Mwanafunzi Ni Zaidi Ya Mwalimu Wake …


Waswahili wana usemi ambao wanasema kwamba mwanafunzi hawezi si zaidi ya mwalimu wake. Ila katika hali ya kawaida kitu ambacho si, kinaweza pia kuwa ni…. Hivyo mwanafunzi anaweza kuwa ni zaidi ya mwalimu wake. Isipokuwa ni kwamba mwanafunzi akishakuwa ni zaidi ya,, asimsahau yule aliyemwezesha kuweza kufika hapo alipofika. Naye ni mwalimu.
Kama mwanafunzi hapaswi kusahau kwamba suala zima la kujifunza huwa halina mwisho. Yaani ni kitendo cha kila siku kuanza januari mpaka disemba. Mwanafunzi wa kweli huwa hana mapumuziko. Yaani huwa hana siku ambapo atasema kwamba leo nimehitimu.

soma zaidi: wanavyokamata Ngedere Nchini India, (Jifunze Kutoka Kwa Viumbe Hawa)

Kitu cha kufanya leo ni kuhakikisha kwamba unajifunza ujuzi mpya. Na hakikisha kwamba hauachi kujifunza mpaka pale siku yamwisho ya wewe kuondoka hapa duniani. Endelea kujifunza kutoka kwa mwalimu yule, lakini pia jifunze kutoka kwa watu wengine. Asante sana, tukutane kileleni.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X