Vitu Vitano Vya Kukusaidia Kuendelea Kuwasha Moto Wa Kufanikisha Malengo Yako.


Lengo lilikuwa ni kukufungua na kukuonesha kuwa mwaka huu mpya umeuanzaje au ndio kwanza unazubaa zubaa.

Nadhani ambao huwa hawasahau ni wenye lengo la kuoa/kuolewa tu!!
Maana wakikupa kadi hata kama ni Januari na wanafunga ndoa mwezi wa tisa.  Halafu ukajichanganya ukatoa ahadi, watakudai ahadi yako mpaka utoe senti ya mwisho…

Naona unacheka! Umekumbuka ule ujumbe unaokukumbusha kutimiza ahadi yako nini?

Sasa leo nataka nikuulize kwa mara nyingine, hivi bado kweli unakumbuka lengo lako la mwaka huu? Bado kweli una motisha ya kulifanyia kazi?
Bado unajisukuma kulifanyia kazi?

Kwa hiyo, hakikisha kila siku asubuhi unajikukumbusha malengo yako, mchana unajikumbusha malengo yako, jioni unajikumbusha malengo pia.

Jikumbushe malengo yako pia unapokwama au unapokuwa katika hali  ya sintofahamu.

Kila siku jipe jukumu la kufikiria mawazo 10 ambayo unaweza kuanza kufanyia kazi mara moja ili yakusaidie kufanikisha lengo lako.
Ushawahi kufanya hili zoezi.
Lianze leo hii.
Anza sasa hivi ni mawazobyapi 10 ambayo unaweza kufanyia kazi leo hii yakakusaidia kusogea karibu na lengo lako?
Je, ni kuanza kusoma kitabu fulani…
Je, ni kupiga simu..
Je, ni kuonana na MTU fulani..
Je, ni kuachana na tabia fulani…

Ni nini sasa…ebu andika chini.

Bado huamini tu, najua kuamini kwa mwafrika ni mpaka aguse πŸ˜‚πŸ˜‚. Haya, pata nakala yako sasa hivi ili ujionee mwenyewe.
Nakala ngumu ni elfu 20. Na nakala laini ni elfu 10. Tuwasiliane Sasa hivi kwa 0755848391.

Niache kwanza niendelee mbele maana safari bado…

Toa ripoti kila Mara kwake ili aweze kuona maendeleo yako. Ukikwama mshirikishe ili akuoneahe namna unavyoweza kuendelea mbele zaidi…

Iko hivi, lengo huwa halitimii kwa siku moja mwishoni mwa mwaka. Kila siku Ni siku yako kufanyia kazi lengo lako.

Huwezi kuweka lengo na kusubiri lengo Hilo lije kutimia mwishoni mwa mwaka. Lengo lako linapaswa kufanyiwa kazi kila siku. Jumatatu mpaka jumapili, siku saba za wiki.

Pambana kila Mara kuhakikisha unalifanyia kazi.

Bado unataka niendelee au umechoka?
Umechoka eti!
Kama bado una motisha na nguvu zaidi kama Mimi, weka jina lako na email yako ili niendelee kukupa mafunzo yalioenda shule kama hili kupitia email. Fanya hivyo Sasa hivi hapa chini πŸ‘‡πŸΏπŸ‘‡πŸΏ


2 responses to “Vitu Vitano Vya Kukusaidia Kuendelea Kuwasha Moto Wa Kufanikisha Malengo Yako.”

  1. SOMO ZURI SANA NAJIFUNZA MENGI KWAKO SICHOKI KUSOMA MAKALA ZAKO. YAANI, UNASOMA KITU UNAKIELEWA NIMEJIKUTA KUKITAMANI KITABU CHAKO CHA SIFURI HADI KILELENI NIPE MAWASILIANO NIKUTUMIE HELA LEO

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X