TAFAKARI YA WIKI; Jinsi ya Kuunganisha Elimu Ya Shuleni Na Maisha Ya Kawaida


GODIUS RWEYONGEZA (Songambele)
SUA, chuo kikuu
0755848391

Ni takaribani wiki tatu sasa yangu niandike makala iliyokuwa na kichwa cha *mambo kumi (10) unayopaswa kuyafahamu Kabla ya kufumua nywele Zako Za  graduation*. Kwa hakika, hii ilikuwa makala iliyofumbua macho ya watu wengi sana.

Siku hii ya Leo, tutafakari ni kwa jinsi gani unaweza kuunganisha kile ulichojifunza darasani na maisha ya kawaida.

Kwanza kabisa unapaswa kutambua kwamba kujifunza darasani ni sehemu moja ya shilingi, ila kuweka katika matendo ulichojifunza pia ni sehemu ya pili.

Ukiwa shuleni unajifunza vitu vingi sana. Na pengine asilimia kubwa shuleni ni nadharia, ila mwisho wa siku nadharia inahitajika kuonekana katika uhalisia.

Kuna watu wanakosea kwa kuamini kwamba, kujifunza shuleni ndio mwisho wa kila kitu. Baada ya hapo vitu vingine havitumiki. Najua watu wa namna hii umewahi kuwasikia.

Kwa mfano mtu unasikia anakwambia, Mimi najifunza elimu ya maumbo (geometry) ili inisaidie nini?  Au utasikia mwingine anakuuliza ni wapi kwenye ajira utaenda kutumia kanuni ya Archimedes, (ARCHIMEDES PRINCIPLE).
Haya hapa ni baadhi ya mazungumzo ambayo huwa yanaendelea miongoni mwa wanafunzi na wahitimu.

Na maongezi haya ni ishara tosha kabisa kwamba watu hawajui kwa nini wanasoma. Na kama hawajui kwa nini wanasoma basi hawawezi kutafsiri elimu ya shuleni kwenye uhalisia maana wanaona elimu ya shule kama danganya toto.

👉Kumbe ukweli wa shule ni kukupa mwanga, wa mambo yalivyo wewe ukaendelee kuchimba kwa undani zaidi.

Shule inaonesha njia tu, ila jukumu la kusafiri ni lako. Kwa hiyo baada ya kuhitimu, hakuna mwalimu atakayekufuatilia nyuma ili utafsiri elimu ya  kwenye uhalisia.

Hakuna elimu/maarifa ambayo unajifunza/kupata ambayo hupotea bure alisema Ben Carson kwenye Kitabu chake cha YOU HAVE A BRAIN. Kumbe mambo uliyojifunza shuleni, inawezekana ulikuwa huoni umuhimu wake kwa wakati huo, ila sasa hivi yana umuhimu mkubwa sana.

Ngoja nikupe mfano kidogo wa kitu nilichokuwa nadharau kipindi nasoma shule ya sekondari na wala sikuwahi kufikiri kama kitu hiki kitakuja kuwa na matumizi yoyote maishani. Kitu hiki upimaji kwa kutumia  cc (cm³) Yaani kidato cha tatu kulikuwa na sura iliyokuwa inashughulika na MOLARITY na VOLUMETRIC ANALYSIS. Sasa bwana sura hii nilikuwa naiwezea sana, ila sikuwahi kuona umuhimu wake hata siku moja.
Hapa ulikuwa unakuta wanakwambia vitu kama,
Lita 1= cc1000
Lita❌❓=cc50

Hahahah! najua baadhi hapa wanakumbuka haya mambo ya kitambo kidogo. Sasa hayo mahesabu hapo nilikuwa sioni umuhimu wake hata kidogo. Siku zote nilijua ni upotezaji wa muda tu! Ila kumbe mimi nilipoteza muda sana kwa kusema hayafai kwa watu ambao sio  sahihi. kusema hayafai na wala siyahitaji. .

✔✔mahesabu haya nayatumia wakati wa kabla ya kutumia viwatilifu shambani.
✔✔Wakati mwingine wakati wa matumizi wa mbolea n.k

Yaani leo hii ndio unaona umuhimi wa haya mambo wakati miaka ya 2012, sikuwahi kuona umuhimu wowote. Sasa na wewe unaweza kuwa huoni umuhimu leo hii ila kumbe kile unachodharau, ni muhimu sana.

Mpaka sasa naomba tuzungumzie jinsi ya kubadili Elimu ya shuleni na kuileta kwenye uhalisia.

