Naam, leo ni siku nyingine ambapo tunaenda kufanya mambo mengine,
Makubwa kwa makuvwa zaidi pengine,
Ili tuendelee kutengeneza kesho bora nyingine
Itakayopendeza sana zaidi ya leo.
Hongera sana rafiki kwa siku hii bora.
Kuna mtu kila siku utamkuta anasema, kesho nitafanya hiki.
Ukikutana naye baada ya siku na kumuuliza, vipi tayari umeshafanya shughuli yako, utasikia anasema, yaani nilikwama kidogo ila kesho.
Yaani hali ya nitafanya kesho, kesho, kesho haiishi.
Mwisho wa siku, siku zinasogea, muda nao unasogea maana haumsubiri mtu yeyote. Basi kinachotokea mtu anaanza kulalamika. Mtu anaanza kuona kwamba maisha sio rafiki. Lakini yote hayo yameanza na kitu kimoja tu KUSEMA NITAFANYA KESHO.
Kwa hiyo njia rahisi ya kuairisha ulichopanga kufanya ni kusema NITAFANYA KESHO.
Hii ndio njia ya wazembe. Wazembe tu.
Lakini wewe huhitaji kutumia njia ya kizembe sana kama hii hapa. Ukiamua kutumia njia hii basi jua kwamba unakaribisha umasikini. Maana njia hii haikufai wala huihitaji kwa maana haipeleki watu kwenye mafanikio, afya njema, busara na utajiri. Badala yake inafanya kinyume chake.
Unapaswa kuifahamu njia wanayotumia waliofanikiwa na matajiri. Na njia hii sio nyingine bali ni kufanya kitu unachopaswa kufanya sasa. Baasi!
Kwa hiyo kama kuna kuna kitu umepanga, kukifanya basi kifanye sasa. Kifanye sasa hivi bila kuchelewa hata kidogo. Kadri unavyojichelewesha ndivyo unachelewesha kung’aa kwako.
Kazi ya kufanya siku ya leo. Kafanye unachopaswa kufanya siku hii ya leo bila kuhairisha.
Soma Zaidi: TATIZO SI RASILIMALI ZILIZOPOTEA, tatizo hujaondoa vitu ambavyo sio wewe
Ndimi,
Godius Rweyongeza
0755848391
KUPATA KITABU CHA KUTOKA SIFURI MPAKA KILELENI BONYEZA HAPA
HUDUMA NYINGINE UNAZOWEZA KUPATA KWANGU HIZI HAPA
KUPATA MAKALA MAALUM KWA WATU MAALUM KILA WIKI BONYEZA HAPA