TAFAKARI YA WIKI; ELIMU YA CHUO HAITOSHI, (Kitu Kimoja Unachopaswa Kuambatanisha Na Elimu Yako)


Kwa kawaida mtu unapokuwa umefanya kitu na kukikamilisha mpaka mwisho, basi kifuatacho unakuwa unangojea pongezi, shukrani au vitu vya namna hiyo. Ila sio mara zote, ukikamilisha kitu utapongezwa. Na sio watu wote hukupongeza. Kuna wengine wataona madoa katika jambo jema sana ulilofanya. Na kuna wengine watakupongeza na kukutaka uongezee kitu cha ziada kwenye kile ulichokamilisha.

Kitabu Kinapatikana Na kupo Kwa Ajili Yako. Kwa sh.15,000/-

Mfano ukihitimu darasa la saba wazazi, ndugu, jamaa na marafiki watakupongeza sana, ila bado watakutaka uongezee kitu cha ziada. Yaani watataka uende sekondari ukasome zaidi. Hivyo hivyo ukihitimu kidato cha nne, wazazi watakupongeza ila bado watahitaji uongezee kitu cha ziada.

Sasa msingi kama huo ndio umejengwa kwenye makala hii. Msingi huo ni kupongeza wahitimu Wa chuo, lakini bado kuwataka waongeze kitu cha ziada.

Je, kitu hiki ni kipi?
Bila shaka utajihoji katika namna kama hiyo hapo, ila naomba uwe na subira ili niweze kukudadafulia kitu hiki.

Iko hivi, kwa sasa umehitimu chuo na tayari una kitu cha kukutofautisha. Ukihitimu chuo  moja kwa moja unaanza kufahamika kama mhasibu, mwanasheria, daktari n.k
Lakini Je hii inatosha?
Haitoshi hapa ndipo nataka nikwambie kwamba,  unapaswa kuunganisha taaluma yako na kitu kingine na kutengeneza kitu chotara.
Yaani uunganishe vitu viwili kwa wakati mmoja ili kutengeneza kitu kimoja. Mfano unaweza kuunganisha udaktari na ujasiliamali.
Uhasibu na uandishi
Uhandisi na udereva

Kwa nini kuunganisha?
Iko hivi, wewe umehitimu chuo. Na darasani kwenu mmekuwa ni kikundi kikubwa cha watu. Na nyote mnataka kuajiriwa au kujiajiri kwa cheti na elimu ile ile ambayo mmeipata kwa kufundishwa na walimu wale wale wa darasani.
Sasa, kitu gani kitakutofautisha wewe na watu wengine ambao wameajiriwa kama wewe?
Je, ni kitu gani kitakufanya uonekane wa kipekee kama utaanzisha biashara?
Hapa ndipo unahitaji kujitofautisha kwa kutengeneza kitu chotara (hybrid) kiasi kwamba unakuwa na upekee ambao hakuna mtu yeyote mwenye uwezo wa kufanya kitu kama kile ambacho unafanya.

Acha kujihurumia, anza sasa hivi kutafuta eneo ambapo utajenga upekee wako.

Soma Zaidi; TAFAKARI YA WIKI; Unatumia Mabadiliko Ya Mitandao Ya Kijamii Na Intaneti Au Yanakutumia?

Ndimi,
Godius Rweyongeza
0755848391

KUPATA KITABU CHA KUTOKA SIFURI MPAKA KILELENI BONYEZA HAPA


HUDUMA NYINGINE UNAZOWEZA KUPATA KWANGU HIZI HAPA

KUPATA MAKALA MAALUM KWA WATU MAALUM KILA WIKI BONYEZA HAPA


2 responses to “TAFAKARI YA WIKI; ELIMU YA CHUO HAITOSHI, (Kitu Kimoja Unachopaswa Kuambatanisha Na Elimu Yako)”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X