Enheee! Leo bwana, nataka nikuchokonoe kidogo. halafu baada ya kuwa nimekuchokonoa nitakwambia ni kitu unapaswa kufanya ili uweze kufika kule unapotaka kufika. Au basi!
Ninajua, kwamba wewe una ndoto kubwa, una ndoto za kufika mbali na ndoto za kufanya makubwa kwenye maisha yako. Si ndio. Na kwa siku nyingi sana umekuwa unapambana ili kuweza kufikia hizo ndoto na malengo yako au siyo! Mpaka watu wamekuita mpambanaji, fighter, jembe na majina mengine ya aina hiyo. Sasa bwana leo hii, kuna kitu nataka niseme kwako.
Nakumbuka siku za nyuma niliwahi kuandika makala hapa nikawa nimsema kwamba kama unataka kufanikiwa na kufika mbali unatakwiwa kuwa na kiu ya mafanikio kama vile ambavyo unahitaji kupumua. Na hiki kitu kilikuwa kinaanza na stori moja hivi ya Socrates. Naomba kwa haraka niweze kuirudia hii stori ili tuweze kwenda sawa siku ya leo.
Stori yenyewe iko hivi,
Kuna kijana mmoja alimfuata mzee baba Socrates ili amfundishe mbinu za mafanikio. Socrates akamwambia rudi nyumbani, halafu utakuja kwangu siku fulani. Siku hiyo waliyokubalina kukutana kijana alionekana kwa wakati, akonesha kwamba kweli yupo tayari kujifunza mbinu za mafaniko ili aweze kufanikiwa. Socrates akawa amemwambia yule kijana kwamba “nifuate”.
Socratesa akaongoza msafara mpaka walipofika sehemu fulani hivi yenye maji. Kufika pale Socrates akaanza kuzama ndani ya mji, wakati huohuo akawa amemwambia kijana amfuate. Kijana vile alikuwa anataka mafanikio akawa anazidi kumfuata tu Socrates. Walipofika katikati ya maji, ghafla Socrates alimshika kijana kwa nguvu na kumzamisha kwenye maji. Kijana akawa anajitahidi atoke ila wapi, akajitahidi kwa nguvu zote, ila hakuna chochote klichotokea.
Kijana kuona kama hakuna matumaini ya kuachiwa, basi akawa amejikusanya na vinguvu vyote alivyokuwa navyo akalazimisha kutoka majini, na akawa amefanikiwa kweli.
Sasa baada ya hicho kitu, Socrates alimwuliza kijana, ni kitu gani ulikuwa unataka sana sana ulipokuwa majini. Yule kijana alijibu kwamba nilipokuwa majini, nilikuwa nataka sana sana kupumua.
Basi, Socrates akamwambia kwamba kama unataka kufanikiwa basi unapaswa kuwa tayari kutafuta mafanikio kama ambavyo ulikuwa unahitaji pumzi ulivyokuwa majini. Hiyo ndio siri ya mafanikio.
- SOMA ZAIDI: AMSHA UUNGU ULIO NDANI YAKO: Sifa 3 Za Kimungu Unazopaswa Kuzitumia Kuanzia Leo
- Una Uwezo Mkubwa Ndani Yako
- Una Uwezo Mkubwa Ndani Yako
Umeona ee! Siri kubwa ya mafanikio ni kwamba unapaswa kutafuta mafanikio kama vile unavyohitaji kupumua. Nimekuwa nikiwaambia watu wengi sana kuhusu hiki kitu na nikweli watu wengi, wamekuwa wakitafuta mafanikio kama vile wanavyotaka kupumua. Lakini sasa nimekuja kugundua kitu hiki pia kinawakwamisha watu. Ili uweze kunielewa vizuri kwanza angalia mchoro huu niliochora kwenye diary yangu.
Kama unasema kwamba Songambele anachora vizuri na anastahili kupata maksi mia kwa mia nyoosha mkono basi.
Hahah, sasa mchoro huo hapo juu maana yake nini?
Kwa leo ninaenda kuyagawa mafanikio kwenye ngazi kubwa tatu.
- Ngazi ya kwanza ni kushindwa,
- ngazi ya pili ni kupumua/kuishi au kula chakula na
- ngazi ya tatu ni mafafanikio yenyewe sasa.
- SOMA ZAIDI: Mafanikio ni nini?
- Mafanikio ni nini?
Sasa kitu ambacho kimekuwa kinatokea kwa watu wengi na kwako ni kuishia kwenye ngazi ya pili ya mafanikio bila kupanda ngazi ya tatu. Na hiki kitu ndio kimekuwa kinafanya watu wanakusifia kwamba wewe ni mpambanaji mkubwa ila wewe ukiwa haufikii mafanikio hayo unayoyataka.
