Kutoka sifuri mpaka kileleni ni kitabu ambacho kimeandikwa kwa wakati muafaka kikikulenga wewe ambaye una ndoto ya kufikia eneo kubwa sana maishani. Yaani kileleni.
Ndani ya kurasa za kitabu hiki utapata kujifunza vitu kadha kadha ambavyo vitakufanya wewe uzidi kusonga mbele kila siku.
1. Utapata kujua kama unaishi au uko hai. Maana hivi vitu ni viwili ila vyente utofauti mkubwa sana. Ndani ya kurasa za kitabu hiki utapata kujifunza kwamba kuishi ndio suala la msingi ambalo unapaswa kulipigania hapa duniani.
Soma Zaidi; Vitu Utakavyojifunza Kwenye Kurasa Za Kutoka Sifuri Mpaka Kileleni
2. Je, ushawahi jujiuliza umuhimu wa umoja?
Ninajua umewahi kuambiwa umoja ni nguvu. Ninajua pia umewahi kusikia kwamba kwa pamoja tunaweza. Bila shaka pia utakubaliana na mimi kwamba umoja ni ushindi.
Ndani ya kurasa za kitabu cha kutoka sifuri mpaka kileleni, utapata kujifunza juu ya umuhimu wa umoja.
Utapata pia kujua njia sahihi ya kusimama kwenye mabega ya watu wengine ili uzidi kusonga mbele.
3. Je, unayo malengo? Je, unataka kwenda wapi? Kwa nini unataka kwenda huko? Je, kuna kitu gani ambacho kinakuvutia?
Kuna watu wengi sana wanatembea katika maisha. Bila ya kuwa na malengo. Hawajui wanaenda wapi. Na hawajui jinsi ta kuweka malengo. Ndani ya kurasa za kitabu hiki hapa utapata kujifunza jinsi kuweka malengo. Na hatua kwa hatua jinsi ya kuweza kuyafikia.
Huwa napenda kusema kwamba hata kama wewe ni kilaza na hujawahi kuweka malengo, kwa kusoma kitabu kile lazima tu utapata kujifunza jinsi ya kuweka malengo. Na utayaweka.
4. Marafiki ni watu muhimu sana kwetu kufikia mafanikio. Lakini pia rafiki wanaweza kuwa ni kikwazo cha wewe kusonga mbele. Ndani za kurasa za kitabu hiki utajua umuhimu wa marafiki katika kuhakikisha kwamba unasonga mbele. Lakini pia utajifunza jinsi ya kukaa na marafiki sahihi.
5. Je, unamjua mtu anayehusika na maisha yako? Je, ni nani huyu?
Ndani ya kurasa za kutoka sifuri mpaka kileleni utapata kumfahamu jamaa huyu. Na huyu ni wewe. Kama sio wewe ni nani? Kama sio sasa ni lini?
6. Rafiki yangu mpaka hapo najua utakuwa unasema nimekuelewa lakini sina muda hata kidogo wa kufanya hayo unayoyasema. Wala nasemaaa, usihofu. Suala zima.la muda limeelezwa kwa undani.
Ukiujia umuhimu wa sekunde moja utakuwa umejua umuhimu wa dakika.
Ukiujua umuhimu dakika utakuwa umejua umuhimu wa saa,
Ukiujua umuhimu wa saa utakuaa umeujua umuhimu wa siku.
Ukiujua umuhimu wa siku utakuwa umeujua umuhimu wa wiki,
Ukiujua umuhimu wa wiki utakuwa umeujua umuhimu wa mwezi……
Hapa kuna nondo za kutosha.
7. Hahah! Naona unanielewa ila unasema utafanya kesho! Duuh, ngoja kidogo kabla hujaamua kufanya kesho . Naomba nikupe challenge ya kufanya sasa hivi. Kwa nini usianze sasa hivi?
Ndani ya kurasa za kutoka sifuri mpaka kileleni utapata kujua kwamba KESHO SIO SIKU. Ndio kesho sio siku.
Siku za juma ni jumatatu, jamanne, jumatano, alhamisi, ijumaa jumamosi na jumapili.
Sasa hapo kesho ipo? Umeiona wapi kesho?
Kwa hiyo hapa namalizia kwa kusema kwamba kesho sio siku.
8. Umefurahi kweli rafiki yangu. Ila bado unajiuliza vipi mbona mimi sina kipaji cha kuanza. Mbona waliofanikiwa ni watu wenye vipaji?
Na, mimi nakwambia hivi, unasema hivyo kwa sababu tu hujaweza kugundua kipaji chako. Unasema hivyo kwa sababu hujui kipaji chako ni kipi?
Ukishika KUTOKA SIFURI MPAKA KILELENI mkononi mwako, nina uhakika haitakuchukua zaidi ya saa kabla ya wewe kuweza kugundua kipaji chako.
Kama mpaka sasa hujui kipaji chako unapiga mazoezi ya mgambo. Lakini Ukikijua utaanza kupiga mazoezi ya kikomando. Kumbuka, huwezi kuwa komando kwa mazoezi ya mgambo.
9. Je, umewahi kusikia habari za kwamba hakuna haraka barani afrika. Je, umewahi kusikia habari za kwamba waafrika huwa wanawahi mazishi tu! Sasa ndani ya kurasa za kitabu hiki utapata kujua umuhimu wa muda kwa undani na kwa nini unapaswa kuwahi.
10. Je, mpaka hapo tupo pamoja rafiki? Niendelee,
Sasa naomba uchukue kitabu hiki na uwe nacho mkononi mwako. Kwa hakika utapata kujifunza mengi zaidi kuliko ambavyo umewahi kujifunza katika historia ya dunia.
Kama mwaka huu unapaswa kusoma kitabu kimoja basi soma, KUTOKA SIFURI MPAKA KILELENI. Nina hakika kitakutoa sifuri kweli, na kukupeleka kileleni.
JINSI YA KUPATA KITABU.
Gharama ya kitabu hiki Ni elfu 10 tu ya kitanzania.
Pesa inatumwa kwenda 0755848391 jina GODIUS RWEYONGEZA, baada hapo nitumie ujumbe mfupi kwenye namba hiyo hiyo. Utapokea kitabu chako baada ya kutuma email yako.
Ndimi,
Godius Rweyongeza
0755848394
Asante,
One response to “KITABU, KUTOKA SIFURI MPAKA KILELENI”
[…] Soma kitabu cha kutoka SIFURI MPAKA KILELENIUnataka kufikia malengo yako mwaka 2022? Upo siriazi kabisaaa na malengo yako? Basi soma kitabu cha […]