Vitu Vitano Viinavyokuunganisha Wewe Hapo Na Watu Waliofanikiwa


Ulipozaliwa ulilia wakati wengine walicheka, unapaswa kuishi maisha kiasi kwamba ukifa watu wengine walie wakati wewe hapo  ukichekelea. aliandika Robin Sharma. 
Katika hali ya kawaida huwa sio rahisi kujua ni lini wewe hapo utakufa na kuondoka hapa duniani. Ila kuna kitu kikubwa sana ambacho huwa kinanipa nguvu kwamba mimi pia naweza kuwa mtu mkubwa sana hapa duniani maana kuna watu ambao waliweza kupiga hatua kubwa hapa duniani. Katika dunia hii ambayo mimi niniaishi kuna watu wameweza kujenga majina yao  japo waliweza kuishi miaka kadhaa iliyopita,  ukifuatilia watu hawa hawakuwa  na kuwa kitu kikubwa sana ambacho walianza nacho. Kikubwa sana ambacho walikuwa nacho wote ni vitu hapa vitano, hivi ni vitu ambavyo watu wote walioweza kuishi duniani wamekuwa navyo sawa, hakuna mtu ambaye amewahi kumyanga mtu mwignine. Labda tu unaweza kuwazawadia watu vitu hivi lakini hakuna mtu wa kukunyanganya. Vitu hivi ni kama ifuatavyo
SOMA ZAIDI; Hili ni Kosa Ambalo Watumiaji Wengi Wa Mtandao Hufanya


1.     Oksijeni ni moja
Oksijeni kila mtu anayo bure kabisa. Labda tukiondoa nyakati fulani fulani ambapo mtu akiumwa atahitaji kununua hewa hii katika mahospialini. Mtafute aliyefanikiwa kupiga hatua katika jambo lolote na umuulizea kama yeye anahewa yake anayovuta tofauti na oksijeni. Nenda mashariki, toka uende mpaka  magharibi baada ya hapo nenda kusini na kasikazini. Utagundua kwamba watu wote wanavuta  hewa ile ile. Hakuna mwenye zaidi wala mwenye kidogo sana. sasa kwama waliofanikiwa wamvuta hewa hii hii ambayo na wewe unavuta kwa nini wewe usiweze kufikia hatua kubwa sana?


2.     Gravity ni ile ile
Kila mtu hapa duniani anavutwa katikati ya dunia na nguvu il ile ya uvutano iitwayo gravitational force. Hakuna mwenye nguvu hii zaidiya mwenzake. Wala hakuna ambaye anaweza kubadili vitu kwa namna moja au nyingine ili yeye aweze kuvutwa zaidi ya wengine. Hakuna. Kama waliofanikiwa wanavutwa kwa na nguvu hiyo hiyo inayokuvuta na wamefanikiwa kwa nini wewe usiweze?


3.     Masaa 24 ni yale yale
Ukiamka asubuhi kila siku unakuwa na zawadi ya masaa 24. Huwezi kuwa na zaidi au kidogo ya hapo. Na mwenzako pia anayo masaa hayo hayo. Je, wewe ya kwako unayatumia kufanya nini?

SOMA ZAIDI; Sheria Tano (05) Za Mchezo Wa Mwaka Huu


4.     Uhuru wa kuchagua
Kila mtu anaweza na anao uhuru wa kumtosha kuchagua kile ambacho anakitaka maishani mwake. Kila mtu yu huru na uhuru u sawa. Unaweza kuukuza na kuongeza uhuru wako au aunaweza kuupunguza uhuru wako na kuurushisha chini kabisa. Sasa amua kuutumia uhuru wako huu katika kuhakiisha kwamba unafanya maamuzi sahihi na unaachagua vitu vizuri vinavyokufaa.


5.     Vitabu ni vile vile
Hahaha! Usishangae, moja kati ya vitu ambavyo nimegundua, watu wanavyo kwa usawa ni vitabu. Unapazaliwa vitabu vyote vinakuwepo kwa ajili yako. unakuwa hauna vitabu vingi sana zaidi ya mwenzako wala unakuna hauna vitabu vichache sana zaidi ya mwenzako. Ila unakuwa na uhuru wa kuchagua vitabu gani usome na vitabu gani usisome. Kwa hiyo unaweza kuchagua vitabu vya kimafanikio kama ambavyo watu wengine wanafanya na hatimaye kuweza kuanikiwa. Au unaweza kuamua kutosoma kabisa.  Ndani ya vitabu kuna maarifa. Ndio maana vitabu nimevirodhodhesha kwenye orodha ya vitu ambavyo unavyo kwa usawa na watu wengine. Ni kwa sababu watu walioweza kuandika majina yao vizuri ni watu ambao wanasoma vitabu na kusoma vitabu. Na kwa kuwa zawadi hii ipo, basi ichangamkie au acha kabisa.


One response to “Vitu Vitano Viinavyokuunganisha Wewe Hapo Na Watu Waliofanikiwa”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X