Mtu mmoja aliwahi kusema kwamba tupo katika zama ambazo mtu anaweza kuwa maarufu dunia nzima ndani ya dakika kumi na tano tu!
Ukweli huu sio wa kubeza hata kidogo. Ukiangalia kwenye zama za sasa utaona kwamba,
👉unaweza kutoa video moja ukashangaa Ndani ya muda kidogo imesambaa maeneo mengi sana.
👉Pengine mtu ambaye ulikuwa hutegemei kabisa aone Picha yako akawa wa kwanza kukupigia simu na kukwambia kwamba ameiona na umependeza sana.
👉Sio hili tu, sasa hivi tumefikia hatua ambapo mtu unaweza kuongea na mamilioni ya watu kwa wakati mmoja.
Wakati zama kale zilihitaji watu wasafiri ili kuhudhuria semina au kufanya maongezi na wewe, kwenye zama hizi hapa unakaa chumbami kwako na kuongea na ulimwengu. Semina zinafanyika mitandaoni. Vikao vinafanyika mtandaoni.
Zamani iliaminika kwamba barua ni nusu ya kuonana! Ebu sasa wewe niambie Mara ya mwisho kusikia msemo huu ulikuwa mwaka gani? Kama sikosei Mara ya mwisho kusikia msemo huu ni kipindi kile ulipokuwa unakariri methali na nahau shuleni.😇😇
Kumbe barua sio nusu ya kuonana tena!😀😀😀. Mitandao kama Skype, Instagram, Facebook, wasapu, kutaja ila michache imerahusisha maisha!
Lakini swali ni je, wewe unanufaikaje na mabadiliko haya!
🔥 anza kuitumia Mitandao hii kwa manufaa
🔥acha kufuatilia maisha ya watu wengine
🔥anza kuishi leo.
kwa hakika ZAMA ZIMEBADILIKA
Maisha nayo pia yamebadilika
Sasa ni wakati wako kubadilika.
Imeandikwa na
GODIUS RWEYONGEZA
0755848391
www.songambeleblog.blogspot.com
*RASMI SASA:* kitabu cha ZAMA ZIMEBADILIKA, kitazinduliwa rasmi tarehe 15/4/2019 asubuhi na mapema sana!
Kitabu kitaanza kupatikana kwa soft copy kwanza.
Bei itatolewa baadae