Bilionea Ni Mtu Wa Aina Gani?


Bilionea ni mtu anayemiliki rasilimali zenye thamani ya bilioni moja. Bilioni ina milioni elfu moja NDANI yake. Ubilionea hupimwa kwa thamani ya fedha ya nchi husika.

Kutokana na thamani za fedha kutofautiana, kwa sasa kipimo kinachotumika kupima ubilionea ni dola ya Marekani.

Kwa hiyo ukisikia wanasema fulani ni bilionea, ujue ni kwa thamani ya dola za Marekani.  Hii ndio kusema kwamba unaweza unaweza kuwa na rasilimali zenye thamani ya bilioni moja kwa fedha za Tanzania ila usiwe bilionea kwa sababu kipimo kikuu kinachotumika kwa sasa kupima ubilionea ni dola za Marekani.

Bilioni moja ya shilingi za Tanzania kwa sasa ikiwekwa kwenye dola za Marekani ni sawa na dola laki nne na elfu thelathini. Kwa hiyo, ukiwa na bilioni moja ya kitanzania wewe siyo hata milionea!

Bilioni moja ya kitanzania ikiwekwa kwenye dola za Marekani

Ili uwe milionea kwa thamani ya dola unapaswa kuwa na rasilimali zenye thamani ya shilingi za Tanzania bilioni 2.3 

Jinsi ubilionea unavyopimwa

Ubilionea (UTAJIRI)= THAMANI YA RASILIMALI-MADENI YOTE.

Wewe mwenyewe pia unaweza kupima thamani ya utajiri wako kwa kuchukua thamani ya rasilimali zakokisha ukatoa madeni yote unayodaiwa.

Chukua thamani ya mali zako kwa sasa kama ungekuwa unaziuza kisha toa madeni.

Je, bilionea ana fedha zote mfukoni?

Kwa sasa hivi ubilionea unapimwa kwa kiwango cha thamani ya rasilimali ulizonazo baada ya kutoa madeni. Mabilionea wengi wamewekeza kwenye makampuni au rasilimali zisizohamishika (kama nyumba, ardhi,) au wamewekeza kwenye soko la hisa (hisa, hatifungani na vipande), hivyo bilionea hana fedha taslimu mfukoni mwake. Utakuta ana fedha za kawaida tu za kumtosha kufanya mambo yake yote muhimu ila hana bilioni zote za fedha taslimu mfukoni.

Ila mali zake zote zikiuzwa kwa thamani ya wakati husika zina uwezo wa kufikia bilioni husika.

HAKIKISHA UMESOMA KITABU CHANGU CHA MAAJABU YA KUWEKEZA KWENYE HISA HATIFUNGANI NA VIPANDE ili ujifunze zaidi kuhusu UWEKEZAJI. Kupata kitabu hiki rusha elfu tano kwa namba 0755848391 jina ni Godius Rweyongeza. Utatumiwa ebook yako bila kuchelewa.

Nawezaje kuwa bilionea?

Watu wanakuwa mabilionea kwa kurithi
Au kwa kupambana wenyewe.

Kama huna sehemu ambapo utarithi ubilionea basi utapaswa kupambana mwenyewe.

Ili kuwa bilionea utahitaji kuweka kazi sana na kwa muda mrefu. Utahitaji kujipa muda, maana ubilionea hauwezi kutokea ndani ya siku moja. Unahitaji muda, kazi, KUWEKEZA, kuanguka na kusimama tena.

SOMA ZAIDI: KUTOKA SIFURI MPAKA UBILIONEA (Mbinu Kumi Zitakazokuinua Mpaka Ubilionea)

Je, ni kazi gani inaweza kunipa ubilionea?

Niwe tu mkweli, hakuna kazi inayokulipa mshahara inavyoweza kukupa ubilionea.
Ili ufikie ubilionea utapaswa kuwa na biashara na (au) kufanya Uwekezaji.

