Kila unapoamka kila siku asubuhi, siku yako unakuwa nayo masaa mengi sana yaani masaa 24, lakini hata siku moja, muda siku zote huwa unaonekana kama hautoshi hii ni kutokana na ukweli kwamba kazi zinakuwa zinaonekana ziko ningi sana. tena ukifanya kazi zako kufikia jiooni unajikuta kwamba umechoka sana lakini ukiingalia siku yako umefanya nini unaonekana kama vile siku hii ye leo haujafanya kitu.
Hili tatizo sio kwamba linakukumba wewe hapo peke yako, bali kuna kundi kubwa sana la watu ambao wanakubwa na hili tatizo. Je, hali kama hii tuiache iendelee kuwepo tu kila siku? Bila shaka hapana? Je, kuna watu wameweza kufanya kazi zao kwa usahihi na kwa umakini wa hali ya juu na kwa mpangilio mzuri sana? hapa jubu lake ni ndio! Sasa haawa watu wana nini? Ukweli ni kwamba ni asilimia chache sana, ya watu ambao huwa wanaamka kila siku asubuhi na kwenda kufanya kazi na kufikia jioni wanakuwa wamefanya kazi kwa ubora wa hali ya juu sana, wengine wanajjikuta kwamba walikuwa na kazi nyingi sana ila wakiangalia kitu kimoja muhimu sana ambacho wameweza kukifanya ndani ya siku yao hata hakionekani. Tatizo ni nini? Jibu ni rahisi sana, ni malengo! Ni asilimia tatu ya watu ambao wana malengo wameyaanfdika na kuyaweka sawa sawia! Asilimia 97 ya watu haawana malengo. Ingawa kila siku wanaonekana kwamba wapo bize wanafanya kazi hapa na pal ila ukweli ni kwamba watu walio wengi kabisa hawajui wanachokifanya. Yaani mtu anaenda kazini kwa sababu tu alikuwa kazini jana na anarudi nyumbani kwa sababu tu ametoka nyumbani asubuhi. Ukiwaita watu na kuwauliza, je, ni kitu gani kimoja ambacho kama hata kama utakosa kufanya vitu vingine siku hii ya leo basi utapaswa kukifanya kitu hicho? Basi, utashangaa, watu hawajui. Yaani wanataka kile kitu wafanye. Tamthilita waangalie, mpira nao waufuatilie, kuchati wachati mpaka watakakpochoka, facebooka washnde asubuhi mpaka jioni wakifurahia kila kila kura ambayo inapigwa kwenye picha zao. Yaaniw wanapoteza muda na kupoteza muda kila siku kilwa wakatiki na kila saa.
Hawajui umhimu wa muda. Moja kati ya vitu muhimu sana ambavyo unavihitaji ili kuweza kupiga hatua kubwa sana kwenda unapotaka kwenda hatua kubwa sana ni kuwa na melgno. Katika sura hii tutajadili kwa kina jinsi ya kuweka malengo yako ambayo yatatimia.
1. Hatua ya kwanza katika kuweka malengo ni KUAMUA KABISA JUU YA KILE AMBACHO UNAKIHITAJI
Je, unataka kwenda wapi? Unahitaji kujua kitu ambacho unakihitaji katika maisha yako. kiweke katika akili yako na kione kabisa kitu hicho. Kaa chini kabisa na uhakikishe kwamba unafikiria kwa umakini ambacho unapaswa kuwa nacho maishani mwako.
2. KIANDIKE CHINI
Lengo zuri ni lile ambalo limeandikwa kabisa chini kwenye daftari yako. kwa hiyo hakikisha kwamba lengo lako limeandikwa kabisa chini. Lengo zuri ni lile linaloandikwa kwenye wakati ulipita kidogo na wakati uliopo. Au lile ambalo linaonesha kwamba kitu ambacho unakifanya sasa tayari kimekamilika. Mfano wa uandishi wa malengo ni pale unapoaandika kwamba nimenunua shamba, ninamiliki nyumba, ninamiliki gari aina ya ….yenye rangi ya ….
Hii itakusaidia sasa kuanza kupanda ngazi sahihi. Moja kati ya vitu ambavyo vinaangusha watu wengi kwenye maisha ni pale watu wanapokuwa wanapanda ngazi ambayo haijakaa kwenye jengo sahihi.
3. Weka ukomo kwa malengo yako
Malengo ambayo yameandikwa bila ya kuwekewa ukomo ni hatari sana, maana huwezi kujua ni wapi unatokea na ni wapi unakwenda. Yaani wewe unachokifanya ni kuhakikisha kwamba unatembea tu kila wakati kukitokea huku na kwenda sehemu nyingine. Lakini kiukweli hutakuja kujua ni lini lengo lako limekamilika. Ubora wa lengo ni kwamba uliwekee kikomo katika ukamilikaji wake. Lengo lenye ukomo litakufanya wewe uweze kuongeza kuhudi katika utendaji wake wa kila siku haswa pale unapokuwa unajua kwamba lengo kwa sasa linakaribia mwishoni. Hivyo hakikisha kwamba unawekea lengo lako ukomo wa muda. Andika hivi kufikia tarehe….mimi….ninamiliki….
4. Andika orodha ya kila kitu ambacho utakihitaji katika kuhakikisha kwamba unafikia lengo lako. Je, kuna vitu gani karibu ambavyo vitakusaidia wewe kuweza kufikia ndoto lengo. Mfano kama umeweka lengo la kulima hekari moja ya mahindi mwaka hub huu ndio muda wa kuanza kuagalia ni rasilimali gani ambazo zipo karibu yako ambazo unazihitaji kwa ajili ya wewe kuweza kufikia malengo yako. inaweza ikawa ni ardhi ipo tu na haina mtu ambaye anaitumia, linaweza likawa ni jembe ambalo unapaswa kulinunua
5. Angalia ni watu gani utawahitajni katika kutimiza malegno yako. je, utatimiza lengo lakko ukiwa peke yako? je, unahitaji watu. Je, ni watu gani unawahitaji katika kutimiza lengo lako? Waorodheshe pia watu hawa ambao unajua wazi kwamba ili wewe uweze kutimiza ndoto yako basi watu hao unawahitaji. Wanaweza kuwa ni watu wako wa karibu sana au hata wale wa mbali. ila hakikisha pia nao unawaandika
6. Sasa ipangilie orodha yako. kama umeweka malengo mengi sana sasa ni muda wako kuhakikisha kwamba unapangilia kazi zako kwa umakini wa hali ya juu sana. swali moja na la muhimu ambalo unapswa kujiuliza ni je, ni ktu gani kimoja ambacho kama nitakifanya na kukikamilisha basi nitakuwa nimefanya kazi kubwa sana. basi kitafute kitu hicho na hakikisha kwamba unakifanyia kazi kitu hicho. Je, kipo? Yape malengo yako namba kuanzia lengo la kwanza mpaka la mwisho.
7. Anza kulifanyia kazi lengo lako mara moja. Hakikisha haipiti ile iitwayo leo bila ya wewe kuhakikisha kwamba umelifanyia kazi lengo lako. Lengo huwa halifanyiki na kukamilika ndani ya siku moja. Utimilifu wa lengo ni mkusanyiko wa malen go mengi madogo madogo ya kila siku. Kwa hiyo ukichukua hao yote ukayaangunisha unakuna kupata kitu kimoja ambacho ni kamili.
2 responses to “Hatua Muhimu Katika Kuweka Malengo”
[…] SOMA ZAIDI HAPA:Hatua Muhimu Katika Kuweka Malengo […]
[…] Hatua Muhimu Katika Kuweka Malengo […]