naomba nikwambie kwamba kwa siku sasa umekuwa ukicheza mpira wa miguu bila ya kuwa na magoli uwanjani. Hii ndio kusema kwamba haukuwa na sehemu ya kulenga ili kufunga goli. Na umekuwa unafurahia hall hii kwa siku sasa. Mchezaji wa mpira anajua kwamba bila ya kuwa na magoli hatapata sehemu ya kulenga na kufunga. Kwa hiyo mwisho wa siku hatuwezi kusema kwamba timu yake imeshinda kwa sababu hayakuwepo magoli na hatuwezi kupima ufungaji kwa chenga tu alizopiga mchezaji.
Hii ndio kusema kwamba lazima magoli yawepo ili tujue nani kafunga na nani hjafunga.
Sasa mimi nachezaje mchezo wa maisha bila ya kuwa na magoli?
Bila shaka utakuwa unajiuliza swali hilil hapa
Wewe hapo unacheza mchezo wa maisha bila ya kuwa na MALENGO. Maisha bila ya kuwa na malengo ni sawa na kucheza mpira wa miguu bila ya kuwa na magoli. Malengo ndio yanatupa mwelekeo, malengo ndio yanatuambia wapi tulenge na wapi tusilenge, lakini pia melengo ndio yanatuambia kitu gani tunapawa kufanya na kitu gani hatupaswa kufanya. Hivyo kama hauna malengo maana yake utakuwa kama mtu amabye anacheza mpira wa miguu bila ya kuwa na mweleko. Yaani yeye kila sehemu inayokuja mbele yake yeye anapiga mpira wake.
Haya maisha sio maisha sio maisha ambayo unapaswa kuyaishi, haya sio maisha ambayo wewe umepangiwa kuishi. Wewe umepangiwa kusihi maisha bora zaidi ya haya ambayo unaishi sasa hivi. Wewe unastahili kuishi maisha mazuri zaidi ya hapo. Na maisha hayo utaweza kuyaishi kama utakuwa umejiwekea malengo ya kimaisha na kuhakikisha kwamba umeweza kuyafuata.
Hakikisha kwamba unajulikana wewe sehemu unapofunga goli lako. Kwa hiyo hakikisha kwamba unajiuliza swali hili mara kwa mara je, ninacheza mchezo gani sasa hivi? Je, ninapaswa kuwa nacheza mchezo huu? Je, kwenye mchezo huu nafunga wapi? magoli yako wapi? kama utakuwa huyaoni magoli, hakikisha unayatafuta magoli yalipo ili upate sehemu sahihi ya wewe kufunga.
Naomba nikutakie wakati mwema rafiki yangu.
Usikose kujipatia kitabu cha kutoka sifuri mpaka kileleni. Ambacho kitakufundisha zaidi juu umuhimu wa kucheza mpira huku kukiwa na magoli.
Tukutane kileleni.
Wewe Ni Zaidi ya ulivyo sasa.
Tukutane kwenye meza ya wanamafanikio.
Tukutane kwenye mzunguko wa wanamafanikio
Tukutane kwenye meza ya wanamafanikio.
Tukutane kwenye mzunguko wa wanamafanikio
Kujiunga na kundi la wasp la HAZINA YETU BONYEZA HAPA
Ndimi
Coach Godius Rweyongeza
godiusrweyongeza1@gmail.com
www.songambeleblog.blogspot.com
Ili kupata kitabu cha KUTOKA SIFURI MPAKA KILELENI BONYEZA HAPA
Bonyeza hapa ili uweze kupata makala maalumu kila wiki.
Bonyeza hapa ili uweze kupata makala maalumu kila wiki.