Mfanyie Kitu Hiki Mtu Huyu Hata Kama Humpendi


Kutokana na ukweli kwamba ajira zimekuwa hazipatikani kwa urahisi, basi watu wamekuwa wanajitoa ili kuingia kwenye ujasiliamali na kuanzisha biashara. Jambo hili ni jema sana, hata hivyo kuna watu wanaingia kwenye biashara bila wao kujua nini haswa kimewapeleka kwenye biashara hizo. Hivyo watu hujikuta wakiwahudumia wateja kwa mazoea sana, lakini pia hujikuta wakianzisha biashara ambazo hazikidhi mahitaji ya wateja wao.

Kuna kitu ambacho unapaswa kukijua na unapaswa kumfanyia mteja wako. Kitu hiki ni kumpa mteja kile ambacho anakihitaji.

Zig Ziglar amewahi kusema kwamba, “unaweza kupata chochote unachotaka, kama utakuwa tayari kuwapa watu kile wanachohitaji”.

Kwa hiyo siku zote jiulize, watu wanataka nini?
Ukishajua watu wanataka nini basi jitolee kukifanyia kazi kwa bidii. Mpe huduma mteja wako kwa viwango vya juu sana.

Unajua nini?
 utapata unachotaka kama utakuwa tayari kuwasaidia watu kupata kile wanachotaka.

Kazi ya kufanya leo. Jiulize wary wqnataka nini? Ukishakijua, weka mkakati wa kuwasaidia.
Naomba nikukumbushe kwamba, utapata chochote unachotaka, kama utakuwa tayari kuwapa kile wanachohitaji

Soma Zaidi; Kuna Kitu Nataka Kuandika Hapa! Kuna Kitu Nataka Kuandika

Umekuwa nami,
Godius Rweyongeza
0755848391

KUPATA KITABU CHA KUTOKA SIFURI MPAKA KILELENI BONYEZA HAPA


Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X