Ukiangalia orodha ya sasa ya mabilionea, wengi wanatoka kwenye sekta mbalimbali Ila Kuna sekta 11 zinajitokeza  kwa mabilionea wengi. Nashauri upate ebook yangu ya SEKTA 11 ZA KUTENGENEZA MAMILIONI YA FEDHA TANZANIA ili ujue maeneo sahihi unapoweza kuwekeza fedha zako. Haya ni maeneo mazuri pia inavyoweza kuanzisha biashara ya kukupelekea kwenye ubilionea.
Ebook hii inapatika kwa elfu tano (5,000/-) tu. Rusha elfu tano (5,000/-) kwa 0755848391 jina ni GODIUS RWEYONGEZA ili nikutumie ebook hii.

Ubilionea wa MO DEWJI

Kwa Tanzania tunaye bilionea mmoja ambaye ni MO DEWJI. Huyu ndiye ana utajiri unaofikia bilioni moja na nusu (1.5) kwa dola za kimarekani. Fedha zake zikiwekwa kwenye shilingi za Tanzania anakuwa na zaidi ya trilioni 2.

Hii ndio kusema  kama una mpango wa kufikia ubilionea, unapaswa kujipanga walau ufikishe uwekezaji wenye thamani ya shilingi trilioni 2.

Upo hapo?

Kwa hiyo kuwa bilionea ndio haiwezekani kabisa?
Hapana. Siyo kwamba haiwezekani, ngoja nikupe mbinu ya kutengeneza kufikia ubilionea.

Ukitengeneza bidhaa inayouzwa kwa dola moja moja. Ili uwe bilionea unapaswa kuiuza kwa watu bilioni moja na unapaswa usitumie hiyo fedha. Hahaha.

Ukiuza bidhaa hiyohiyo kwa dola mbili basi utapaswa kuiuza kwa watu milioni mia tano (500).

Ukiiunza kwa dola kumi maana yake utapaswa kuiuza kwa watu milioni mia.

Ukiwa na bidhaa mbili za aina hiyo maana yake utapaswa kuziuza kwa watu milioni hamsini mara mbili. Ukiwa na bidhaa tatu, utaziuza kwa watu milioni 33.3 mara tatu.

Kwa hiyo wewe, unaweza kuangalia namba ipi unaweza kupambania. Lakini pia soma hapa kuna mbinu zaidi

Kama nilivyoeleza hapo mwanzo. Ubilionea siyo kitu cha kulala na kuamka ukiwa umekifia. Ni kitu kinachukua muda.

Mabilionea wengi wamefikia kiwango cha ubilionea baada ya kufanya kazi kwa miaka 20 au zaidi.

WARREN Buffet ni miongoni mwa mabilionea maarufu kwa sasa. Ila bilionea huyu anasemekana kuwa alianza kuwekeza akiwa na umri wa miaka 11 na aliendelea kuwekeza kila mara. Ila alikuja kuufikia ubilionea akiwa na miaka zaidi ya 50.

Ebu fikiria hili na ujipange vizuri kwa ajili ya mchezo huu wa kuufikia ubilionea, Ila hili lisikukatishe tamaa.

Kwa hiyo nikate tamaa ya kupambania ndoto yangu ya ubilionea kwa sababu unachukua muda kuufikia?

Unachopaswa kufahamu ni kuwa miaka 20 inaenda kupita. Sasa ikipita ni au utakuwa umeitumia kwa manufaa au umeitumia hovyo. Kama umeitumia kupambania ndoto yako ya ubilionea utakuwa umepiga hatua kubwa sana hata kama utakuwa haujaufikia ubilionea, Ila utakuwa umefika mbali.

Ila ukikata tamaa hata kabla ya kuanza. NI wazi kuwa hata umilionea utakushinda. Utashindwa hata kuwa lakionea, hahaha.

JE, UNA MPANGO WA KUWA BILIONEA au kufikia ndoto yako kubwa?
karibu ujiunge na kundi letu la THINK BIG FOR AFRICA.

BONYEZA HAPA KUJIUNGA

AU WASILIANA NAMI KWA 0755848391

Makala nyingine zinazohusiana na hii

,

4 responses to “Bilionea Ni Mtu Wa Aina Gani?”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

X