Ukitaka kujua umuhimu wa dakika moja, muulize mwanajeshi katika medani ya vita. Kila dakika ambayo inakuja mbele yako kila wakati ni dakika ya muhimu sana wala si ya kupoteza. Kila dakika hakikisha kwamba unaitumia kufanya mambo makubwa sana. usiipoteze hata dakika moja katika kazi zako. Ipangilie vizuri kila dakika ambayo inakuja mbele yako ili uweze kujifunza mambo makubwa sana ambayo yapo katika dunia hii. Dunia hii imejaa vitu vingi sana ambavyo unaweza kufanya. Siku pia ina masaa mengi ambayo uunaweza kuyatumia kufanya kitu. Lakini masaa yote yanatengenezwa na dakika moja tu. Ujue umuhimu wa dakika moja katika maisha yako na hakikisha kwamba unatumia vizuri muda wako kusonga mbele.
GODIUS RWEYONGEZA
0755848391
#tatizo si rasilimali zilizopotea
TOKA 0 SASA ANZA KUELEKEA KILELENI