Haya Ni Mambo Ya Kipekee Niliyojifunza Kwa Mzee Wa Zaidi Ya Miaka 55


Wahenga walisema “kuishi kwingi ni kuona mengi”. Nina hakika kwa msingi huu wahenga walitaka tujue kwamba wazee wetu wana mengi sana ambayo tunaweza kujifunza kwao na kuchukua hatua.

Sio hilo tu kuna mtu mwingine aliyewahi kusisitiza kwa kusema kwamba, ukitaka kujua mengi basi waulize wazee wangekuwa wanarudi kwenye ujana wao wangefanya nini kikubwa? Ni kitu gani ambacho wanatamani warudi ujanani kukibadilisha?

Basi nikiongozwa na maswali ya namna hiyo na mengine mengi, juzi nilipata nafasi ya kuongea na mzee mmoja mwenye miaka zaidi ya 55.

Kwanza nilimpongeza kwa kazi njema aliyoifanya ujanani. Maana ameweza kuwekeza kwenye nyumba za kupanga na mabasi kiasi kwamba sasa hivi hana hofu ya leo wala kesho. Alifurahi sana kuona nimethamini juhudi zake na hivyo alikuwa tayari kunishirikisha baadhi ya siri zilizomfanya afanikishe mambo makubwa.

1. Unapokuwa kijana achana na anasa ya aina yoyote ile. Anasa zipo tu, ukipata hela utafurahia sana.

2. Anza mapema ukiwa na nguvu na haswa unapokuwa na miaka 18-35. Unapofikisha miaka 40 na kupanda juu nguvu zinashuka.

3. Usimsikilize mtu na usifuate mkumbo kufanya maamuzi. Mzee anasema tangu yupo kijana mpaka leo hii hajawahi kabisa kusikiliza watu na kuishi maisha ya watu wengine.

4. Soma sana upate maksi nzuri. Ila usikimbilie kuajiriwa. Kuajiriwa ni kurubuniwa kwa hali ya juu sana.

5. Kama hauna mtaji wa kuanzia maisha, basi tafuta ajira ila usikae sana kiasi cha kusema unasubiri mafao. Toka mapema kaanzishe biashara

Soma Zaidi; Hizi Ni Aina Tano Ambazo Unaweza Kufanya Mwaka Huu

6. Kwenye biashara kuna mafao. Tena mafao ya biashara ni makubwa sana kuliko ya kuajiriwa.

7. Kama unataka mafao makubwa kwenye biashara, anza kuyatengeneza ukiwa kijana. Wekeza kwenye rasilimali ambazo zitakulipa siku ukizeeka.

8. Usidharau biashara ndogo ndogo. Zinalipa sana.

9. Kama una ndoto kubwa na hauna mtaji wa kutosha, anza kufanya biashara za kawaida. Tafuta mtaji kisha hamia kwenye biashara kubwa.

10. Unapoajiri kuwa makini. Ajiri taratibu sana ila usifumbie macho uovu. Kuwa tayari kumwondoa mtu ambaye hafanyi vizuri.

11. Hakikisha unapata muda wa kukagua biashara zako. Usijidai uko bize, utapoteza biashara yako.

12. Unapoweka vijana kusimamia kazi usiwaamini kwa asilimia 100.  Hawa hawa ndio unakuta wataka waile biashara yako mpaka iishe. Ukizembea hutapata hata faida.

Soma Zaidi; Huu Ni Ushauri Ambao Andrew Carnegie Anatoa Kwa Kila Mtu

Mwisho mzee huyu aliniambia kwamba kwa sasa vijana tuna fursa nyingi sana zimetuzunguka kuliko miaka ya ujana wake. Hivyo tuwe tayari kuzichangamkia.

Umekuwa nami,
Godius Rweyongeza
0755848391

KUPATA KITABU CHA KUTOKA SIFURI MPAKA KILELENI BONYEZA HAPA


One response to “Haya Ni Mambo Ya Kipekee Niliyojifunza Kwa Mzee Wa Zaidi Ya Miaka 55”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X