Hiki Ndicho Kitu Cha Pili Kinachofuata Kwa Umuhimu Baada Ya Oksijeni


Hivi umewahi kujiuliza ni vitu gani ni muhimu sana hapa duniani? Je, ni vitu gani ambavyo usipokuwa navyo maisha hayaendi kabisa. Je, unavijua?

Kiukweli binafsi najua vitu viwili mpaka sasa hivi. Usipokuwa na hivi hauna maisha. Cha kwanza kabisa ni oksijeni. Oksijeni inapatikana bure kabisa.  Ukikosa Oksijeni kwa zaidi ya dakika tatu, basi unaweza kupoteza maisha. Ila ubora wake ni ya bure na kwa sababu hiyo kuna watu huwa hawaoni umuhimu wake kabisa. Maana wengi sana huwa hawathamini vitu vya bure.

Kitu cha pili kwa umuhimu ni pesa/hela/fedha au vyovyote vile unavyoiita.
Ukiacha Oksijeni kitu kinachofuata ni pesa.

Katika maisha ya Kila siku huwezi kuzungumzia Nguo bila pesa.
Huwezi kuzungumzia chakula bila pesa.
Usafiri haupo bila pesa.

Kwa hiyo pesa ndio inafuata kwa umuhimu baada ya vitu Oksijeni.
Ile ukiamuka tu asubuhi unaanza kutumia pesa. Kwanza kitanda ulichokuwa umelalia ni pesa.
Wakati unaweza kupata usingizi bure kabisa huwezi kupata kitanda, mashuka na godoro bila pesa.
Wakati unaweza kutembea kwa miguu yako bure kabisa, ila huwezi Kutoka nje bila kuvaa (hapa pesa pia inatumika).

Kwa hiyo basi, nikusihi kuanzia leo uanze kuiangalia kwa jicho la kipekee sana. Wakati unaweza kupata Oksijeni bure kabisa, pesa ya bure haipo. Ili upate pesa unapaswa kuwa na thamani sokoni. Kwa hiyo kuanzia leo anza kupeleka thamani sokoni.
Na wewe pia hakikisha unakuwa MTU wa thamani

Je, ni thamani gani unaenda kupeleka leo?
Chukua hatua muda ni sasa rafiki yangu!

Ndimi,
Godius Rweyongeza
0755848391

KUPATA KITABU CHA KUTOKA SIFURI MPAKA KILELENI BONYEZA HAPA


HUDUMA NYINGINE UNAZOWEZA KUPATA KWANGU HIZI HAPA

KUPATA MAKALA MAALUM KWA WATU MAALUM KILA WIKI BONYEZA HAPA


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X