TOO BUSY TO WATCH YOUR DREAM; Hatua Sita (06)Za Kukutana Na Watu Maarufu, Wafanyabishara Wakubwa Na Wanamziki Nguri Bila Kutumia Nguvu


Kwa kawaida huwa sipendi kutumia kiingereza katika maandishi yangu labda pale ambapo huwa ninakazia kitu fulani hapo ndipo huwa nalazimika kutumia kiingereza ili uweze kuelewa zaidi.

Makala ya siku hii ya leo imebeba kichwa chenye lugha ya kiingereza. Na kwa sababu kuna kitu kikubwa sana nakazia basi itabaki hivyo hivyo.

Samahani sana kama utakuwa hujaelewa kichwa cha makala, ila nina uhakika utaelewa ujumbe ulioandikwa kwenye makala haya.

Endapo utaona umesoma nusu ya makala haya na huoni mwelekeo wa kuelewa kitu chochote au kupata kitu chochote cha kufanyia kazi, basi achana nayo. Kafanye kazi nyingine inawezekana makala hii haikufai wewe inawafaa watu wengine. Asante na karibu sana kwenye makala ya siku hii ya leo.

Watu wapo bize (busy), bize kweli kiasi kwamba muda wa kukaa na kuanza kukufikiria wewe hapo hawana. Watu wapo busy. Bila shaka mpaka hapo unajiuliza hivi huyu Godius Rweyongeza anataka kusema nini.

Nataka kusema watu wapo bize. Najua mara nyingi watu wangependa ndoto zao wawashirikishe watu wakubwa sana, na wao waitikie papo hapo na kuwasaidia.

Mwingine sasa hivi anawaza yaani sasa hivi nikikutana na Raisi Magufuri nikamwambia juu ya ndoto yangu ya kupata kazi. nitafurahi sana.

Mwingine anawaza juu ya kukutana na mwigizaji maarufu sana leo, ili amshirikishe kwenye tamthilia yake ambayo anafikiria kuiigiza.

Mwingine hajawahi kuimba wimbo mmoja wa bongo fleva ila anataka wimbo wake wa kwanza au wimbo wowote atakaotunga amshirikishe Diamond, Alikiba na wengineo maarufu.

Mwingine ana wazo la biashara, anataka Mengi, Mo Dewji au wengine wamsaidie kupata mtaji.

Tena mtu huyu anapata namba za watu hawa na kuwapigia ili wamsaidie juu ya ndoto yake hiyo, ila cha ajabu hawapokei.

Pengine akipokea anapokea msaidizi. Na pengine akipokea mwenyewe anapokea baada ya wewe kuwa  umemtafuta miezi sita mfululizo ukipiga simu kila siku, bila kupokelewa. Na baada ya kupokelewa anakwambia anaingia kwenye kikao mtaongea siku nyingine.

Watu wapo bize. Ndio maana leo nikaja na kichwa cha makala TOO BUSY TO WATCH YOUR DREAM.

Katika makala haya ya siku hii ya leo napenda ujifunze njia rahisi ya kuwapata maarufu na jinsi ambavyo unaweza kuwashirikisha kwenye ndoto zako bila kutumia muda mwingi sana. Lakini kikubwa unachopaswa kufahamu watu hawa maarufu, wapo bize, bize sana kiasi kwamba hawana muda wa kusikiliza vitu vidogo vidogo.
Sasa hatua sita za kuwapata watu hawa ni kama ifuatavyo;

1. NA WEWE ANZA KUWA BIZE.
Tumeona watu maarufu, wafanyabiashara, viongozi wa serikali na wengineo wako bize sana. Je, hawa watu wanafanya nini. Jibu ni rahisi sana, wanafanya KAZI. kumbe kama hawa watu ubize wao unatokana na kufanya kazi. Basi na wewe amua kuwa bize. Tafuta kazi ambayo unaona inakufaa, kazi unayoipenda na wewe kuwa bize kiasi kwamba usiwe na muda wa kufuatilia umbea, muda wa kuangalia TV, muda wa kusoma magazeti, muda wa kupiga soga. Be busy.

Kuna usemi wa kiingereza unaotuasa hivi, IF YOU CANNOT BEAT THEM, JOIN THEM. Ukimaanisha kama huwezi kuwapiga basi ungana nao.

Sasa badala ya wewe kulalamika watu hawa hawanijali, watu hawa hawana muda wa kunisikiliza, nakushauri uwe bize. Na wewe kuwa bize. Kiufupi ni kwamba ziangalie ndoto zako wewe mwenyewe maana wengine wapo bize hawataweza kufuatilia ndoto zako.

Hatua ya kwanza BE BUSY. Itafikia hatua watakutafuta.

2. WEKA MALENGO
Je, ni kitu gani kinawafanya watu hawa maarufu wanakuwa bize. Je, ni kazi pekee. Jibu ni hapana. Sasa nini hiki? Jibu ni kwamba
Watu wako bize wanatimiza malengo yao.

Kumbe  wafanyabiashara hawapo bize ilimradi waonekane bize, au hawapo bize kwa sababu wakatae kupokea simu zako, bali wapo bize wanatimiza MALENGO YAO.

Je, wewe unajua malengo yako ni yapi? Weka malengo yako leo. Na anza kuyafanyia kazi. Mwisho wa siku utakuwa unajua kweli upo bize ukifanya jambo fulani la maana.

Hatua ya pili be BUSY WITH GOALS. Kuwa bize na malengo, siku moja mtakutana kwenye meza ya wanamafanikio.

