Hiki Ni Kitu Ambacho Unapaswa Kuachana Nacho Mara Moja


                                                        
Habari ya siku hii njema sana rafiki yangu. Hongera sana kwa siku hii ya leo. Imani yangu kwamba u mzima wa afya na leo kama kawaida unaenda kufanya kazi kwa juhudi kubwa sana. kitu kitakachokufanya wewe uweze kufikia mafanikio makubwa sana,
Mara nyingi sana tumekuwa tunaongea na kuelimisha na juu ya mambo ya msingi ya kufanya ili uweze kufikia mafanikio.  Najua mpaka sasa hivi unajua kwamba malengo yako ni muhimu sana kwako kuweza kufikia mafanikio makubwa sana. Najua pia unajua kwamba ili ufanikiwe unahitajji kuwa na nidhamu, unapaswa kujituma  na unahitaji uadililfu. Hongera sana kwa hilo.
Ila ili uweze kufanikisha malengo kuna vitu hutapaswa kufanya kabis kwenye maisha yako. ndio kuna vitu ambavyo hutapaswa hata kuvigusa. Leo hii tutaona kitu kimoja cha muhimu sana ambacho  kwa hakika hutapaswa kukifanya. Na kitu hiki sio kingine bali ni KUBEBA MZIGO USIOSITAHILI KUUBEBA. Hiki ni kitu ambacho hupaswi kuwa nacho kwenye safari yako ya kuelekewa kwenye malengo yako makubwa ya mbeleni. Kama kuna kitu hupaswi kuwa nacho, basi usijishughulishe nacho. Kama kuna mahusiano unaona wazi wazi kwamba hapa huyahitaji. Achana nayo.
Kama una tabia ambayo unayo ila unaona wazi wazi kwamba tabia hii ni mzigo kwako, achana nayo.
Kuna vitu vingi sana ambavyo ni mzigo kwako na hupaswi kuvibeba kamwe kuelekea kwenye safari yako ya mafanikio. Kaa chini na uangalie mizigo hii na jinsi utakavyoachana nayo.
Hapa ninakuwekea baadhi ya mizigo ambayo unapaswa kuitua mara moja. Yaani hupaswi kuchelewa kuondokana nayo. Na mizigo hii sio mingine bali
Kama unavuta sigara, huu ni mzigo ebu utue sasa  hhivi ili uweze kufikia mafanikio yako vizuri
Kama unakunnywa pombe, huu nao ni mzigo utue
Kama unatumia muda mwingi sana kupiga soga kwenye vijiwe na watu, TUA MZIGO HUU.
Kama unatumia muda mwingi mtandaoni na hauingizi chochote, EBU TUA NA MZIGO HUU,
Kama unaamka saa mbili za asubuhhi na kujiambia kwamba sasa leo umeamka mapema, rafiki yangu unahitaji kufikiri upya juu ya maisha yako. UNAPASWA KUTUA MZIGO HUU PIA.
Tua, mizigo, tua mizigo tua mizigo
Yaani hakikisha unaiendea safari yako ya mafanikio bila ya kuwa na kikwazo ambacho kinakuzuia wewe kuweza kusonga mbele.
Asante sana rafiki yangu, tukutane kwenye jukwaa la wanamfanikio.
Rafiki yangu, sasa


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X