Mwishoni mwa mwaka 2018 Rafiki zangu wengi sana walikuwa wakinitumia jumbe mbali mbali za kuuaga mwaka, na kuukaribisha mwaka. Wengine walinitumia jumbe za shukrani, wengine jumbe za kuukaribisha mwaka, wengine jumbe za kuuaga mwaka kutaja ila machache.
Jumbe zote hizi kwangu zilikuwa zina maana kubwa sana. Moja kati ya ujumbe ambao ulinifanya nione kwamba maisha ni rahisi sana ni ujumbe wa rafiki yangu mmoja uliosomeka hivi “2018 NI UKURASA MPYA WA KITABU AMBAO HAUJAANDIKWA HATA TONE, JE, WEWE UTAANDIKA NINI”?
Basi hapo ndipo niliposema kama kila siku ni ukurasa basi mwaka huu naweza kuandika Kitabu kikubwa sana. Ukubwa wa Kitabu hiki ni Kurasa 365. Kama 2018 kuna karatasi ambazo hazijatumika basi na wewe zitumie. Zitumie kuandika kitabu hiki. Kichwa cha Kitabu hiki, utaamua wewe mwenyewe kiitweje. Lakini mimi cha kwangu kitwaitwa GODIUS RWEYONGEZA. Nitaandika ukurasa mmoja mmoja kila siku. Mpaka mwishoni mwaka 2018.
Leo ni siku ya kuandika ukurasa wa pili, kama jana hukuadika ukurasa wa kwanza basi anza leo kuandika na mwishoni mwaka mwaka utakuwa umeandika Kurasa 364.
Nakutakia siku njema sana.