Watafute Watu


 Miongoni mwa vitu ambavyo unavihitaji sana maishani mwako ili kufanikiwa na kuhakikisha kwamba unapiga hatua kubwa sana  ni watu. Unahitaji watu ili uweze kufanya biashara zako. Unawahitaji watu ili uweze kuwa kiongozi. Maana kipimo bora cha kwamba wewe ni kiongozi bora kitaonesha majibu pale patakapokuwa na watu.
Unahitaji watu ili ukae darasani na kusoma. Hawa wanaweza kuwa ni walimu au wanafunzi wengine. Yaani hii ndio kusema wamba watu unawahitaji katika kile kona kila siku na kila wakati.
Kama wewe utakuwa mjasiliamali basi jua kwamba unahitaji watu katika biashara yako. Watu hao wanahitajika katika maeneo mbali mbali kama vile mahesabu, kutunza kumbukumbu , mauzo na mahusiano kutaja ila wachache. Hii ndio kusema kwamba hata siku moja usije ukasema kwamba mimi naweza kupiga safari kubwa sana ya kimafanikio bila ya kuwepo kwa watu na nikaweza kufikia hatua kubwa sana. Kumbuka kwamba hata pesa zako ambazo unazihitaji zipo mfukoni mwa watu. Hivyo mahusiano na watu ni muhimu sana na hakikisha kwamba muda wote unayatunza kama ambavyo unatunza mayai. Ukitunza vizuri uhusiano wako na watu wengine mwisho wa siku watu wenyewe watapenda kuutunza uhusiano huo ili wasije wakaupoteza, kwa hiyo utajikuta kwamba unaimarika zaidi.
Ni hayo tu kiwa siku hii ya leo rafiki yangu na ndugu msomaji wa blogu yako ya SONGA MBELE.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X