Jinsi Ya Kufanyia Kazi Ndoto Zako Wazazi Wanapokuwa Wanakupinga


Baada ya kusema hayo, nataka kwanza nikupe stori.

Miaka ya 1850 wazazi kwa kuona kuwa kijana wao angefaa kuwa mchungaji/padre walimpeleka kwenda kusoma na kupata mafunzo ya uchungaji. Kijana alisoma kwa bidii, ila ndani yake alikuwa akisikia kwamba kuna kitu anapenda kufanya nje ya uchungaji. Hivyo,  baada ya kumaliza masomo kijana kwa mshangao mkubwa aliwashangaza wazazi wake kwa kusema kwamba alikuwa anaenda kuzunguka dunia huku akitafuta mimea na wanyama mbalimbali. Wazazi wake walitaka kijana awe mchungaji mara moja , ila kijana aliomba kwanza azunguke dunia walau mara moja halafu baada ya hapo atakuja kuendelea na uchungaji.

Wazazi wake walikuwa wanapenda kweli awe mchungaji lakini kumbe yeye moyoni mwake kabisa alikuwa na kitu kingine alichokuwa anapenda kufanya.

Na wewe unaweza kukuta kwamba una ndoto kubwa ya kufanyia kazi kwenye maisha yako, ila sasa wazazi wako, ndio kikwazo kwako. Wenyewe wanataka ufanye kitu fulani ambacho ni kingine kabisa. sasa unafanyaje? Unafanyaje kwenye mazingira kama haya. Na hiki ndicho mwenzetu mmoja alitaka kujua

Unapaswa kuijua ndoto yako na wapi hasa unataka ndoto yako ikupeleke. Uwe na picha kubwa ya miaka kumi na ishirini ijayo. Hii ni picha ambayo hakuna mtu mwingine ambaye anaweza kuiona. Hata ukiwaambia wazazi wako ni wazi kuwa hii picha hawawezi kuiona,  badala yake wataona kwamba umekengeuka.

Wazazi kama walivyo watu wengine kwenye jamii, kuna maisha fulani ambayo wanataka kukuona ukiwa unaishi. Sasa ukienda kinyume na hayo maisha, basi wazazi kama wazazi, watataka wakurudishe ili uweze kwenda mstari. Mstari ambao jamii imechora na kusema kwamba haupaswi kuvukwa na mtu, hata kama watu hawasemi ila mstari huu upo vichwani mwa watu na mtu yeyote yule anayetaka kuuvuka huu mstari, ni sawa na mtu anayeenda na kinyume na taratibu za jamii.

Na unapokuwa na ndoto kubwa sana, maana yake unaenda kinyume na vitu vingi ambavyo jamii inaamini. Kwa mfano, utakuwa unaenda kinyume na umasikini ambao umetawala kwenye jamii na badala yake utataka kutengeneza utajiri mkubwa. Au utakuwa unaenda kinyume na imani fulani ambayo inaaminika kwenye jamii, huku wewe ukiona kwamba unaweza kuigeuza.

Mfano, rafiki yangu Kunyaula, yupo hapahapa Morogoro. Yeye ndoto yake kubwa ni kuona kwamba watu wanaacha kunywa soda na badala yake watu wanakunywa juisi freshi kabisa za matunda aliyotengeneza yeye kwenye kampuni yake ya Kunyaula FOODS….

Hii ni ndoto kubwa na ya kipekee ambayo inaenda kinyume na imani za watu wengi, lakini sasa hiyo ndio ndoto yenyewe. Ukija Morogoro, hakikisha unafika KFFJ na unapata walau hata juisi moja. Juisi zake ni za viwango vya tbs. Sijaona mtu mwingine akitengeneza juisi za viwango kama huyu jamaa hapa Tanzania. Namba yake ni hii hapa +255788080405

Mkurugenzi wa KFFJ akiwa kazini. Juisi zao ni za viwango vikubwa. Wapo Morogoro na delivery wanafanya pia. Watwangie tu kwa +255788080405

ukifika Mororogoro, usiondoke bila kufika KFFJ kwa Kunyaula

Enewei tuendelee..

