Hii Ni Kwa Wale Tu Wanaohitaji Mafanikio Kama Vile Wanavyohitaji Kupumua


Siku moja kijana mdogo alimwendea Socrates ili amuulize siri ya mafanikio. Alichofanya  Socrates alimwambia njoo kesho muda fulani, tutakutana  kwenye mto. Kesho yake kijana alijiandaa na kufika eneo husika.

Socrates alianza kuingia kwe maji huku akimwambia kijana nifuate. Kijana alishangaa huyu ananipeleka wapi? Waliingia kwenye maji na kina cha maji kilianza kuongezeka. Ghafla Socrates alimshika kijana kwa nguvu na kumdumbuiza kwenye maji. Kijana alitapatapa lakini Socrates aliendelea kumshikilia kwa nguvu. Katika hatari ya kufa Socrates alimwachia kijana. Kijana alitoka chini ya maji na kuvuta pumzi kwa nguvu sana.

Socrates alimwuliza “ni kitu gani ulikuwa unakipenda kukipata ulipokuwa chini ya maji”? Kijana alisema “kupumua”
Socrates akamwambia “ukipenda mafanikio kama ambavyo unapenda kupumua, basi utafika mbali sana”.

Sasa makala hii nimeiandaa maalum kwa ajili ya mtu ambaye anapenda mafanikio kama ambavyo anapenda kupumua.

1. Unaweza kuwa unavyotaka kama utaamua. Unaweza kuwa mkurugenzi, waziri, kiongozi wa kampuni, mbunifu, mwimbaji au mchezaji.
Unachopaswa kufanya ni kuandika wajibu wako kwenye tamthilia hii ya maisha. Je, kwenye tamthilia hii wajibu wako ni upi?
Malengo yako ni yapi?
Ndoto zako ziko wapi?
Je, unapenda kukamilisha nini mwaka mmoja kutoka Sasa? Vipi kuhusu miaka kumi ijayo?

2. Mahusiano yako yatakujenga au yatakubomoa. Hamna mahusiano ambayo hayana madhara kwako. Kwa hiyo hakikisha unakuwa makini linapokuja suala zima LA kuchagua marafiki. Kama umezungukwa na marafiki wa kawaida basi amua kuwekeza muda wako mwingi kwenye usomaji wa vitabu. Kumbuka watu waliokuzunguka wanakuhamasisha kusongambele au wanakukatisha tamaa, hakuna anayefanikiwa peke yake.

3. Tabia ni kama alama za vidole, inakuyofautisha wewe na mtu mwingine yeyote.

4. Unapaswa kuwa makini haswa pale fursa zinapojitokeza kwako. Dunia ni sehemu nzuri sana, inakutumia fursa za kila aina kila siku.

 5. Ukiendelea kufanya ambacho umekuwa unafanya basi utapata kile ambacho umekuwa unapata siku zote.

6. Hakutakuwepo na muda sahihi wa sisi kufanya makubwa. Kuna wakati tutapaswa kuachana na vile ambavyo tumezoea na kujitoa kufanya makubwa. Kama nike tunapaswa kusema  EBU KIFANYE TU (JUST DO IT).

7. Unapofanya maamuzi ya kubadilika, dunia itafanya kila kitu iwezacho kuhakikisha inakufanikishia ndoto yako.

8. Unapoamua kufanya maamuzi ya kutimiza kitu fulani hakikisha unaamua haswa. Kutakuwepo na vipingamizi vya hapa na pale ila simama wima na simamia kile ulichoamua.

Haya ndio mambo muhimu kwako ambaye unahitaji mafanikio kama ambavyo unapenda kupumua. Yaweke katika matendo uliyosoma hapa.


One response to “Hii Ni Kwa Wale Tu Wanaohitaji Mafanikio Kama Vile Wanavyohitaji Kupumua”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X