Soma zaidi: KITABU; KUTOKA SIFURI MPAKA KILELENI

3. WEKA VIPAUMBELE.
Je, watu ambao wako bize wanafanya kila kitu kwa wakati mmoja. Yaani kwa sababu tu wana malengo basi kila kinachokuja mbele yao wanakimbizana nacho? Jibu ni hapana. Mtu hawezi kuwa anashugulika na kuwa baba au mama bora wa familia, wakati huo huo anashughulika kuwa mchungaji kwenye kanisa lake, wakati huo huo anafanya biashara. Watu hawa wana vipaumbele. Ndio maana wako bize.
Akiwa na familia anakuwa na familia kweli, na anahakikisha anautumia vizuri muda huo. Akiwa na kwenye biashara anatafuta jinsi kuikuza biashara yake kila wakati.  Ndio maana anakuwa bize kwa sababu wewe hakujui na wewe sio kipaumbele kwake basi utamtafuta sana, huku yeye akiendelea kung’aa.

Hata ukipiga simu kwa sababu wewe sio kipaumbele. Basi ataipuuza kwa sababu vipaumbele vinamvuta akavitimize.

Hatua ya tatu  BE BUSY WITH YOUR PRIORITIES. Kuwa bize na vipaumbele vyako.

Soma Zaidi:  Vipaumbele Vyako Ni Vipi?

4. SOMA WANACHOSOMA.
Watu waliofanikiwa sana, sana. Kuna vitabu wanasoma. Hii ni siri nimekuibia, usimwambie mtu. Hahahah! Chagua watu watatu ambao unawaamini sana ambao unapenda mafanikio yao. Basi fuatilia wanasoma vitabu gani. Visome vitabu hivyo haswa. Kitu kingine cha  ziada ambacho wewe unapaswa kufahamu ni kwamba  hata hawa waandishi kuna watu wanawakubali. Wafuatilie na hawa pia.

Kikubwa zaidi kwenye vitabu ni matendo sio maneno. Kwa hiyo kuwa mtu wa matendo zaidi kuliko maneno. Ukisoma kitu basi hakikisha unawahi kukifanyia kazi. Angalia kama kinafanya kazi au la! Kama kinafanya kazi endana nacho, kama hakifanyi kazi achana nacho.

Hatua ya nne, BE BUSY  WITH BOOKS. Kuwa bize na kusoma vitabu.

5. MTU MMOJA UNAYEMKUBALI
Watu waliofanikiwa wapo wengi. Karbia kila sekta ina mtu aliyefanikiwa. Ndio kila sekta. Sasa wewe unamhitaji mtu mmoja ambaye utamfuatilia na kutaka kujua zaidi kutoka kwake kila mara. Jifunze kutoka kwake.

Mjue nje ndani. Zijue biashara zake, na jua jinsi anavyozisimamia. Kama ana huduma ambayo utapaswa kuilipia ilipie ili upate kujifunza zaidi kutoka kwake. Kwa hakika utafurahia sana

Hatua ya BE BUSY WITH ONE DISTINGUISHED PERSON. Kuwa bize na mtu mmoja aliyejitofautisha.

6. TAFUTA NJIA YA KUMSAIDIA
Moja kati ya vitu ambavyo watu huwa wanakosea ni kutaka wasaidiwe wao na kusaidiwa tena na tena.

 My friend, Kanuni hazifanyi kazi kwa namna hiyo hapo.
Wewe unapaswa kutafuta njia ya kumsaidia mtu kiasi kwamba yeye atakuwa tayari kujihusisha na ndoto zako.

Ukikutana na mtu maarufu, au ukimpigia simu usioneshe kwamba unamhitaji sana wazi wazi. Ni kweli unamhitaji ila jua kwamba yuko bize. Yuko bize anataka kuona biashara zake zinafanikiwa zaidi. Kwa hiyo badala ya wewe kuonesha  unamhitaji, jenga uhusiano utakaomfanya yeye akuhitaji wewe hapo. Ni kwa jinsi hii utaweza kuwa umempata mtu huyu huyu mzima mzima.

Ila kikubwa unachopaswa kufahamu ni kwamba wewe unapaswa kuwa bize. Kuwa bize. Kuwa bize kweli maana watu wengine wapo bize.

Asante sana rafiki yangu, na hongera sana kwa kusoma mpaka mwisho makala haya. Endelea kutembelea SONGA MBELE BLOG kila siku ili upate kujifunza kitu kipya. Asante sana, tukutane kwenye meza ya wanamafanikio.

Nakushukuru sana kwa kuweza kusoma andiko hili mpaka mwisho. Umekuwa nami rafiki yako wa ukweli Godius Rweyongeza

Hakikisha Umesubscribe kwenye Channel yangu ya youtube kwa KUBONYEZA HAPA

Jiunge na mfumo wa kupokea makala maalumu kwa njia ya barua pepe kwa KUBONYEZA HAPA

Jipatie nakala za vitabu vyangu vya kiswahili kwa KUBONYEZA HAPA

Kama ungependa kujifunza kuhusu uandishi wa vitabu kutoka kwangu wasiliana nami kwa 0755848391

 Kupata nakala ngumu ya kitabu cha KUTOKA SIFURI MPAKA KILELENI na kitabu cha JINSI YA KUFIKIA NDOTO ZAKO basi tuma ujumbe au piga kwa 0755848391

Kutengenezewa blogu yako kitalaamu tuwasiliane kwa 0755848391

kila la kheri

Kunialika kwa ajili ya kutoa mafunzo au semina kwenye kikundi chako, taasisi, kongamano n.k. wasiliana nami kwa email: songambele.smb@gmail.com au simu 0755848391


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X