Je, Sehemu Yako Ya Kusimamia Ni Ipi?


Kuna wakati kuku huwa anaficha mguu mmoja na kusimama kwa mmoja. Kuna wakati paka huwa anasimama kwa miguu yake ya nyuma na kuiacha miguu ya mbele ikielea.

Hii ndio kusema sehemu zinazotupa uhakika zipo kila wakati na kwa kila mtu, ila kuna wakati tunapaswa kuzikataa na kutafuta sehemu bora zaidi.

Ndio maana kila siku tunaalikwa kuhakikisha tunajaribu kufanya kitu kipya. Tusikubali tu kuendelea kuridhika na kitu kile kile kila siku. Ebu ufikie wakati tunanyue miguu yetu ya mbele na kujitosa katika kufanya kitu kipya.

Kuna usemi unaosema kwamba, sijawahi kushindwa hajawahi kujaribu. Kwa lugha nyingine sijawahi kushindwa ni yule ambaye kila wakati anasimama na miguu yake yote miwili. Na hataki kuunyanyua hata mmoja. Ila ifahamike kwamba, ili ufanikiwe utapaswa kuanza kunyayua mguu wako kwanza. Nyanyua mguu wako. Unyayue tena na tena. Usiridhike na hali ya sasa. Usiridhike tu na kile ulichonavho sasa, maana una kitu cha ziada ambachon unaweza kufanya.

Igundulike kwamba kile ambacho tayari kinaonekana ni kidogo sana kulinganisha na kile kilicho ndani yako. Ndio maana kile ambacho umekitoa hupaswi kuridhika nacho.

Tafuta kupata kikubwa zaidi. Malengo uliyitimiza sasa yasiwe chanzo cha wewe kuridhika na kusimama chini kwa miguu miwili. Weka juhudi. Songambele, simama na simama tena bila kuchoka.

Asante sana,
Tukutane kwenye meza ya wanamafanikio.

Ndimi,
Godius Rweyongeza
0755848391

KUPATA KITABU CHA KUTOKA SIFURI MPAKA KILELENI BONYEZA HAPA


HUDUMA NYINGINE UNAZOWEZA KUPATA KWANGU HIZI HAPA


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X