Vitu Vinavyokufanya Utangetange Kila Mahali


Habari ya siku hii njema sana rafiki na ndugu msomaji wa makala haya kutoka kwenye blogu yako pendwa ya songambele. Imani yangu kwamba leo ni sikku njema sana kwako na unaenda kuweka juhudi kuhakikisha kwamba unafanya kazi kwa bidii, kujituma na kuhakikisha kwamba unafikia malengo yako. hongera sana rafiki yangu kwa siku hii njema sana.
Hivi ushawahi kujiuliza kwa nini huwa unagusa kitu hiki na kuacha na kwenda kugusa kitu kingine na kuacha na kufuata kungine? Unajua kwa nini?
Ushawahi  kujiuliza kwa nini unaanzisha biashara na kuacha na kwenda kufanya biashara nyingine na unaposikia kwamba biashara fulani sasa ndio inalipa zaidi ya hii ambayo unayo kwa sasa hivi unaamua kuach na kwenda kuifuata hiyo?
Kama mpaka sasa umekuwa unatanga tanga kiasi hiki hapa, leo hii nipo hapa kukwambia kwamba sasa umefika wakati wako wa kujitulilza sehemu moja na kuhakikiisha kwamba unafanya kitu kimoja ambacho kinaeleweka na chenye manufaa makubwa sana kwako na kwa jamii nzima Kiujumla.
Kuna sababu kadha kadha ambazo zinakufanya utange tange kila mahali kila siku. Laiti kama utaziendeza sababu hizi utazidi kutanga tanga maisha yako yote.
#1. HAUNA MALENGO
Kitu kikubwa sana kinachokufanya utange tange kila mahali ni kwa sababu haujui ni kitu gani haswa unapaswa kufanya. Ndio maana unagusa hiki na kuacha na kugusa kitu kingine. Pasipo na malengo utafanya kila kitu kinachokuja mbele yako. rafiki yangu, jipange,
Acha mchezo huu wa kuigiza wa kugusa na kufanya kila kitu. Amua sasa kuwa wewe na kuanza kuishi. Weka malengo yako mahususi sasa na uanze kuyafanyia kazi sasa.
Weka malengo ambayo utayafanyia kazi kidogo kidogo  kila kukicha. Kamwe usitange tange na kuacha malengo yako yakiwa hayajatimizwa. Malengo yako yawe ndio mwongozo wako wa kuishi. Yakwambie kwamba unapasawa kufanya nini na hupaswi kufanya nini.
#2. UNAAMBIWA KWAMBA FURSA IMEPITA
Hivi ni mara ngapi watu wamewahi kuja kwako na kukwambia kwa ma fursa fulani ipo imekuja na usipoipokea basi ndio imeenda? Bila shaka ni  mara nyingi sana. lakini je, ni kweli kwamba huwa wakisema hivyo fursa huwa zinaisha kuja? Jibu ni hapana.
Watu wakitaka kuiteka akili yako watakwambia kwamba hii ni fursa ambayo haijawahi kutoke a kwenye dunia hii. Watakwambia ukiikosa ndio umeikosa. Hivyo na wewe kwa sababu hupendi kupitwa unajikuta kwamba unakimbizana nayo. Na hiki kinakuwa chanzo cha wewe kutanga ytanga. Ukwelli ni kwamba fursa zipo kila siku. Yaani kila kukicha ni fursa, kila uendapo ni fursa, kila unayekutana naye ni fursa. Hivyo ni mwendo wa fursa, fursa na fursa. Kwa hiyo usihadaike kwamba fursa fulani ikipita ndio mepita. Hakuna kitu kama hicho.
Kiufupi ni kwamba fursa ni kama magari ya daladala, likikupita hili, basi nyuma kuna jingine linakuja.
Hivyo sasa rafiki yangu kitu kikubwa sana ambacho unapaswa kufahamu  ni kwamba UNAPASAWA KUWA NA MALEANGO. Lakini pia USIKIMBIZANE NA KILA IITWAYO FURSA. Kwa kufanya hivi utapunguza kutanga tanga na kufanya kila kitu kinacho kuja mbele yako.
Asante sana rafiki yangu , tukutane kwenye meza ya wanamafanikio.


One response to “Vitu Vinavyokufanya Utangetange Kila Mahali”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X