Moja kati ya ndoto yangu kubwa hapa maishani basi ni kujenga chuo kikuu kikubwa sana kuwahi kujengwa hapa Afrika. Ndoto hii kubwa nimekuwa nayo kwa muda sasa. Mwanzoni nilikuwa nawashirikisha watu wachache sana ila baadae nimekuwa nikiwashirikisha watu wengi sana. Na kadri ninavyowashirikisha watu wapo wanaosema kwamba haiwezekani niachane na na kitu hicho. Ila Mimi ninachojua ni kitu kimoja tu. Ninakwenda kujenga chuo kikuu kikubwa hapa barani Afrika.
Sasa chuo hiki nitakijengaje?
Kwanza kabisa niseme kwamba kujenga chuo kunahitaji pesa nyingi sana. Na hili ndilo linawafanya watu waseme haiwezekani. Juzi nilikuwa naongea na profesa mmoja wa chuo maarufu hapa nchini akaniuliza utaitoa wapi hela? Utatoa kwa wazazi? Jibu hilo naenda kulijibu hapa.
Kwanza naomba ufahamu kwamba pesa ni zao la thamani. Hivyo nitatoa huduma zinazoongeza thamani kwa jamii kiasi kwamba nipate pesa ya kujenga chuo.
Pili pesa inatokana na kutatua matatizo. Hivyo Mimi nitatatua matatizo mengi yanayowakabili watu ili nipate pesa ya kujenga chuo kikuu kikubwa hapa barani Afrika.
Mwisho jibu nitatekeleza jibu lilitolewa kwenye mtandao was Quora.
Kwenye mtandao wa QUORA, kuna mtu mmoja aliuliza hivi? Ninawezaje kuwa bilionea ndani ya dakika tano.
Kati ya majibu mengi aliyopewa aliambiwa hivi. Waombe watu milioni tano wakuchangie dola 204. Dola 204 ni sawa na shilingi laki tano za kitanzania. Mwandishi wa jibu hili alisema ni rahisi sana kuomba dola 204 kuliko kufanya kitu kingine chochote. Na ili kuomba dola 204 kwa watu milioni tano utapaswa kuwa na huduma ambayo watu wengi watalipia kiasi kidogo na kukufanya kuwa bilionea.
Sasa nitatumia njia hii kupata pesa ya kujenga chuo kikuu kikubwa barani Afrika.
Hivi ndivyo nitajenga chuo kikuu bora na kikubwa sana barani Afrika.
Je, unapenda kushiriki kwenye safari hii. Nitumie ujumbe godiusrweyongeza1@gmail.com
Soma Zaidi; Ifanye Dunia Ijue Kwamba Kuna Mtu Huyu Ndani Ya 2019
Umekuwa nami,
Godius Rweyongeza
0755848391
KUPATA KITABU CHA KUTOKA SIFURI MPAKA KILELENI BONYEZA HAPA
One response to “Hii Ndio Njia Nitakayoitumia Kujenga Chuo Kikuu Kikubwa Barani Afrika (HARVARD OF AFRICA)”
[…] kuhusu tena kuhusu hii mada ya kipekee. Ambayo kila nikishika kalamu kuandika basi najikuta nahamasika zaidi kufanyia kazi ndoto zangu mwenyewe. Halafu eti nikishika kalamu wakati natumia kibodi ya […]