Hizi Ni Aina Tano Za Maamuzi Unazoweza Kufanya Mwaka Huu


Habari ya siku ya leo Rafiki yangu na ndugu msomaji wa makala haya kutoka SONGA MBELE BLOG. Imani yangu leo ni siku jema sana ambapo uaenda kufanya kazi kwa juhudi nguvu na bidii kubwa sana. Hongera sana kwa siku hii ya leo.

Kwa kawaida kila siku huwa ni mpya. Huwa ni siku njema zaidi ya jana na siku bora kabisa. Ndani ya siku husika huwa tuna maamuzi ya aina mbili. Kuitumia vizuri siku husika au kutoitumia kabisa. Hivyo amua kuitumia leo hii.

Mbali na ukweli kwamba kila siku huwa unafanya maamuzi. Leo hii ningependa kukushirikisha maamuzi makuu ambayo utapaswa kufanya ndani ya mwaka 2018. Kama utayatekeleza vizuri sana maamuzi haya, basi jua kwamba mwaka huu utaweza kuwa mwaka mzuri sana kwako.

1. ISHI WITO WAKO
Mara nyingi sana huwa unakuta kwamba mzazi anapokuwa na watoto watano basi anaanza kufikiri, sasa hawa watoto nitawatengeneza kama ifuatavyo;
Yohana nitamjengea mazingira ya kuwa daktari maana mshahara ni mkubwa na ataweza kuishi vizuri.
Musa atakuwa dereva kwa sababu babu yake alikuwa dereva.
Petro awe mwanasheria kwa sababu Mimi baba yake ni mwanasheria
Deus atakuwa mwanajeshi wa jeshi la wananchi maana wanalipwa vizuri na atastaafu mapema….

Baada ya hapo anaanza kuzunguka mjini kuangalia ni wapi anaweza kuona kazi atakayoifanya Paulo. Baada ya kuzunguka kwa muda sasa hatimaye anafika Benki na kumwona mhasibu. Basi anarudi nyumbanj kwa furaha na kumwambia Paulo, Paulo wewe utakuwa mhasibu. Kwa hiyo unakuta watoto wamesoma wanafanya kazi ambazo hata haukuwa wito wao. Anafanya kwa sababu tu, baba alimwambia.

Kama wewe ni mmoja wapo hakikisha kwamba mwaka huu sasa unachange. Huu ndio mwaka wa mabadiliko.
anza kubadilika maana zama zenyewe zimebadilika.
Kama unataka kufanya vizuri sana maishani wako basi hauhitaji kukumbatia kitu ambacho wewe hujaumbwa kufanya. Kama umeumbwa kuchora na kuipendezesha dunia kwa michoro, basi anza kufanya hivyo. cha kufanya, anza sasa kuangalia ni wapi umeitiwa na uanze kutimiza hilo kududi lako.

2. MARAFIKI
Mwaka 2018 sio tena mwaka ambao unapaswa kutembea kwa namna ya kawaida sana. Sio tena mwaka ambao unapaswa kuishi kwa namna ile ile.  Ebu jiambie sasa kwamba huu ndio mwaka mwaka wangu. Sema kwamba huu mwaka huu lazima nifike kileleni. Na ili uweze kufika huko basi huna budi kubadilisha marafiki. Marafiki uliotembea nao mwaka jana na wakakufikisha hapo ulipo sio walewale watakaokufikisha unapotaka kwenda. Kumbe kuna haja ya kubadili marafiki maana huwezi kupiga hatua kwa kufanya mambo kwa namna ile ile uliyoitumia siku za nyuma. Ngoja nikwambie kitu. Mwaka huu kuna marafiki ambao utapaswa kuachana nao. Kuna marafiki wachache sana utapaswa kuambatana nao. Kuna marafiki utapaswa kuwaingiza kwenye mzunguko wako. Hakikisha kwenye mzunguko wako kuna watu ambao wanafikra za kujenga. Sio wale wanaobomoa. Siku zote marafiki wako ndio wanaotuambia aina ya tabia uliyonayo. Sasa Fanya uamuzi kuntu wa kutembea na marafiki wenye maono 2018.

Soma zaidi; Mfahamu Vicenti Thomas Lombardi

3. KUWEKEZA
Je, umekuwa unawekeza wapi miaka iliyopita?
Mwaka 2018 ni mwaka ambao unahutaji kufanya uamuzi wa kuwekeza haswa kwenye maeneo makuu mawili.
Elimu
na
Uchumi

Hakikisha unawekeza katika kusoma vitabu mwaka 2018. Soma vitabu vingi, vingi sana kadri ya uwezo wako. Soma vitabu asubuhi, mchana na jioni. Hakikisha kila unapoenda unatembea na kitabu kwa ajili ya kuongeza maarifa.

Wekeza pia katika masula ya kiuchumi. Wekeza katika vitu ambavyo vitakuja kuongezeka thamani siku zijazo. Wekeza wekeza wekeza!

4. BIASHARA
Ndani 2018 hakikisha unaanzisha mfereji mpya wa kipato. Kama mwaka jana ulikuwa na mfereji mmoja wa kipato (ajira). Hakikisha mwaka huku unaongeza mifereji mingine ila anza na mmoja sasa. Na hapa unaweza kuangalia huduma  ambayo unaweza kuitoa kwa kutatua matatizo yanayowakabili watu. Mwaka 2018 anzisha biashara.

5. ENEO
Je, likitajwa jina lako watu wanajua uko wapi? Wanajua kitu gani kinaongelewa? Mfano tukitaja VODACOM kila mtu anajua ni nini? Anajua wako wapi hapa mjini na wanajushughulisha na nini? Tukiitaja NMB basi kila mtu anajua ni nini? Inahusika na nini? Na iko wapi? Wewe uko wapi? Unashughulika na nini?
Mwaka huu ni wako. Tukujue wewe kama wewe kwamba uko wapi? Unafanya nini?

Hakikisha unaanza sasa kujitambulisha uko wapi? Hapa simaanisshi uende kwa watu uanze kuwaambia kwamba Mimi nipo Dar, nipo Morogoro! Hasha! Matendo yanaongea zaidi ya maneno. Wewe toa huduma tutakujua tu!!

Tukutane siku nyingine hapa hapa safuni!

Ulikuwa nami

Godius Rweyongeza

Jipatie  sasa nakala ya vitabu vyangu, TATIZO SI RASILIMALI ZILIZOPOTEA na KUTOKA SIFURI MPAKA KILELENI kwa pamoja kwa bei ya sh. 14,000tu badala ya sh. 20,000.

Tuma pesa kwenda nambari 0755848391 jina GODIUS RWEYONGEZA
baada ya hapo nitumie ujumbe wa njia ambayo ungependa nikutumie vitabu hivi, inaweza kuwa wasap, telegram au email.

Karibu sana.

Bei ya kitabu kimoja kimoja

1. TATIZO SI RASILIMALI ZILIZOPOTEA (6,000)

2. KUTOKA SIFURI MPAKA KILELENI (8,000).

bei hizi ni kwa siku chache tu baada ya hapo kila kitabu kitakuwa kinapatikana kwa sh. 10,000


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X