MUDA WA ZIADA; Sehemu Moja Muhimu Ambayo Unaweza Kupata Muda Wa Kufanya Kazi Zako Ambazo Ni Tofauti Na Ajira


Habari ya siku hii ya leo rafiki yangu. Hongera kwa siku hii nyingine nzuri sana kwako rafiki. Leo ni siku njema sana, hivyo hakikisha kwamba unaitumia leo hii kufanya makubwa sana.

Mara nyingi sana unapoona watu wanaweza kufanya kazi fulani nyingi nyingi na kuziwezea basi unahisi kwamba hawa watu wana kipaji cha kipekee sana.

Mfano ukimwona Mchezaji maarufu anacheza kwa kiwango cha juu, basi unaanza kusema kwamba huyu hapa kazaliwa na kipaji cha kipekee.
Au pengine utasema ni mazingira anayoishi ndio yanamfanya kuwa jinsi alivyo.

Ngoja nikwambie kitu. Unachoongea ni kweli. Huyo unayemwona anacheza mpira vizuri na huyo huyo unayemwona akiimba nyimbo nzuri na maarufu. Basi ana kipaji. Pia mazingira yake yanamruhusu kufanya hivyo. Yaani juu ya hilo hata sikatai.

Soma Zaidi: Kipaji Ni Nin?

Sasa swali langu kwako? Kipaji chako kipo wapi? Tofauti kati yako wewe na huyu unayemwona kwenye TV imelala kwenye matumizi ya kipaji. Yeye ameamua kukitumia kipaji chake vizuri sana na wewe hata hujishughulishi kutumia kipaji chako.

Yeye anajitengenezea mazingira mazuri ya kutumia kipaji chake, wewe unapoteza muda kulalamika na kupiga kelele kila wakati.
Hapa ndipo ilipo tofauti.

Sasa rafiki yangu ili na wewe uweze kuingia kwenye asilimia za watu wachache sana ambao wanafanya mambo makubwa sana. Yaani watu wachache sana ambao wanatumia vipaji vyao, watu wachache sana ambao wanasifika kwa kuuza, watu wachache ambao wanamahusiano mazuri. Basi utapaswa kujitengenezea muda, ndio muda wa kutosha. Na muda huu uutumie kufanya kitu ambacho kitakufanya uzidi kusonga mbele kila wakati.

Soma Zaidi: Hivi Ndivyo Unaweza Kutengeza Kazi Inayokonga Nyoyo Za Watu

Unaweza ukawa umeajiriwa sehemu au una kazi fulani lakini ukawa unautumia muda huu kufanya kazi nyingine ambayo wewe unaipenda na kazi ambayo inakufanya uzidi kuinua kipaji chako.

Unaweza ukawa wewe ni polisi lakini unapata muda huu kuendeleza kipaji chako cha kuimba.

 Unaweza ukawa wewe ni mwalimu lakini ukautumia muda huu kuanzisha biashara yako ya ziada ambayo itasaidia maisha ya watu wengi.

Hivi ndivyo maisha yanavyoenda. Na hivi ndivyo hawa watu wachache sana ambao wewe unaona kwamba wameweza kufanya mambo makubwa sana  walifika huko. Ndivyo watu hawa wenye vipaji wameweza kuviibua, kuviinua na kuendeeleza vipaji vyao.

Sasa, bila shaka mpaka hapo utakiwa unajiuliza muda huu nitaupata wapi?

Rafiki yangu, muda huu utaweza kuupata kwa KUAMKA MAPEMA.

Kuamka mapema asubuhi kabla watu wengine wote hawajaamka. Wakati watu wengine wote wakiwa wamelala, hapo ndipo utapata kufanya vitu viwili vikubwa.

1. UTAPATA MUDA WA KUENDELEZA KIPAJI CHAKO.
Badala ya wewe kusema kwamba watu fulani (wazungu) wana bahati, utaanza kuona bahati inakufuata wewe maana bahati siku zote inamfuata mtu aliyejiandaa kuipokea. Kwa hiyo mazoezi ya kuinua kipaji chako ni KIITA BAHATI.
 Hakikisha unakuwa na muda huu kila siku.

Kama tayari umeshaanza kuutumia vyema muda huu. Basi kuna kitu kikubwa sana cha kuongeza. Ni kwamba utapaswa  kuangalia ni kitu gani kimoja ambacho leo unaweza kufanya ili kuweza kuvuta watu zaidi, kuongeza mauzo zaidi au kuendelea kupata wateja zaidi. Huu ni muda wako.

Soma Zaidi: Usifanye Kitu Hiki Kikiwa Cha Kwanza Unapoamka Asubuhi

2.  UTAKUWA UMEJENGA MAZIGIRA AMBAYO UNAONA WENGINE WANAYO ILA WEWE HUNA
Yale mazingira unayosema kwamba wengine wanayo na wewe huna, basi wa wewe kuhakikisha kwamba unatengeneza mazingira haya ni palee asubuhi unapoamka.  hapa hakuna usumbufu, na haoa hakuna mtu wa kukupigia kelele. Hivyo yale mazingira unayosema wengine wanayo na wewe huna, muda mzuri wa kupata mazingira haya ni asubuhi.

Asante sana rafiki yangu
Tukutane kwenye jukwaa la wanamafanikio.

Ndimi,
Godius Rweyongeza
0755848391

KUPATA KITABU CHA KUTOKA SIFURI MPAKA KILELENI BONYEZA HAPA


HUDUMA NYINGINE UNAZOWEZA KUPATA KWANGU HIZI HAPA


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X