Ifahamu Kanuni Ya Asilimia Moja Na Jinsi Ya Kuitumia


Hii ni kanuni ambayo ukiifahamu utaishi maisha mazuri na utafanya makubwa kwa nguvu kidogo sana.

Yaani, itakuwa kama unagusa tu na mambo yanajipanga.

Kulingana na kanuni hii ni kwamba, Kila siku kwako inapaswa kuwa ni siku ya kukua kwa asilimia moja tu.

Kama umeweka malengo basi siku ya leo yafanyie kazi kwa asilimia moja, na kesho yafanyie kazi kwa asilimia moja nyingine, hivyohivyo na kesho kutwa na siku zifuatazo. Baada ya muda hizo siku moja moja zitaunganisha nguvu na hizo asilimia moja moja zitaungana na kuleta matokeo mkusanyiko ambayo ni makubwa.

Kama una biashara, Kila siku ikuze kwa asilimia moja tuu. Leo ongeza bidhaa fulani ambayo watu wanahitaji ila hawapati kwako. Kesho boresha huduma kwa wateja
Kesho kutwa hakikisha hesabu za biashara zipo sawa n.k.

Baada ya muda nguvu ya riba mkusanyiko itafungamana na kutengeneza kitu Kikubwa.

Kama upo kwenye mahusiano unaweza kuitumia pia hii kuboresha mahusiano yako na kufanya nyumba yako kuwa mbingu hapa duniani . Kila siku, ifanye kuwa siku ya kuboresha mahusiano yako. Siku ya leo boresha mahusiano yako kwa asilimia moja tu. Leo unaweza kuandika barua ya kumpongeza mwenza wako kwa kupika wali mzuri.
Kesho ukamletea zawadi ya heleni.
Keshokurwa ukampa muda wa kuongea na wewe ili atoe ya moyoni. Kwa vyovyote vile hakikisha kila siku unakuza mahusiano yako kwa asilimia moja tu basi.

SOMA ZAIDI: Sheria Tano Za Nguvu Zitazokusaidia Kushinda Mengi Kwenye Maisha Ya Mtaani. Zifuate Kwa Faida Yako, Zivunje Kwa Hasara Yako

Unataka kusoma vitabu? Tumia kanuni hii hii katika usomaji. Kila siku soma kurasa kadhaa. Kurasa hizi zitakuongezea maarifa na kukufanya uwe bora kila kunapokucha.

PATA ZAWADI YA KITABU CHA BURE HAPA

Unataka kuamka mapema. Anza kesho kuamka saa 12 kasoro dakika moja. Kisha kila siku amka dakika moja kabla ya ile ya jana. Kama kesho kesho ukiamka saa 11 dakika 59, kesho kutwa amka saa 11 dakika 58 Utajikuta una uwezo wa kuamka muda unaotaka wew.

SOMA ZAIDI: Kuamka Asubuhi Na Mapema Ni Tabia (Njia Sita Za Uhakika, Zilizothibitishwa Na Zisizoshindwa Zitakazokuwezesha Kujenga Tabia Ya Kuamka Asubuhi Na Mapema)

Unataka kuandika kitabu? Andika maneno 500 kila kwa mwezi utakuwa umeandika maneno 15,000+. Maneno 500 siyo mengi Sana. Ila ukiyaandika kwa siku 30 mkusanyiko wake ni mkubwa Sana.

Unataka kufanya mazoezi? Tumia kanuni hiihii, leo Anza na push-up moja tu. Kesho piga push-up mbili. Keshokutwa tatu. Unaona eeh, yaani huhitaji kutunia nguvu kubwa kufanya mabadiliko. Unatumia nguvu kidogo ila unafanya mabadiliko makubwa. Hivi kweli hata muda muda wa kupiga push-up moja utakosa leo. Kweli?

SOMA ZAIDI: HUWEZI KUMKODISHA MTU WA KUKUPIGIA PUSH UP

Unataka kujifunza lugha mpya? Anza tu kwa kwenda dukani na kununua daftari ya kutumia kujifunza lugha. Kisha kila siku jifunze neno moja la ziada.
Kwenye kitabu cha KUTOKA UMASKINI MPAKA MAFANIKIO CHA ERICK SHIGONGO ameeleza alivyokuwa akijifunza misamiati kidogo tu ya kiingereza kila siku na hatimaye akawa MBOBEVU kwenye kiingereza.

Yaani, kwa kutumia hii nguvu unaweza kufanya chochote unachotaka hapa duniani. Hakuna kitakachokushinda.

Kitu kimoja labda ni kwamba Kuna uamuzi usipoufanya leo, muda utapita na utaishia tu kujuta kwa nini hukufanya uamuzi. Usipoanza kuweka akiba leo, miaka 10 ijayo utakuwa bado unalia kuwa huuna mtaji. Sasa si Bora tu uanze kutumia hii kanuni ya asilimia moja kuanzia leo.

Usipoandika kitabu chako leo hii, miaka 10 ijayo utakuwa unalalamikiwa kuwa ulikuwa na ndoto ya kuwa mwandishi ila hujaandika.

Mimi sitakuvumilia, ndio maana leo nimekwambia mapema ili uanze kuchukua hatua.

Kuna mzee mmoja alikuwa na ndoto ya kuwekeza kwenye kilimo cha miti tangu miaka 1990. Hakufanya hivyo kwa kuhairisha kila mara.
Vijana walikuja kupanda miti miaka ya 2005 na Sasa hivi wanakula matunda yeye anaishia tu kusema Bora ningepanda miti miaka hiyo.

Sitaki uje kujuta. Chukua hatua kuanzia leo hii. Inawezekana.

NB. Kama unataka kuachana na tabia mbaya, amua tu kuwa unaachana nazo mara moja. Usiache pombe kwa kanuni ya asilimia moja.
Usiache sigara kwa kanuni ya asilimia moja.
Usiache uzinzi kwa kanuni ya asilimia moja.

Hivi vitu amua tu kwamba unaachana navyo na muda uoiokuwa unautumia kufanya hivi vitu vibaya utumie kufanya vitu vya maana na vitu vya kukujenga.

Sambaza upendo, sambazabujumbe huu kwa rafiki zako pia.

Ni Mimi rafiki yako wa ukweli
Godius Rweyongeza

0755848391

Morogoro

,

7 responses to “Ifahamu Kanuni Ya Asilimia Moja Na Jinsi Ya Kuitumia”

  1. Kweli, Wenye maarifa ndio watakao tawala dunia hii. Unamaarifa kemkem baba.

    Namshukuru Mungu wa Mbinguni kwa ajili yako.

    Sitoacha kukufuatilia maana kwako kuna mzinga nitafuata nyuki (Makala zako) ile nile asali (Maarifa)

  2. Mungu akutunze uendelee kutupa maarifa hakika kanuni hizi nitaanza kuzifuata leo na ninaimani zitanisaidia kufika ninapohitaji

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X