Zama Zimebadilika, Unafanya Nini Ili Mabadiliko Haya Yasikuathiri


Hongera sana rafiki yangu kwa nafasi hii ya kipekee sana ya kuishi tena, leo. Imani yangu kwamba umeshukuru kwa kupata nafasi ya kipekee. Lakini pia unaitumia siku hii ya kipekee kufanya makubwa sana.

Leo hii tuzungumzie mabadiliko ya zama. Kama ambavyo nimekuwa nakwambia siku zote, ni kwamba zama za sasa hivi zimebadilika sana.

Moja kati ya eneo ambalo limebadilika sana ni  kwenye matumizi ya madawa. Kwa sasa hivi Kila kitu ambacho watu wanafanya, wanapenda kutumia dawa au kurahisisha kitu hicho au kukifanya kitu hicho kipite bila wao kujua.

Tumefikia hatua ambapo mtu akitaka eti kukaa kwenye ukumbi ili asikilize vizuri basi anapaswa kuwa amekunywa dawa fulani ya kumfanya awe sawa (kahawa).

Kuna mtu hawezi kufanya mazoezi mpaka awe amepata kitu ambacho yeye anasema kinampa nguvu.

Imefikia hatua ambapo watu wanameza vidonge ili wakwepe matatizo au changamoto walizonazo kwa sasa.

Imefikia hatua ambapo hata mahusiano yanatafutiwa dawa za kumeza ili yaweze kudumu.

Sio huko tu, hata kwenye kutafuta pesa. Kuna watu wanatafuta kuwa mamilionea kwa kubeti (dawa) ili wapate utajiri Wa haraka.

Cha kushangaza hata usingizi ambao ni Wa asili kabisa, sasa hivi una madawa yake.  Yaani unameza madawa haya ili usinzie kuepukana na hali fulani ambayo inakukuta. KWA HAKIKA ZAMA ZIMEBADILIKA

Vitu hivi vyote vinafanyika kwa mantiki ya kupata raha ya muda mfupi, ila watu hawaangalii madhara ya muda mrefu.
Mfano unaweza kupata dawa kupata vidonge vya  kusinzia kwa sababu ya kukwepa tatizo fulani, lakini swali je, umetatua tatizo?

Kusinzia hakuondoi tatizo. Bali kunalisogeza mbele.

Rafiki yangu katika zama hizi, utapaswa kuwa makini sana. Epukana na vitu hivi ambavyo kwa hakika vinaonekana vinaleta raha sana. Ila ukivifuatilia, unagundua kwamba vina madhara makubwa sana mbeleni kuliko raha ndogo ambayo unapata kwa sasa hivi.
Amua kuishi bila madawa haya na wewe utafurahia maisha yako.

Asante sana,
Tukutane kwenye jukwaa la wanamafanikio.

Ndimi,
Godius Rweyongeza
0755848391

KUPATA KITABU CHA KUTOKA SIFURI MPAKA KILELENI BONYEZA HAPA


HUDUMA NYINGINE UNAZOWEZA KUPATA KWANGU HIZI HAPA

KUPATA MAKALA MAALUM KWA WATU MAALUM KILA WIKI BONYEZA HAPA


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X