365: ANZA KUTUMIA KILE ULICHONACHO


MADE IN AFRICA:  IMETENGENEZWA BARANI AFRIKA

Mbinu 366 Za Kujing’arisha barani Afrika

GODIUS RWEYONGEZA

MBINU YA 365:

ANZA KUTUMIA KILE ULICHONACHO

Mara nyingi watu huwa wanazunguka huku na kule kutafuta fursa. Na sio jambo la ajabu kukuta watu wamekaa tu kwa kisingizio cha kwamba hawana kitu au hawana kazi ya kufanya.  Na hapo hapo watu hao hao unakuta wanalia kwamba maisha ni magumu sana.

Lakini watu hao hao utagundua wana ndoto kubwa sana za kuandika vitabu, wana mawazo makubwa sana ya biashara, wana ndoto kubwa sana za kujulikana duniani, wana malengo ya kuwa viongozi wakubwa wa taifa hili hapa.

Wanasubiri fursa zimiminike na kuanguka kama maji ya mvua.  Je, wewe ni mmoja wapo?

Swali langu kwako ni Je, una nini mkononi mwako? Ni nini hicho ambacho unaweza kuanza nacho?

Siku zote vitendea kazi vikubwa sana vya kuanza kuitimiza ndoto zako unavyo hapo mkononi mwako. Yaani hauihitaji kwenda kuvitafuta mbali sana. Unahitaji tu just kuamua kuanza kuvitumia basi.

Fikiria juu ya mtu mwenye ndoto ya kuanzisha bustani na nyumbani kwake kuna eneo dogo halijalimwa na anasubiri apate hekari mia. Je, na huyu kweli hana pa kuanzia?

Au mtu anasema anataka shamba, wakati huo huo anaona watu wanachoma mbolea anacheka tu! Je, na huyu kweli kakosa mtaji.

Vitu vidogo vidogo ambavyo tunavyo sasa hivi ndivyo vyenye uwezo wa kutufanya tupate vikubwa zaidi. Nina hakika sio mara yako ya kwanza wewe kusikia kwamba mbuyu ulianza kama mchicha.

Kumbe rafiki yangu kama unataka kuwa mbuyu imara hapa barani Afrika, usiogope kuanza kama mchicha imara.

Asante sana
Tukutane kwenye jukwaa la wanamafanikio


One response to “365: ANZA KUTUMIA KILE ULICHONACHO”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X