Jambo Moja Litakaloikuza Biashara Yako Bila Kikomo


Hivi ni kitu gani kinawafanya baadhi ya watu kuweza kujingarisha na kukuza biashara zao bila kikomo, wakati huo huo kuna watu wanaanzisha biashara zinakufa?

Kwa nini baadhi ya biashara zimekuwepo kwa muda mrefu na zinazidi kuonekana zikikua zaidi zaidi?

Hapa lazima kuna siri. Lazima kuna kitu fulani hapa ambacho wamiliki wa biashara hizi kubwa wanakifahamu.

Kiukweli kitu hiki na kitu hiki sio kingine bali ni KUJITANGAZA.

Wapo watu wanaofikiri kwamba makampuni makubwa ni makampuni yanayotengeneza bidhaa zenye bora sana. Hapana, makampuni makubwa sio makamouni yanayotengeneza bidhaa zenye ubora sana. Ni makampuni ambayo yanatangaza bidhaa zao sana.

Unaweza kuwa na bidhaa nzuri sana lakini kama hutaitangaza watu wakaijua, rafiki yangu utabaki kuiona wewe mwenyewe tu.

Kwa hiyo kujitangaza na kutangaza bidhaa zako kila siku ni jambo la maana sana. Kila siku inayokuja mbele yako unapaswa kuhakikisha kwamba unajiuliza ni kwa jinsi gani unaenda kuitangaza bidhaa yako. Je, ni mbinu gani ambayo unaenda kuitumia kuhakikisha kwamba unaweza kuwafikia watu wengi zaidi na zaidi.

Soma zaidi; Maswal Muhimu Ya Kuzingatia Kabla ya Kuingia Katika Ujasiliamali

Kila siku inayokuja ni siku ambayo wewe unapaswa kuhakikisha kwamba umewafikia wateja wapya kwenye biashara yako. Na ili uweze kuwafikia wateja hawa, basi hakuna jinsi isipokuwa wewe kuhakikisha kwamba unafanya matangazo. Fanya matangazo kila siku, itangaze biashara yako. Ili uweze kuijenga bishara yako na kuifanya iimarike zaidi na zaidi.

Asante sana rafiki yangu.

Tukutane kwenye meza ya wanamafanikio.

Ndimi,
Godius Rweyongeza
0755848391

KUPATA KITABU CHA KUTOKA SIFURI MPAKA KILELENI BONYEZA HAPA


HUDUMA NYINGINE UNAZOWEZA KUPATA KWANGU HIZI HAPA


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X