Siku siyo nyingi nilikuwa nasoma kitabu cha JONATHAN LIVINGSTONE SEAGULL. Hiki kitabu kimeandikwa kwa mfumo wa hadithi ila kina mafunzo makubwa sana kuhusu kufuata ndoto zako najinsi ambavyo unaweza kuzifikia.

Kama sijakosea Seagull ni nyange kwa Kiswahili. Kitu kikubwa ambacho nyange wanafanya ni kutafuta chakula na kurukaruka mwaloni au sehemu yoyote iliyokaribu na maji ili kutafuta chakula. Hakuna zaidi ya hapo.

Lakini sasa nyange  mmoja alikuwa anajulikana kama Jonathan Livingstone alikuwa na ndoto ya kupaa na kufika juu mawinguni kama tai. Hii ndoto hii, nadhani unaweza kuona jinsi ambavyo inaenda kinyume na mazoea au mstari ambao nyange wenyewe wamechora. Ebu ngoja hata nikuulize wewe, umewahi kuona nyange anapaa juu maiwnguni kama tai? Umewahi kuona hicho kitu?

Na ikitokea ukaona kitu kama hicho si utashangaa? Sasa hiyo ndiyo ndoto ambayo Jonathan Livingstone Seagull alikuwa nayo. Alitaka kupaa mpaka juu mawinguni zaidi hata ya tai.

Kilichotokea kilikuwa ni kukataliwa na wazazi wake na hata jamii nzima ya nyange. Kwa hiyo akaishi peke yake na baadaye akakutana na nyange wengine waliokuwa na ndoto kama hiyo, wakaungana na akawa ameweza kutimiza ndoto zake.

Kwa hiyo, unapokuwa ana ndoto kubwa ujiandae kabisa kuwa kila mtu atakuwa na maneno yake juu ya ndoto yako.

Juzijuzi tu nilikuwa naasoma kichekesho mtandaoni kilichosema kwamba. UKIZALIWA AFRIKA ni kama kuna sheria hivi ambayo haijaandikwa sehemu ila ipo vichwani mwa watu kuwa lazima tu utakuwa mkulima.

Hivi bado najibu swali au nimeenda nje ya mada…Basi naomba nihitimishe pointi yangu ya kwanza kwa kusema kwamba, unapokuwa na ndoto kubwa, hakikisha kwamba unaijua kwa undani kabisa na wapi unataka ikupeleke.

Sitaandika sana kuhusu hili, maana kuna makala za kukusidia kwenye hili. Kwa kuwa leo nataka nijikite zaidi kuhusu namna unavyoweza kushughulika na wazazi ambao hawasapoti ndoto zako, ila hapa nataka tu nikudokeze kuwa unapaswa kuanza kuifanyia kazi ndoto yako. Anza kuifanyia kazi hata kwa udogo, usisubri mpaka uwe na kila kitu. Hatua ndogo ndogo zitakufikisha kwenye ndoto yako rafiki yangu. Hii ni toafauti na na mtu ambaye anakaa bila kufanya kitu chochote kile. kwanza angalia picha hii hapa chini.

Umeiona picha hiyo. Haya ni mashindao ya wanyama na wanyama wengine tayari wameshaanza kukimbia ila kamnyama kamoja bado kamelala humo ndani. Kanajua kukimbia kweli kuliko hao wengine wote, ila sasa asipotoka na kukimbia, hatashinda.

hiki kitu ndio nataka nisisitize na kwako. unaweza kuwa una ndoto kubwa. au una kipaji na unataka ukifikishe mbali. nisikilize, kama hutaanza kukifanyia kazi hutakaa ukifanikishe. Kwa, hiyo, anza kuifanyia kazi ndoto yako kuanzia sasa hivi.

Kama nilivyosema kwamba unapokuwa na ndoto kubwa, hakuna mtu ambaye anaweza kuiona picha kubwa unayokuwa nayo. Siyo hata mwenza wako. Kwa hiyo, linapokuja suala zima la wazazi, kaa chini ongea nao. Waambie kwamba mimi ndoto yangu ni hii na ninaenda kuwa naifanyia kazi, hii ndoto itakuwa na manufaa yafuatayo kwwangu, kwenu na kwa taifa…

Hivyo naomba mnichae kwanza niifanyie kazi ndoto yangu.

