Kama wewe ni mpenzi wa hadithi na tamthilia basi utakuwa unafahamu kwamba kwenye hadithi hizi huwa kuna mtu mmoja ambaye ndiye mhusika mkuu kwenye hadithi/tamthilia husika.
Mtu huyu huwa anapata misukosuko. Pengine huwa anapigwa kiasi cha kufa. Unakuta pengine anatekwa ila mtu huyu huwa anaendelea kupambana. Huwa hachoki wala huwa haachi kusimamia vitu fulani.
Mbali na misukosuko yote ambayo humkuta bado unakuta mtu huyu anafika mwisho wa hadithi na kuwa mshindi.
SOMO; Wewe pia utakutana na misuko suko. Utasukumwa, utaanguka. Ila ukianguka usibweteke. Anguka ila bado weka juhudi ili kuhakikisha unasongambele.
Kuna mtu mmoja amewahi kusema kwamba, ukianguka chini okota kitu cha kuondoka nacho. Sasa na wewe ukianguka basi usitoke bure. Jifunze kitu, kifanyie kazi, songambele.
Usione wale watu kwenye tamthilia ukadhani ni maigizo tu. Kuna kitu unapaswa kujifunza kutoka kwao.
Soma zaidi: Ukiweza Kumpa Mtu Kitu Hiki, basi Utapata Chochote Unachotaka Kutoka Kwake
Umekuwa nami,
Godius Rweyongeza
0755848391