Hili ni swali ambalo nimekutana nalo kwenye mtandao wa QUORA.
Nilifungua kuona muuliza swali kapewa jibu gani.
Yametolewa majibu mengi sana
Moja akaambiwa abadili dola laki moja kwenda kwenye kwacha. Atakuwa bilionea ndani ya dakika tano.
Ila jibu lililonivutia zaidi ni hili.
WAOMBE WATU MILIONI TANO WAKUPE DOLA 204.
Mtoa jibu kasema hii ndio njia rahisi sana ya kuwa bilionea ndani ya dakika tano.
Sasa unaombaje dola 204 kwa watu milioni tano?
Jibu ni kutoa huduma ambayo watu wengi watakuwa tayari kukulipa hata kama ni kiasi kidogo.
Lakini hii sio tu kwamba hapa utapaswa kulala tu. Utapaswa kuweka juhudi, kufanya kazi kwa bidii na kutatua matatizo ya watu wengi zaidi.
Soma Zaodi; Vitu Vitano Vyenya Thamani Zaidi Hapa Duniani
Umekuwa nami,
Godius Rweyongeza
0755848391
KUPATA KITABU CHA KUTOKA SIFURI MPAKA KILELENI BONYEZA HAPA
One response to “Ninawezaje Kuwa Bilionea Ndani Ya Dakika Tano?”
[…] Kwa hiyo wewe, unaweza kuangalia namba ipi unaweza kupambania. Lakini pia soma hapa kuna mbinu zaidi […]