Kwa kutumia mfano wetu wa Socrates hapo juu. Unakuta kwamba mtu yupo kwenye hali mbaya ya kimaisha. Yaani, ni kama anazama kwenye maji (ambayo kwenye mchoro wetu hapo juu ndio kushindwa). Kitu hiki kinamstua, anaona ee, kumbe mambo ni magumu, sasa nafanyaje ili nisizame kwenye haya maji ili nisije nikakosa kupumua. Kama hana hela anaanza kupambana kwa nguvu zake zote kuhakikisha kwamba anapata fedha ya chakula. Akishaipatahiyo fedha anarelax, anasahau kuwa kuna wakati alikuwa anataka kuzama. Anaanza tena kuishi maisha ya kawaida, baada ya siku au muda fulani, anaanza kuzama tena. Anastuka tena kumbe nazama ee! Anapambana kwa nguvu zake kuhakikisha kwamba hazami, kwa hiyo muda wote anakuwa anachezea kwenye ngazi hizo mbili za chini. yaani, anachezea kwenye ngazi ya kushindwa au kuzama kwenye maji na ngazi kupumua. Mtu muda wote anakuwa anapambania pumzi yake tu ili asife. Au anapambania chakula.
Yaani, ni kama mtu yuko baharini, ila muda wote ametoa kichwa chake juu tu ili asizame. maji yakiongezeka anapambana kwa nguvu zake zote ili asizame, na akishatoa kichwa juu tu, kazi imekishwa.
Mtu wa aina hii ni mpambanaji kweli, ila sasa hapambanaji kiasi cha kutaka kuyafikia mafanikio makubwa. badala yake anaishia kwenye ngazi ya kuvuta pumzi ili asife au ngazi ya kula chakula ili asife. Ila maisha ni zaidi ya hapo.
Ndio maana, huku mtaani unaweza kukuta kwamba kuna watu ambao hata hawana sehemu ya kulala. Ila chakula wanakula. Hakuna hata siku moja mtu analala njaa. Kwa hiyo yeye mapambano yake yote, ni kuhakikisha kwamba anapata chakula. Kulala? Atalala hata stendi, sokoni au sehemu yoyote atakayoona. Hawa watu ndio wanachezea kwenye hizi ngazi mbili. ngazi ya kushindwa na ngazi ya kupumua au ngazi ya kula chakula.
Wewe pia unachezea kwenye hii ngazi kwa sababu, kila siku unaendelea kutafuta fedha ya chakula, fedha ya kulipa bili na kodi. Ukishaipata unarelax baadaye unakuja kustuka imeisha unaanza kupambana tena. Ukiendelea kuchezea kwenye huu mtego wa panya, kuna siku utazama moja kwa moja. na ndio maana leo nikaanza kwa kusema kwamba ninataka nikuchokoze, lakini sitaishia tu kukuchokoza, mwisho wa siku nitakupa mwongozo.
Sasa ni kitu gani kinahitajika ili kukutoa kwenye hii ngazi na kukupeleka kwenye ngazi za juu zaidi. kinachohitajika hapa siyo kitu kikubwa sana.
Ni vitu vya kawaida tu. Yaani, kiufupi ni kwamba vitu vinavyokutoa kwenye kushindwa, na kukuleta kwenye ngazi ya kupumua, vitu hivyohivyo, ukivitumia vizuri, lazima tu vitakufikisha kwenye ngazi ya kufanikiwa. Tatizo la watu wengi kuna wakati huwa wanarelax. Yaani, mtu anafanyia kazi mambo fulani halafu baadaye anarelax. Na hiki kitu nimekuwa nakiona kwa watu ambao wanafuatilia kazi zangu pia. Mtu anasoma makala humu, anajifunza na kufanyia kazi vile alivyojifunza. Baada ya muda anaanza kuona matokeo.
Sasa badala ya kuendelea zaidi na zaidi, anarelax, kitu kinachompelekea kwenye anguko lake jingine na hivyo kila mara anajikuta kwenye kwenye huu mtego wa panya.
Kiufupi, siri za kufanikiwa tayari wewe unazijua. Kama umewahi kushindwa, ukainuka mpaka ukafikia hatua fulani, ya kuwa comfortable ujue wazi kuwa kanuni unazijua. Kinachokosekana kwako ni mtu au timu ya kuendelea kukushikilia tu ili sasa uweze kutoka hilo eneo ambpo uko comfortable nakufikia mafanikio.
Na hapo ndipo kundi letu maalumu la THINK BIG FOR AFRIKA linaingia ndani. Nashauri usome maelekezo yakujiunga na jumuiya hii ya kipekee na ujiunge leo hii. Utaratibu wa kujiunga na kundi hili huu hapa.
9 responses to “Unajua kwa nini mpaka sasa hivi hufanikiwi?”
Nimeipenda Sanaaaa hii
tuko pamoja sana.
Good work hii inaweza kubadilisha watu wa kileo Kama kweli watayazingatia yanayozidi kuandikwa humu ,Mungu abariki blog hii!
WAPASHE HABARI VIJANA WAFIKE HAPA KUJIFUNZA HIVI VITU.
ni kweli, something like mtu akiwa kwenye comfort zone anajisahau…….
Hakika mafanikio ni mapambano
Ni kwel I kabisaaaa Kwani katika maisha ni vigumu sana Kwa watu na ata mm pengine kuamini katika kujitoa wengi tunapenda mtelemko na weng tunapenda maisha bora pasip kupambana na hata tunapopambana hatutaki kupata vikwazo Kwani changamoto ndyo Siri ya mafanikio makubwa na nidhamu ya pesa uletwa na kujituma
Very true 😢
Daaaaah kaka wew ni genius kwakweli asant kwa kunifumbua