Hii Ni Hazina Kubwa Kuwahi Kutokea Katika Dunia Hii


            HII NDIO HAZINA KUBWA SANA KUWAHI KUTOKA KATIKA DUNIA HII
Habari ya siku hii ya leo rafiki na ndugu msomaji wa makala haya murua kabisa kutoka katika blogu yako ya SONGA MBELE. Imani yangu kwamba leo umekuwa na siku njema sana na unaenda kufanya makubwa sana siku hii ya leo. Ni jambo jema sana na la kumsuhukuru mungu maana siku hii ni ya kipekee sana na haijawahi kutokea katika dunia hii. Siku hii ya leo tunaenda kuzungumza juu ya hazina kubwa ambayo tunayo hapa duniani. Hii ni hazina ambayo kila mtu mweye akili timamu na kila mtu ambaye anaishi katika dunia hii anapaswa kuhakikisha kwamba anaitumia kila siku bila kuchoka. Ubora wa hazina hii kadri inavyokuwa unaitumia ndivyo hazina hii inavyokuwa inazidi kukua zaidi na zaidi. Kiufupi ni kwamba hazina hii huwa haishiwi. Yaani kila siku hazina hii inatoa zaidi na zaidi na zaidi. Kikubwa ni kwamba wewe hapo unapswa kuwa tayri kuitumia hazina hii ili uweze kufaidika nayo. Kuwepo kwa hazina hii hakutoshi, ila kuzitumia hazina hii ndio kitu cha maana kubwa. Hazina hii ipo, isipotumiwa yenyewe inakuwa haina shida yoyote ila kama itatumiwa itakufaidisha wewe kwa manufaa ya sasa hivi na siku zijazo. Hazina hii ni VITABU. Kiukweli dunia hii ina vitabu vingi sana juu  ya kitu ambacho wewe kama wewe ungependa kufuatilia. Hazina hii imejaa kila aina ya maarifa ambayo unayahitaji. Kikubwa ni kwamba wewe unapaswa kuwa tayari kuyatumia maarifa haya na kuyaweka katika matendo ya kila siku. Vitabu hivi vipo katika mifumo mingi sana ila kama hutachukua hatua kuhakikisha kwamba unavitafuta vitabu hivi unaweza kuishi maisha yako hujawahi kusoma na kujua mang’amuzi yaliyo kwenye vitabu hivi hapa. Vitabu vipo kwa ajili yako na kwa ajili ya manufaa yako. hivyo ni vyema sana na wewe ukahakiisha kwamba unavisoma vitabu hihi ili uweze kunufaika na maarifa haya yaliyo kwenye vitabu. Vitabu ni vya kwako kwa ajili yako ili na wewe uweze kuendelea mbele na kusonga mbele. Hakikisha siku hii ya leo unatafuta kitabu kimoja na kukisoma, kama hujui kni kitabu gani unaweza kukisoma basi ngoja nikwambie vitabu vitatu ambavyo ukivisoma utaelimika na vitabu hivi sio vingine bali ni
#1, KUTOKA SIFURI MPAKA KILELELNI
#2,TATIZO SI RASILILMALI ZILIZOPOTEA
#3, NYUMA YA USHINDI
Hivi ni vitabu vitatu ambavyo ukivisoma utapata kuelimika sana na kupata maarifa zaidi.
Vitabu viwili vya mwanzo vinapatikana kwa shilingi 10,000 kila kimoja. Na kitabu cha pili kinapatikana kwa shilingi 2,000 tu za kitanzania.
Vitabu hivi ni soft copya na vinatumwa kwako popote pale ulipo katika dunia hii.
Kikubwa sana unapaswa kulipia vitabu hivi kupitia nambari 0755848391 jina GODIUS RWEYONGEZA baada ya hapo nitumie ujumbe wenye jina la kitabu ambacho umenunua na utapokea kitabu punde baada ya wewe kutuma pesa.
Asante sana, tukutane kwenye mzunguko wa wanamafanikio
Ndimi, rweyongeza godius


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X