Ifanye Dunia Ijue Kwamba Kuna Mtu Huyu Ndani Ya 2019


Ni siku ya pili sasa ndani ya mwaka mpya 2019. Leo hii napenda nikutaarifu kwamba mwaka huu unapaswa kuufanya wa mafanikio makubwa sana.

Na ili mwaka huu ugeuke Wa mafanikio basi wewe jukumu lako ni kufanya dunia ijue kwamba wewe upo unaishi. Ebu sasa hivi andika chini sentensi ifuatayo. Mimi…..(weka jina lako) Ndani ya 2019 nitaifanya dunia ijue kwamba kweli nipo naishi. Nitaishi kwa kuutumia uwezo wangu, nguvu zangu na akili yangu.

Kumbuka kwamba uwezo ulio nao usipoutumia utakuja kufa nao. Ndio maana huwa napenda kuungana na Myles Munroe ambaye anasema kwamba “utajiri mkubwa hapa duniani haupo kwenye machimbo ya dhahabu huko Afrika Kusini, au kwenye migodi ya mafuta huko Nigeria au machimbo ya Tanzanite huko Mererani”

 utajiri mkubwa upo pembeni mwa mtaa wako, yaani makaburini.

Huko ndiko Kuna watu ambao hawakuionesha dunia wao ni akina nani! Kuna watu ambao walikufa na vipaji vyao bila kuvionesha kwa ulimwengu.
Huko makaburini kuna waigizaji ambao hawakuwahi kuigiza.
Makaburini kuna wachezaji ambao hawakuwahi kucheza.

Hawa ni watu ambao hawakuionesha dunia kwamba wao ni akina nani!

Sasa hakikisha mwaka huu unaishi ndoto zako. Ioneshe dunia wewe ni nani ndani ya 2019.
Usikae na Kitabu ndani yako mwaka huu bila kukiandika.
Usitembee na wimbo mwaka huu bila kuuimba,
Uzirurure na michoro bila kuiweka kwenye karatasi.
Usitembee na biashara bila kuiaanzisha. Huu ni mwaka wako wa mafanikio makubwa sana.

Asante sana, rafiki yangu, tukutane kwenye jukwaa la wanamafanikio ndani 2019.
Tukutane kileleni disemba 2019
Wewe ni zaidi ya ulivyo sasa.

Soma Zaidi; Iko Wapi Sehemu Tajiri Duniani Nikatengeneze Pesa?

Ndimi,
Godius Rweyongeza
0755848391

KUPATA KITABU CHA KUTOKA SIFURI MPAKA KILELENI BONYEZA HAPA


HUDUMA NYINGINE UNAZOWEZA KUPATA KWANGU HIZI HAPA

KUPATA MAKALA MAALUM KWA WATU MAALUM KILA WIKI BONYEZA HAPA


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X