Sheria Tano (05) Za Mchezo Wa Mwaka Huu




Katika mchezo wa mpira wa miguu wachezaji wanajua kwamba kipenga kikipulizwa basi huwa hakuna kitu kingine bali kucheza mpira. Kipenga huwa sio ishara ya kujiandaa bali huwa ni ishara ya ANZA. Kwa hiyo hakuna mchezaji ambaye huwa anaanza kujiandaa pale kipenga kinapopiulizwa. Bali kipenga huwa kinawakuta wachezaji uwanjani moja kwamoja. Jambo kama hili hapa limejitokeza mwaka huu 2018. Mwanzoni mwa mwaka huu kipenga kimepulizwa jambo ambalo limemlazimisha kila mtu kuingia uwanjani na kucheza mpira. Tofauti na mechi za kawaida ambapo mtu huwa anakuwa na dakika 90 tu. Katika mechi hii hapa ya mwaka 2018 kila mtu anazo siku 365. Na kila siku ina saa 24. Na kila saa lina dakika 60. Hii ndio kusema kwamba mwaka huu tu unazo dakika 525,600. Hahah! Dakika nyingi sana, si unaona eeh! Zinaweza kuonekana ni nyingi sana au kidogo kulingana na mtazamo wa mtu. Katika Makala ya leo hatutaziita dakika 525.600 bali, tutaziita dakika 90.   Kwahiyo, hapa kuna vitu vitano ambavyo unapaswa kuvifanya ndani ya dakika 90 za mwaka huu. Ambavyo naviita sharia za mwaka 2018!

1. unapaswa kuwa na malengo. Huu ni mwaka wa kazi. ndani ya mwaka unaweza kuamua kufanya kazi au kutokufanya kabisa. Huu sio mwaka wa kusema kwamba nitajaribu kufanya kitu Fulani. Wala huu sio mwaka wa kusema kwamba unajaribu. Badala yake hakikisha kwamba unafanya haswaaa! Hakikisha kwamba unakuwa na malengo yako ambayo yanakuongoza ndani ya mwaka huu li uweze kuyatimiza. Usikae tu na kutulia ukitegemea vitu vizuri kuja vyenyewe. Unapaswa kuhakikisha kwamba unavitengeneza ndani ya mwaka huu wa 2018. Maisha yanaongozwa na malengo. 
2. mahusiano. Mwaka huu ni mwaka ambao unapaswa kuhakikisha kwamba umekuza mahusiano yako na watu wengine ambao wamekuznguka. Si hilo tu mwaka huu unapasawa kuhakikisha kwamba umeenda hatua ya ziada na kukutana na watu ambao hujawahi kukutana nao maishani mwako. Nenda hatua ya ziada, kwa kuongea na watu ambao hujawahii kuongea nao maishani mwako. Huu mwaka ni wa kwako. Ongeza mzungukao wa watu wanaokufamu mwaka huu. Huuu mwaka ni  wa kwako. Hakikisha kwamba haukui tu kwa umri bali pia unakua kwa idadi ya watu ambao wanakufahamu.
3.  kuwekeza. Je, una mpango wa kuwekeza kwa mwaka hu 2018. Je utawekeza wapi ndani ya mwaka huu? Kama bado ulikuwa bado hujaweka malengo ya kuwekeza basi muda wako ndio huu hapa ambapo unapaswa kuhakikisha kwamba unaenda kuweka malengo ya kuwekeza. Mwaka huu kama ambavyo nimetangulia kusema hapo awali ni mwaka wako. Hivyo unapaswa kuhakikisaha  kwamba unawekeza katika maeneno mbali mbali. Na leo ninazungumzia eneo moja muhimu sana ambalo unapaswa kuhakikisha wamba unawekeza ndani ya mwaka huu wa 2018. Na eneo hili si jingine bali kuwekeza katika miradi ambayo inakuingizia pesa. Pesa ni jambo la muhimu sana hapa duniani. Likiwa ni jambo la pili kwa umuhimu baada ya hewa yaoksijeni. Hivyo itakuwa si vyema hata kidogo wewe hapo kupuuza na kuacha kabisa eneo hili la pesa. Na ngopja nikwambie kitu cha muhimu sana ambacho unapaswa kuhakikisha kwamba unakizingatia mwaka huu. Uwekezaji wako mwaka huu unapaswa kuwa wa aina mbili. Uwekezaji wa muda mrefu au uwekezaji wa muda mfupi.  Uwekezaji wa muda mrefu uwe ni uwekezaji ambao utakuigizia pesa baada ya miaka kadhaa kipato cha kutosha.  Lakini pia uwekezaji wa muda mrerfu unapaswa kuwa wa chanzo Fulani ambacho kitaingiza kipato leo, kesho na kesho kutwa. Yaani uwekezaji ambao hata hauchachi. Hivi vyote unaweza kuvitengeneza wewe hapo. Uwekezaji wa muda mfupi kwa mwaka huu uwe ule wa kuhakikisha kwamba unaendelea kukupa wewe hapo mahitaji ya muhimu sana, yaani kwamba utaendelea kupata chakula, na matumizi mengine ya muhimu. Isije ikafikia hatua kwamba sasa unakosa hata hela ya kula kwa sababu umefanya uwekezaji wa muida mrefu.
4. tabia. Ndani ya mwaka huu kuna tabia ambazo hupaswi kamwe kuambatana nazo. Ni tabia ambazo unapswa kuhakikisha kwamba unaziacha na kuwaachia watu wengine. Unaziacha kwa sababu hazikuongozi kwenda kwenye malengo yako. Unaziacha kwa sababu tu si sehemu ya wewe kuelekea kule ambapo unataka. Hivyo, hakikisha kwamba ndani ya mwaka huu unaanzisha tabia mpya ambazo zitakupeleka kwenye mafanikio.
5. anza.
Mwaka huu unaswa kuhakikisha jkwamba unaanza. Usiogope kuanza ndani ya 2018. Huu ni mwaka wako. Kubali kuanguka ndani ya 2018. Kubali kuanguka mara nyingi sana lakini kila unapoanguka hakikisha unasimama na unaanza tena. Huwa napenda sana nikisoma maneno kutoka vitabu vitakatifu. Maneno haya huwa yanamzungumzia rafiki wangu YESU MNAZARETI. Yaani yanasema alipokuwa anapigwa mijeredi na kuanguka alikuwa anasimama tena nakuendelea na safari yake. Na wewe ukipigwa mijeledi ukaanguka chini simama tena na songa mbele. Kubali kuanguka, lakini usianguke mweleka wa mende. Anguka mweleka wa kishujaa. Yaani unaanguka na kusimama hapo hapo hata hakuna mtu yeyote ambaye anagundua kwamba ulianguka. Hata kama bado watu watagundua kwamba umeanguka, jua kwamba bado unapaswa kwamba unazidi kusonga mbele.
Huu mwaka huu lazima kieleweke!!!


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X