Hili Ni Kosa Ambalo Wajasiliamali Wengi Hufanya


Habari ya siku hii njema sana rafiki yangu na ndugu msomaji wa blogu yako ya SONGA MBELE. Imani yangu kwamba leo ni siku njema sana kwako na unaenda kufanya kazi kwa juhudi kubwa sana. Hongera sana kwa siku hii ya leo.

Siku hii ya leo napenda nikwambie kosa moja ambalo wajasiliamali walio wengi sana hulifanya bila kujua. Na kosa hili hatimaye huwafanya wasiweze kusongambele na kupanuka zaidi.
Kosa hili sio lingine bali ni wajasiliamali kutaka kufanya kazi kwa kushindana.
Yaani wanashindana na mtu ambaye anafanya biashara kama wanayofanya wao.
Sasa swali la msingi na la kujiuliza hapa kuna shida gani katika kushindana?
Shida kubwa ya kushindana ni kwamba haikufanyi wewe kama wewe kuweka malengo makubwa. Pia haikupi mwanya wa wewe kufikiri na kubuni kitu kipya kwenye biashara yako. Badala yake nguvu, muda na uwezo wako mwingi unakuwa unauwekeza katika kutaka kujua mwenzako kabuni nini ili na wewe ufanye kile alichofanya.
Hali kama hii haikujengi, wala haikufanyi wewe uzidi kusongambele.

Soma zaidi: A NOTE FROM SONGAMBELE; GO STRAIGHT TO THE POINT

Sasa hapa nifanyeje?
Kama mpaka leo unaposoma hapa una malengo ya kushindana na mtu yafute kwanza na yaweke pembeni.
Weka malengo mapya ya kutawala.
Badala ya kuwa na malengo ya kwamba uangalie rafiki yako kafanya nini ili na wewe uige. Weka malengo ya kutawala. Katika kile kitu ambacho unafanya, hakikisha kwamba unatawala. Usiache kufanya, usiogope kufanya, endelea kusongambele maana wewe upo kwa ajili ya kuhakikisha kwamba unatawala katika kile.kitu ambacho unafanya.

SOMA ZAIDI; KONA SONGAMBELE: Zaeni Mkaongezeke

Kama utaendelea kushindana hutakuja kutawala.
Kamusi ya kiswahili sanifu inazungumzia kutawala kama neno ambalo linatokana na neno tawala.
TAWALA maana yake ni mudu kitu kwa kiwango cha juu. Hii ndio kusema kwamba huwezi kumudu vitu kwa viwango vya juu kama kila wakati wewe ndiye unaangalia wengine wanafanyaje ili na wewe utokee hapo au uige.
Hii ndio kusema kwamba juu yako kunakuwa na watu ambao wanatawala na wewe unaiga hapo.
Sasa hili halipaswi kuwa lengo lako hata siku moja.
Lengo lako linapaswa kuwa kubwa sana. Yaani unapaswa kuwa na lengo la kutawala.

Kazi ya kufanya siku hii ya leo. Weka malengo yako katika sekta kuu tano muhimu.
Andika ni jinsi gani utatawala katika hayo maeneo.
Nenda zaidi kwa kuonesha hatua utakazochukua ili kuhakikisha kwamba unawezankufikia malengo yako.
Asante sana,
Tukutane kwenye meza ya wanamafanikio.


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X