1. ANZA KUSOMA
Kitu cha kwanza kabisa ulichokutana nacho, wakati wa kufundishwa shuleni kilikuwa ni kusoma. Siku ya kwanza shuleni ulifundishwa a, e, i, o, u. Hii sio kwamba ili kuwa bahati mbaya. Hii nilikuwa inakuandaa wewe kuja kuwa Msomaji wa maisha. Sasa  Leo hii umefika wakati wako kuanza kusoma. Inawezekana shuleni kwako kulikuwa na motto ya elimu ni ufunguo wa maisha. Na wakati motto hiyo inasisitizwa sana shuleni kwako, wewe darasani mwalimu wako yuleee, alikuwa anakufundisha kusoma na kuandika.
Leo hii utapaswa kusoma mikataba,
Utapaswa kusoma kujua ugunduzi unaoendelea sehemu fulani.
Utapaswa kusoma kujifunza mbinu mpya za kufanya kitu
Utapaswa kusoma kujua waliofanikiwa katika kile unachofanya na walikifanyaje.
Utapaswa kusoma ili usipitwe

Yaani kiufupi ni kwamba kama kuhitimu chuo sio kuhitimu maisha Bali nwanzo wa maisha. Kwa hiyo kusoma hakuishii shuleni, Bali kunaanzia shuleni. Hivyo basi utapaswa kuwa mwanafunzi wa maisha bila kuchoka. Kwa mtu anayeishi na kupumua huwa hahitimu kusoma na kujifunza, ndio maana shule ikakwambia elimu haina mwisho.

Soma Zaidi; Uchambuzi Wa Kitabu; Screw It, Let’s Do It

2. JENGA UHUSIANO MZURI NA JAMII
Ukiulizwa kwa nini umesoma utasemaje? Bila shaka jibu ambalo unaweza kutoa haraka ni kuihudumia jamii. Sasa usianze kujitenga tenga na jamii. Kujiona wa viwango eti kisa umehitimu sijui chuo  gani huko. Kuwa mtu wa watu.
Jamii yako ndio INA matatizo ambayo wewe una majibu yake. Kama utajificha hutaweza kuona matatizo ya jamii.  Na usipoyaona hutakuwa na kitu cha kutatua.
Kumbuka shuleni umejifunza ushirikiano kidogo kupitia kazi na kusoma na wenzako, sasa ongeza ushirikiano huu na watu.
Na hapa utapaswa kujifunza kuhusu uongozi hata kama chuo hukusomea uongozi. Jua jinsi ya kuishi na Aina tofauti tofauti za watu. Kumbuka utakutana na watu wabishi, wajuaji, wenye ujuzi wa miaka mingi sana, n.k
Sasa je, upo tayari kuishi na kila aina ya mtu?

3. ONA MATATIZO KAMA FURSA
Najua umekuwa mlalamikajil kwa siku nyingi. Umekuwa unategemea kulishwa na kupewa kila kitu. Pale vitu vilipokuwa vinakosa unalalamika tu. Sasa hivi muda Wa kulalamika hauoo tena. Kama mambo hayaendi sawa Ni wewe umesababisha. Wala sio serikali, au wazazi. Kama vyuma vimekaza, basi wewe ndiwe umehusika kuvikaza.

Kwa hiyo kazi ya kufanya ni kuwa mtatuzi wa matatizo ya watu.

4. FANYIA KAZI KITU KIMOJA ULICHOKUWA UNAPENDA SHULENI
Je, ni kipindi gani ulikuwa unakipenda sana shuleni? Hizi ndicho  unapaswa  kuanza nacho ili kionekane kwenye uhalisia wa maisha. Kifanyie kazi kwa kubadili kile ulichokuwa unapenda katika uhalisia.

Soma Zaidi Tafakari Ya Wiki;  Kipaji Ni Bei Rahisi Sana Kuliko Chumvi

Kwa leo tunaishia hapa. Siku nyingine, tutaendelea. Kuzungumzia Mada hii

Godius Rweyongeza
0755848391

KUPATA KITABU CHA KUTOKA SIFURI MPAKA KILELENI BONYEZA HAPA


HUDUMA NYINGINE UNAZOWEZA KUPATA KWANGU HIZI HAPA

KUPATA MAKALA MAALUM KWA WATU MAALUM KILA WIKI BONYEZA HAPA


One response to “TAFAKARI YA WIKI; Jinsi ya Kuunganisha Elimu Ya Shuleni Na Maisha Ya Kawaida”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X