Vitu Viwili Vitakavyotokea Endapo Utakaa Usipopaswa Kuwa


Hongera sana rafiki yangu kwa zawadi ya siku hii ya leo na ya kipekee sana.

Kitabu hiki kupo kwa ajili yako kwa sh.10,000 tu! Karibu 0755848391

Jana wakati naendelea na shughuli zangu, ilipita helikopita moja iliyokuwa inapiga  kelele sana. Mdogo wangu aliyekuwa mbali kidogo na mimi  aliniita kwa sauti. Nikisikia akisema, “iangalie vizuri hiyo halikopita nakuja kukuuliza swali”.

 Nilitazama angani, kisha kuendelea kazi. Baada ya muda mfupi mdogo wangu alifika nilipokuwa na kuniuliza swali,
“umeona nini”?
Nikwambia “helikopita”.

Akaniuliza tena “kwa nini ilikuwa inapiga kelele sana huku propela yake ikizunguka kwa nguvu”?

Nikamjibu, “haipo mahali inapopaswa Kuwa”.

Akaniuliza tena, “kwani ilipaswa kuwa wapi”?

Nikasema, “ilipaswa kuwa juu zaidi ya hapa, ndio maana kelele nyingi na inatumia nguvu sana kwenda”.

Akaniuliza tena, “sasa hapo wewe umejifunza kitu”?

Nikamjibu “bado sijapata funzo”.

Akarudia tena “umejifunza kitu”?

Nikajibu, “Ndio”.

Akasema “basi inatosha. Nilitaka ujue kitu hicho tu”!

Sasa rafiki yangu, naomba na mimi nikuulize umejifunza kitu? Kama bado hujajifunza kitu naomba twende sawa hapa,

1. Kama haupo unapopaswa kuwa sasa hivi utatumia nguvu kubwa sana kufanya kitu kidogo ambacho hakihitaji nguvu. Hivyo usiridhike na hapo ulipo sasa hivi. Tafuta kupanda juu zaidi ili utumie  nguvu kidogo.

2. Usipopanda juu utakaa chini ukipiga kelele sana. Walio chini na wale ambao hawaweki juhudi ni wapiga kelele maarufu na wakosoaji maarufu. Ila wale walio juu ni watu Wa vitendo. Wanafanya vitu na kuviweka katika uhalisia.

Sasa ni wakati wako kuchagua sehemu sahihi ya kwenda. Chagua kuwa juu sana.

Soma Zaidi; NIMEZALIWA MSHINDI; IJUE KANUNI YA PASI NA HAKIKISHA UNAITUMIA

Ndimi,
Godius Rweyongeza
0755848391

KUPATA KITABU CHA KUTOKA SIFURI MPAKA KILELENI BONYEZA HAPA


HUDUMA NYINGINE UNAZOWEZA KUPATA KWANGU HIZI HAPA

KUPATA MAKALA MAALUM KWA WATU MAALUM KILA WIKI BONYEZA HAPA


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X