Vitu Viwili Vitakavyokupa Nguvu Kwenye Zama Hizi


Hongera sana rafiki yangu kwa zawadi ya siku hii njema ya leo. Leo hii ni siku ya kipekee sana.

Moja kati ya vitu vinavyofurahisha sana, ni pale unapokamilisha kazi ambayo ulikuwa unaifanya kwa siku nyingi sana kiasi kwamba ukawa unajisikia mtupu kwa ndani. Yaani unaona umekamilisha kazi ile na haudaiwi kitu chochote. Umetoa kila kitu kwenye ile kazi na sasa unazidi kusonga mbele. Ukiona umefikia hali hii basi unakuwa umepigana vita vizuri sana kwenye maisha yako. Kama ambavyo Paulo anasema “nimeumaliza mwendo, nimevipiga vita vilivyo vizuri, imani nimeilinda”.

Sio watu wote wanaweza kupigana vita kama hivi hapa. Wengine vita hivi vinawashinda. Lakini kinachowafanya washindwe ni kwa sababu ya kutifahamu mambo haya mawili.

1. HATUA KUBWA ZINAWEZA KUKUUA
Safari ya maili elfu, huanza na hatua moja. Huu ni usemi ambao ulisemwa na Lau Tzu, mwanafalsafa ya kichina miaka kadhaa iliyopita. Lau Tzu alikuwa anatusisitizia juu ya kupangilia mambo yetu na kwenda hatua kwa hatua kila iitwayo leo.

Japo usemi huu ulisemwa miaka mingi sana, lakini usemi huu una ukweli mkubwa sana katika kipindi hiki kuliko wakati mwingine wowote.

Ni ndani ya kipindi hiki watu wanapenda kugusa kitu leo kesho kimekamilika. Ni ndani ya kipindi hiki watu wanapenda kupanda ngazi tatu mpaka nne kwa wakati mmoja. Wanasahau kwamba hatua kubwa bila mwelekeo ni rahisi sana kukuua. Kwa hiyo rafiki yangu usikimbilie kupata mambo makubwa kwa wakati mmoja. Ukiyakosa utalia sana. Kimbilia kutengeneza mambo makubwa kwa hatua, ngazi kwa ngazi na kwa mpanglio. Kwa kufanya hivi utajikuta hata yale ambayo ulikuwa unayaona kama hayawezekani vile yameshawezekana kitambo. Ni kwa jinsi hii utajikuta unakuwa mtupu kila siku. Maana kila siku utafanya kitu cha kukuwezesha wewe kusonga mbele kuelekea ndoto yako kubwa.

Unapaswa Kuwa Na Ndoto Kubwa

2.   JUA AINA VITA UNAVYOPIGANA.
Ili kuondokana na hali ya kupigana kila vita vinavyokuja mbele yako unapaswa kujua ni vita gani unapigana. Jua silaha mahsusi kwa ajili ya vita hivyo. Hali hiyo itakufanya uache kushambulia kila kitu kinachokuja mbele yako.
Hali hii itakufanya uzidi kusonga mbele kwa kujiamini.

Usikubali uingie ulingoni bila kujua aina ya vita unavyopigana. Usikubali uanze siku bila kujua mambo ya msingi unayofanya ndani ya siku yako. Usikubali vitu vipite bila ya wewe kujua ni wapi na kwa kiasi gani unakaribia kwenye lengo lako.

Soma Zaidi: TATIZO SI RASILIMALI ZIKIXOPOTEA 
 tatizo hutaki kuzisema ndoto zako

Hayo ndio mambo mawili unayopaswa kuyazingatia kila kukicha ili uweze kukamilisha kazi kubwa na kukaa ukiwa mtupu

Ndimi,
Godius Rweyongeza
0755848391

KUPATA KITABU CHA KUTOKA SIFURI MPAKA KILELENI BONYEZA HAPA


HUDUMA NYINGINE UNAZOWEZA KUPATA KWANGU HIZI HAPA

KUPATA MAKALA MAALUM KWA WATU MAALUM KILA WIKI BONYEZA HAPA


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X