Kama bado wazazi hawakuelewi, basi omba wakupe muda wa kuifanyia kazi ndoto yako. Waambie kwamba ninaenda kuifanyia kazi ndoto yangu kwa  mwaka mmoja au mwili kwanza, kama nitakuwa bado sijapata kitu chochote wala kufikia sehemu yoyote ile nitaachana na ndoto yangu na kuendelea nakile mnachotaka.

Kuna watu wametumia hii mbinu na imewasaidia.

Ndani ya hiyo miaka uliyowaambia hakikisha kwamba unafanya kitu chako kwa ubora kiasi wkamba mpaka miaka hiyo hii inafika mwishoni, wewe tayari  umepiga hatua fulani, lakinip ia wazazi wako tayari wamekuwa mashabiki wa kile unachofanya.

Ngoja nikwambie ukweli usiopenda kUusikia. Ukweli ni kwamba wazazi wako wanakuzuia wewe kufanyia kazi ndoto zako kwa sababu tu unaenda kuwa mzigo kwao. Wanataka ufanye kitu fulani walau uweze kuingiza kipato uache kuwasumbua. Lakini pia na wao wanataka wapate kitu chochote kutoka kwako. hahah

Sasa ukilijua hili halitakusumbua. Badala yake utapaswa kuhakikisha kwamba  hatua ya kwanza unaanza kujitegemea. Usiseme kwamba unafanyia kazi ndoto yako, unatoka nyumbani na baadaye jioni unarudi unategemea chakula cha wazazi.

Anza kubeba jukumu la maisha yako kwa asilimia 100. Waambie wazazi wako kuwa hata kama sijaajiriwa ila mimi sitawategemea ninyi kwa kitu chochote. Sitategemea chakula wala malazi kutoka kwenu. Nitapambambmana na hali yangu. walau anzia hapo.

Ukiweza hata kuanza kujihudumia wewe, utafikia hatua ambapo na wenyewe utakuwa unawarushia kiasi fulani cha kutumia. Kitu ambacho wanataka.

Wao wanahofia kwamba ukifanyia kazi ndoto zako, hutapata hela… utaendelea kuwa mzigo kwao. Wewe bado tu hufunguki mshikaji wangu… Au basiiiiiiii.

Kuna usemi kuwa nabii hakubaliki nyumbani. Kwenye biblia Yesu hakukubalika nyumbani kwao na hata walimuua. Ila ukristo ulikuja kukubalika maeneo mengine kuliko hata unavyokubalika nyumbani kwao. Leo hii ni asilimia mbili tu ya wayahudi ambao ni wakristo. Wengine wote wanaendelea na maisha yao kama kawaida.

Kama umetumia mbinu hizo hapo juu na hazijakubalika, basi utapaswa kutoka nyumbani na kwenda kupambana maeneo ya tofauti kidogo nje ya nyumbani. huku kutakuwezesha wewe kukaa mbali na watu ambao wanakukatisha tamaa au kukurudisha nyuma au kukudhoofisha kwa namna yoyote ile. Lakini pia kwa kuwa utaenda kwenye mazingira mapya ambayo hakuna mtu anayekujua, utakuwa na uhuru wa kufanya kitu hchochote kile bila ya kuogopa, badala yake utakuwa tayari kuipambania ndoto yako.

Kwa leo nataka niishie hapa. Kama kuna hoja zaidi basi tuendeleze mjadala kwenye eneo la maoni. Mimi mwenyewe nitakuwepo kujibu hoja yoyote zaidi itakayojitokeza.

Mpaka wakati mwingine, mimi ni Godius Rweyongeza kutoka songembele.

Kupata makala zaidi kutoka kwangu, hakikisha kwamba umejiunga na mfumo wetu wa kupokea makala maalumu kwa kujaza taarifa zako hapa chini.

Mmhh yaani na wewe? Hata kusema tu ngoja nifoward haka ka makala kwenye grupu moja la WhatsApp 😂😂. Au basi!


4 responses to “Jinsi Ya Kufanyia Kazi Ndoto Zako Wazazi Wanapokuwa Wanakupinga”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X