MAKALA MAALUM KWA WATU MAALUM; Kwa Nini Kusoma Vitabu


Katika zama za sasa hivi tulizopo kuna vitu ni rahisi sana kuvipuuzia na kuna vitu inakuwa ni vigumu kuvipuuzia.
Kuna vitu vinavutia kuvifanya na kuna vitu havivutii kufanya.

Mfano kuchati na kufuatilia habari nyepesi nyepesi kwenye mitandao ya kijamiii kunavutia sana kuliko kukaa chini na kusoma kitabu.

Ndio maana watu walio wengi wanatumia muda mwingi sana katika kuchati zaidi ya kusoma.

Japokuwa kuchati kunaweza kuonekana kwamba kunapendeza na akili yetu inapenda, bado suala zima la kwamba kusoma vitabu ni muhimu sana. Hili hapa halina upinzani. Hivyo sina jinsi labda kukushauri kwamba ufanye maamuzi sahihi sasa hivi na uanze kusoma vitabu.
Zifuatazo ni faida za haraka utakazozipata kwenye kusoma vitabu.

Soma Zaidi; Usibadili Kioo

1. Uwezo wako wa kufikiri utaongezeka sana. Tofauti na mitandao ya kijamii ambayo inakupunguzia uwezo wa kufikiri kwa kukupa vitu rahisi rahisi, vitabu kila mara vitakupa kitu cha kukufikirisha zaidi na zaidi.

2. Vitakupunguzia makosa.
 Huwezi amini kupitia kusoma vitabu utapata maarifa ya kukutosha wewe hapo kuchukua hatua kadha wa kadha. Mfano, badala ya wewe kufanya makosa ya miaka saba au nane iliyopita. Vitabu vitakuonesha watu waliowahi kufanya makosa kama hayo na kwa jinsi hiyo utaweza kusonga mbele na kutatua changamoto zinginezo.

3. Vitabu vitakukutanisha na watu ambao hujawahi kukutana nao.
Sasa hivi kuna watu ambao ukisema unataka kukutana nao, ni vigumu kwako kukutana nao uso kwa uso. Inaweza kukuchukua miaka.mitatu mpaka kumi kukutana na Donald Trump uso kwa uso, lakini itakuchukua dakika chache sana kwako kuweza kukutana naye kwenye kitabu. Hivyo rafiki yangu ukitaka kukutana na mtu tafuta kitabu chake ukisome.
Haya ndio machache ambayo napenda kukushirimisha rafiki yangu

Ndimi,
Godius Rweyongeza
0755848391
www.songambeleblog.blogspot.com

KUPATA KITABU CHA KUTOKA SIFURI MPAKA KILELENI BONYEZA HAPA

KUPATA KITABU CHA TATIZO SI RASILIMALI ZILIZOPOTEA BONYEZA HAPA

HUDUMA NYINGINE UNAZOWEZA KUPATA KWANGU HIZI HAPA


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X