Kitu Kimoja (01) Muhimu Kuhusu Muda


Habari ya siku hii ya leo rafiki yangu na ndugu msomaji wa makala kutoka katika blogu yako ya songa mbele. Imani yangu leo ni siku bora sana kwako na unaenda kuweka juhudi kuhakikisha kwamba unafanya makubwa sana ndani ya siku hii ya leo.

Moja kati ya rasilimali muhimu sana ambayo ni lazima tuitumie vizuri sana ni muda.
Muda ni rasilimali nzuri ambayo kila mtu anayo sawa na mwingine. Kila siku mpya inapoanza unakuwa na masaa 24, sawa na rafiki yako. Lakini je, unautumiaje.

Hata mtu aliye gerezani kwa siku anayo masaa 24. Cha ajabu sana ni kwamba tunaruhusu rasilimali hii itumiwe na watu waliotuzunguka kadri wanavyopenda bila ruksa yetu.

Rafiki, leo hii napenda ujue kitu kimoja tu kuhusu muda. Ni kwamba ukipita, ndio umepita. Yaani sekunde ikienda ndio imeenda. Hata sekunde moja ambayo imepita kabla ya wewe kusoma mstari huu hapa imeshapita wala hutakuja kuipata maisha yako yote.

Rafiki yangu ukilifahamu jambo hili muhimu sana juu ya muda hata siku moja hutakuja kuupoteza muda. Badala yake utahakikisha kwamba unaitumia kila sekunde ambayo inakuja mbele yako.

Rafiki yangu, kila wakati kila muda na kila sekunde, jua kwamba muda unaopita ndio umepita hivyo jitahidi kila unapoamka.asubuhi kuipangilia siku yako katika namna ambayo hutakuja kupoteza muda hata kidogo.

Ipangilie kila sekunde inayokuja mbele yako rafiki yangu. Tukutane kwenye meza ya wanafanikio

Ndimi,
Godius Rweyongeza.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X