VITU VITANO (05) VYENYE THAMANI ZAIDI HAPA DUNIANI


Je, ushawahi kujiuliza ni vitu gani vyenye thamani kuliko vitu vingine hapa duniani? Je, vitu hivyo ni vipi? Sijawahi kumuuliza rafiki au ndugu yangu swali kama hili hapa, ila nina uhakika nikiwauliza watu walio wengi majibu ambayo watanipa yatakuwa ni majibu ya vitu kama magari, ndege, nyumba za kifahari na vitu vingine vya aina  hiyo.
Hata hivyo hapa duniani, vitu vyenye thamani kubwa sana si vile ambavyo vinanunuliwa na pesa. Bila shaka umewahi kusikia watu wakisema, pesa inaweza kununua kitanda lakini sio usingizi, inaweza kununua pete lakini sio ndoa, inaweza kununua kalamu lakini sio elimu, inaweza kununua dawa lakini sio afya….
Hapa sio kwamba ninaukataa ukweli kwamba pesa sio muhimu. Hasha, pesa ni muhimu sana. kiukweli pesa ni jambo la pili hapa duniani kwa umuhmu baada ya hewa ya oksijeni kwa umuhimu. Ila kuna vitu vina thamani zaidi na havishikiki kwa mkono. 
SOMA ZAIDI; mambo ya kuzingatia ili kuchagua fursa sahihi
Na vitu hivyo ni
##AFYA
##AKILI

##KUJITUMA
##MUDA
##NGUVU
Ni ukweli usiopingika kwamba vitu hivi vina thamani kubwa sana kuliko pesa yenyewe. Na vitu hivi havishikiki. Kumbe tunaweza kumalizia  kwa kusema kwamba vitu visivyo shikika ndivyo vitu vyenye thamani kubwa sana.

Ndimi
Kocha Godius Rweyongeza
0755848391
godiusrweyongeza1@gmail.com


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X