FaidaOja (01) Ya Kujifunza Ambayo Hujawahi Kuambiwa Popote


Rafiki yangu hongera sana kwa siku hii nyingine tena.
Moja ya mambo ambayo unapaswa kuyafanya ukiwa hapa duniani, basi ni kuhakikisha unajifunza kila siku.

Jambo hili nimeliongelea sana, naliongelea sasa hivi na nitazidi kuliongelea.

Na nimekuwa nakushirikisha faida za kujifunza mara kwa mara ambazo utazipata kutokana na kujifunza kitu kipya.

Leo hii naomba uijue faida hii hapa muhimu.
KUJIFUNZA KUTAPUNGUZIA MUDA MWINGI WA WEWE KUPAMBANA NA MAJANGA.

Soma  Zaidi: JIFUNZE JIFUNZE
Ukijua hili basi hutahangaiaka sana. Maana inagharimu kidogo kujifunza kuliko inavyogharimu kushughulika na kosa linalotokanana uzembe. Kwa hiyo amua kujifunza zaidi, ili upate maarifa zaidi.
Maarifa haya yatakuepusha na makosa yasiyo ya lazima. Na hivyo kukuweka katika nafasi nzuri ya kufanya maamuzi.

Chukulia mfano wa mtu anayejifunza uendeshaji wa gari. Inamchukua dakika chache sana, kujifunza kwamba gari linaendeshewa mkono wa kushoto. Hii ni sheria ndogo sana ambayo bila kuijua ingepelekea mwendeshaji huyu kuendesha kila mahali na kujikuta amesababisha madhara makubwa zaidi ambayo yangemgharimu zaidi kuliko muda huo kidogo uliotumika kujifunza kwamba gari linaendeshewa mkono wa kushoto.

Rafiki yangu, tumia muda wako kujifunza. Dakika chache unazotumia kujifunza leo. Zitakuepusha na makosa makubwa ambayo ungeyafanya na ujinga wako.

Soma Zaidi:  Vitu Utakavyosoma Kutoka Kwenye Kurasa Za Kutoka Sifuri Mpaka Kileleni

Ndimi,
Godius Rweyongeza
0755848391

KUPATA KITABU CHA KUTOKA SIFURI MPAKA KILELENI BONYEZA HAPA


HUDUMA NYINGINE UNAZOWEZA KUPATA KWANGU HIZI HAPA

KUPATA MAKALA MAALUM KWA WATU MAALUM KILA WIKI BONYEZA HAPA

Asante sana,


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X