Hili Ni Jambo Linalonifanya Nimshukuru Mungu Kila Siku


Kushukuru ni kuomba tena. Walinena wazee wa zamani. Kila kunapokucha kuna kitu ambacho kinanifanya Mimi Godius Rweyongeza niendelee kumshukuru Mungu.
Yapo mengi sana ya kumshukuru Mungu na miongoni mwa hayo namshukuru Mungu kwa kutujalia watanzania waandish. Maandishi ni kumbukumbu zinazodumu kww muda mrefu sana. Hakika kumbukumbu hizi ni njema na zinatia moyo. Zinavutia na ni hazina kubwa sana kwa vizazi vijavyo.

Kuna watanzania wengi ambao wamejengewa hali ya kutokujikubali, na kutokuvikubali vitu vyetu. Ndio maana mashabiki wengi wa mpira hawaangalii mpira wa bongo.
Waangaliaji wa movie hawaangalii movie za kitanznia
Wafuatiliaji wa mziki unawakuta njiani wakiimba miziki ya Nchi za nje.
Lakini hali ni tofauti kwa upande wa vitabu.

Binafasi nawapenda sana waandishi wa kitanzania maana uandishi wa lugha ya kitanzania una raha kubwa sana, sana, sana.
Japokuwa ni ukweli kwamba mpaka sasa  nimesoma vitabu vingi vya watu wa nje ya nchi kuliko vitabu vya watu wa ndani ya nchi. Ila huwa nafurahi sana nikisoma Kitabu cha ndani ambacho kimeandikwa na mtanzania. Hali hii imenifanya nijenge utaratibu wa kusoma walau Kitabu kimoja kila mwezi cha mtanzania.
Kwa mwaka 2017 nilipata kusoma vitabu vifuatavyo vya watanzania.

1. Matatizo si Tatizo, matatizo ni daraja padre Dk. Fautsine kamugisha

2. Barabara ya Mafanikio cha Edius Katamugora

3. Maji Yakimwagika Yanazoleka, umevaa miwani gani? Cha padre Daktari Faustine Kamugisha

4. Fursa 3000 Zinazokuzunguka Afrika Masahariki na Mtaji wa Kuanzia cha David RG Nashon

5. Mbinu za mjasiliamali cha Gwakisa T. Balele

6. Ijue Biashara Ya Mtandao cha Makirita Amani

7. Mafanikio ni Haki Yako  cha albert Nyaluke Sanga

8. Kiota cha Mafanikio cha Albert Nyaluke Sanga

9. Hisa, Uwekezaji na Akiba Cha Emiliani Busara na Mrembo Grace

10. Nidhamu Kwenye Masuala Ya Fedha cha BG.Malisa

11. Kitabu cha Mithali Katika Biblia

12. Mafanikio Yako mikononi mwako cha  Joseph D Nyakoma

Hivi vitabu ni vizuri sana, na vina maudhui mazuri sana ndani yake.
Siwezi kukwambia soma hiki na acha kile. Badala yake nakushauri uvitafute vyote na uvisome. Vitabu hivi vimenifanya nizidi kukua kila siku.

Hata hivyo Mimi mwenyewe ndani ya mwaka mpya 2017 nimeandika vitabu vitatu.
1. KUTOKA SIFURI MPAKA KILELENI

2. TATIZO SI RASILIMALI ZILIZOPOTEA volume-1

3. MAMBO 45 YA KUZINGATIA KABLA YA KUANZIASHA BIASHARA

Vipate pia na hivi uviongeze kwenye orodha yako.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X