Jicho La Muda-1


Kwa siku unayo masaa 24 sawa na mtu mwingine anayeishi hapa duniani. Hakuna MTU kwenye muda zaidi ya wewe hata kama ni tajiri kuliko wewe au masikini. Muda wote ni masaa 24. Mpaka sasa hivi hakijagunduliwa kifaa chochote chenye uwezo wa kuongeza muda wa mtu au kupunguza muda wa mtu masaa ni yale yale 24 na yamekuwa hivyo kwa siku nyingi saaana!

Jifunze namna ya kuyatumia Masaa haya.

Tajiri mkubwa na masikini, wote wana masaaa 24 ila matumizi ya muda ndio hutofautiana. Matajiri huutumia muda wao kufanya mambo ya maana. Masikini huhangaika kupoteza muda.

Matajiri hupangilia siku zao kuanzia asubuhi mpaka jioni. Masikini huianza siku kama mbuzi na huimaliza bila kujua.

Ikumbukwe kwamba muda ni sarafu. Yaani, kila sekunde unayoipata ni muhimu zaidi kukufanya usogee.

Anza kuiga tabia njema za kitajiri ili na wewe uweze kuutumia muda wako vizuri.

Soma Zaidi: Hili Ndilo Wazo Kubwa Sana Kuwahi Kutokea

Ndimi,
Godius Rweyongeza
0755848391

KUPATA KITABU CHA KUTOKA SIFURI MPAKA KILELENI BONYEZA HAPA


HUDUMA NYINGINE UNAZOWEZA KUPATA KWANGU HIZI HAPA
KUPATA MAKALA MAALUM KWA WATU MAALUM KILA WIKI BONYEZA HAPA


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X