Mfahamu Vicenti Thomas Lombardi


Vicenti Thomas Lombardi alizaliwa novemba 11 mwaka 1913 katika nchi ya marekani. Alikuwa mchezaji wa mpira wa miguu na lakini pia alikuwa kocha wa timu za mpira Wa miguu ikiwemo timu ya mpira wa miguu ya GREEN BAY PACKERS. Kiukweli aliiongoza timu hii kupata vikombe kadha wa kadha katika nchi yake.

Kuna vitu vingi sana aliweza kufanya wakati wa uhai wake kabla ya kifo chake mwaka 1973 juni 3. Leo hii ningependa tujufunze tabia moja tu.

VICENT THOMAS LOMBARDI alikuwa mtu wa kuwahi na alikuwa mtu  anayefuata muda kwa hali ya juu sana. Moja ya tabia yake kubwa sana kuhusu muda aliyokuwa akisisitiza wachezaji wake ilikuwa kuwahi sehemu fulani dakika 15 kabla ya muda wa tukio.

Soma zaidi; Mambo Matano Ya Kuzingatia Kabla Ya Kuanza Jambo Lolote

Kwa mfano kama wachezaji wake walipaswa kusafiri kutoka mji mmoja kwenda mwingine kwa ajili ya mechi walipaswa kuwahi na kufika pale dakika 15 kabla. Hii ndio kusema kwamba kama safari inaanza saa 10 za jioni basi kila mchezaji alipaswa kuwa eneo la tukio saa Tisa dakika 45 (ambazo ni dakika 15 kabla). Kama mchezaji angechelewa hata kama angefika eneo la tukio dakika 10 kabla, basi huyo alikuwa anaachwa maana hakufuata muda. Hahahah! Umeona eeh! Inachekesha lakini kuna kitu kikubwa sana cha kujifunza. Je, ungependa kupiga hatua kubwa sana? Je, ungependa kwenda hatua ya ziada? Anza kujali muda. Kama unapenda ufahamike kama mtu anayefuata muda anza sasa. Fika eneo unalopaswa kuwa kwa wakati. Fika dakika 15 na tano kabla.

Kiukweli hii ni tabia njema sana ya kujifunza. Na ni tabia njema sana ambayo ukiijenga mwisho wa siku itakujenga.

Ndimi,
Godius Rweyongeza
0755848391


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X