Yafahamu Mambo Manne (04) Ambayo Huwezi Kujifunza Shuleni.


Habari za leo ndugu msomaji  wa SONGA MBELE BLOG. Ni imani yangu unazidi kupiga hatua katika kutafuta na kufikia mafanikio.

Leo tunaenda kuona mambo ambayo huwezi kujifunza shuleni. Haijalishi umesoma hadi chuo kikuu au hujafika. Kuna utofauti mkubwa kati ya masomo yanayofundishwa shuleni na vyuoni, Na yale unayonifunza kutokana na maisha.

Haya hapa ndo mambo ambayo huwezi kujifunza shuleni.
Kama utayafanyia kazi ukiwa shuleni utakuwa umejiandaa vizuri utakapoenda nje ya shule. Lakini kama upo nje ya shule mda wa kuyafanyia marekebisho ni sasa.

1. Jinsi ya kutunza akaunti yako ya benki
Hili ni jambo la muhimu sana, Lakini cha ajabu shule hazijaweka mkazo kufundisha kuhusu pesa. Hii ni sawa na kushindwa kumwandaa mwanafunzi katika elimu ya hali halisi ya maisha ya ukubwani.

Jifunze: Jinsi ya kupangilia pesa yako yote inayoingia na inayotoka kwenye akaunti yako. Tengeneza bajeti yako halisi ambayo utaitumia.Weka chini asilimia kumi (10%) katika kila mshahara unaoupata au asilimia kumi 10%) ya kila hela inayoingia kwenye akaunti yako (jilipe mwenyewe kwanza) endelea kusoma blogu zinazoelimisha kuhusu pesa kama   SONGAMBELE BLOG.

2. Jinsi ya kutengeneza kazi ambayo ni ya kwako.
Vyuo vingi vilianzishwa kipindi ambacho wahitimu walikuwa wakipata kozi moja nakuifanyia kazi maisha yao yote. Leo mambo yamebadilika ni wahitimu wachache sana wanafanyia kazi  kozi hiyo hiyo moja maisha yao yote. Maisha yamebadilika sana ila vyuo vipo taratibu sana kubadilika. Siku hizi mtu anafanya kazi ya kusoma chuo na kazi nyingine ambayo inaweza kutokana na mambo anayoyapenda.
Mfano

  • Mwalimu wakati huohuo mwandishi wa vitabu
  • Mtangazaji wakati huohuo mwanamziki
  • Nesi wakati huohuo mshauri
  • Daktari wakati huohuo mfanyabiashara.
Tengeneza kazi ambayo unaimiliki mwenyewe kwa kuunganisha vitu mbalimbali ambavyo unavipenda. Haya huwezi kujifunza darasani.
Jifunze: Jinsi ya kukaa chini na kufikria kuhusu maisha yako. Fikiria ni jinsi gani utaishi baada ya masomo. Fikria ni jinsi gani ambavyo utaishi kwa kutengeneza kazi ambayo unaimiliki mwenyewe.

Tumia mambo ambayo umejifunza shuleni au ambayo unayapenda kutengeza kazi au biashara  ambayo unaimiliki mwenyewe.

3. Jinsi ya kupambana unapokutana na vikwazo.
Shule hufundisha mafanikio. Na pale ambapo mtu hushindwa au hukosea basi adhabu kali hufuata.
Lakini katika maisha ya kawaida hakuna ushindi katika kila kitu. Moja ya vitu ambavyo inabidi uvifahamu kwamba vipo ni kushindwa. Watu wengi waliofanikiwa walianguka mara kadhaa ila waliinuka na kuendelea kupambana ili kuelekea kule mtazamo na malengo yao yalipo.

Jifunze: Kusoma historia za watu unaowapenda. Angalia ni jinsi gani waliweza kufanikiwa na walivyopambana na vikwazo.Jifunze kuweka malengo makubwa ya maisha.

4. Jinsi ya kutengeza uhusiano mzuri.
Hiki ni kitu ambacho hutakuja kuona kwenye syllabus za shuleni au vyuoni. Lakini kujua haki ya kuwa na mpenzi, kujifunza jinsi ya kukaa nae na kumpenda kama unavyojipenda mwenyewe, ni vitu ambavyo vitatengeza maisha yenye furaha kwako.

Jifunze: Uhusiano na urafiki unaoutengeneza ukiwa katika miaka ya 20 si wa kupoteza mda. Hata kama uhusiano utakuja kupotea, kila uhusiano unaoutengeneza ukufundishe jinsi utakavyokuja kuwa.
Andika ni mambo gani mazuri unataka kutoka kwa mpenzi unayemtaka na ni mambo gani mazuri utakayotoa. Hakikisha una mda kila wiki wa kukaa na uwapendao. Usiwe mtu wa kukaa peke yako.

Hayo ndo mambo muhimu ambayo huwezi kijifunza shuleni. Anza sasa kuyafanyia kazi na kuyabidilisha maisha yako.

Soma zaidi:

Ni mimi ndugu yako
Godius Rweyongeza
Tuwasiliane
godiusrweyongeza1@gmail.com
0755848391
Asante

Endelea kusoma makala za kuelimisha kutoka kwenye blogu hii


2 responses to “Yafahamu Mambo Manne (04) Ambayo Huwezi Kujifunza Shuleni.”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X